Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Interview 10

1.Unaishi sehemu gani?!

Keko mwanga 'A'

2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!

Kuboresha miundo mbinu,mfano mfereji mkubwa kupanuliwa,mifereji midogo midogo ijengwe itakayotiririsha maji kwenye mfereji mkubwa.

3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!

  • Vitu vyote vya ndani vimeharibika.
  • Nyumba imebomoka ukuta.
  • Mifugo kama kuku,bata imekufa baada ya kusombwa na maji.

4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!

  • Magonjwa mlipuko kutokana na uchafu wa maji taka kuzingira nyumba yangu.
  • Kuishi mazingira hatari baada ya ukuta wa nyumba yangu kubomoka hivyo kulala sehemu hatarishi.
  • Nimepoteza rasilimali.

5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!

Vyanzo vya maji mtaani kwetu vyote vimeharibika hivyo kukosa upatikanaji wa kira maji safi na salama.

6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!

January 31, 2012
« Previous Next »

Comments (3)

Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
.Wakazi wa Eneo la keko wanahitaji kuboreshewa miundo mbinu kutokana na maeneo mengi kuharibiwa na maji.
.Kwa waliopoteza rasilimali,mitaji,vifaa vya kazi watafutiwe njia ya kuwawezesha waanze upya kwenye shughuli zao za kazi,kuepusha uhaalifu utaohatarisha maisha ya wananchi wengine.
January 31, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
.Kufanyike utaratibu wa kumwaga dawa sehemu ambazo bado maji yametuama ili kuzuia magonjwa mlipuko katika maeneo hayo.
Kugawa vyandarau ili kuepusha wakazi katika eneo la keko kupata ugonjwa wa Malaria.
.
January 31, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
.kutokana na Serikali kuruhusu ujenzi wa nyumba bila mpangilio,ufanyike utaratibu maalumu wa kuhamisha watu walio kwenye mazingira hayo duni.
Kiwanda cha Ruby kimechangia kwa asilimia 40 kusababisha mafuriko katika maeneo ya keko kwasababu ya kuziba mfereji mkubwa wa maji kwa lengo la kufanya ulinzi katika kiwanda hicho,hivyo serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha kero hii inatoweka.
January 31, 2012

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.