Interview 9
1.Unaishi eneo gani?!
Keko magulumbasi 'A'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Sehemu maalumu ya kuweka taka ili uchafu usizibe mifereji ya maji
- Kujengwe mifereji midogo midogo itakayowezesha kupitisha maji nyumba hadi nyumba.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
- Nimepoteza vifaa vyangu vya kazi kwa maji,nilikua mama ntilie.
- Vifaa vya ndani vyote kuharibika kama friji,tivi,redio,makochi na nguo zangu na za watoto.
Vifaa vyote vya shule vya watoto kuharibika.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
Sina ajira kutokana na vifaa vyangu vya kazi kupotea.
Watoto kukosa vifaa vya shule,kushindwa kulipa ada kutokana na uchumi wangu kushuka sina ajira.
5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Kisima cha jirani tulipokua tunachota maji kuharibika,inatulazimu kwenda mbali kutafuta maji ya kununua kwa gharama ambayo sina uwezo nayo.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Wakati nimejiajiri ilikua hainichukui muda wowote maana sehemu ya kazi ilikua nyumbani,sasa sina ajira.