Fungua
TANZANIA YOUTH NEW FASHION

TANZANIA YOUTH NEW FASHION

Tabora, Tanzania

Taarifa ya kazi ya uandaaji wa PD Budget iliyofanyika jijini dar kuanzia tarehe 10th2012-12th 2012

somo hapo juu lahusika

Napenda kutoa taarifa ya kazi iliyofanyika jijini DR LENGO KUU LIKIWA NI UANDAAJI wa budget, pd pamoja na........................... Kwa ajiri ya mwaka  mpya unaoanza mwezi 10 -2013 staff walio husika katika uandaaji wa kazi hizo ni Poul Sipemba(Director) robert Masele (program Accountant) Agatha NSWILA (M&E) PAMOJA NA Kokuhabwa Byarugaba (program Officer)

 

RATIBA AMBAYO INAONYESHA SIKU VIKUNDI VYOTE VYA WORTH KATIKA KILA KATA VINAOKUTA NA WAWEZESHAJI WAO.

MWEZESHAJI

KITUO KANDA AMBAPO KIKUNDI KULIPO

MWAKA

Hitimisho. Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kabisa toka ndani ya mioyo yetu kama watumishi wa AICT/CCT pamoja tuwalee kwa meneja na uongozi mzima wa shirika la hifadhi la jamii la NSSF. Sintakuwa mwema wa fadhila na shukurani kamasinto wataja kwa majina maafisa toka hifadhi ya jamii mkoani tabora shirika la NSSF kwa kutuunga mkono katika harakati zetu za kuikomboa jamii kupitia elimu, malazi na kazi, afya, pamoja na ujasilimali msaada wa kisheria pia msaada wa kisaikolojia kwa jamii. Mr ........................ kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika zoezi hili zima la kutembelea na kuvipa elimu vikundi vyetu vya WORTH kwa lengo zima la kuikomboa jamii katika dimbwi la umasikini uriokithiri ndani ya jamii. Kama mshauri wa mradi wa huu wa pamoja tuwalee nawapongeza staffs wote yaani project coordinator, Program officers pamoja na mhasibu kwa ushirikiano wao uriotukuka katika zoezi zima la kuwapa elimu wanajamii wetu kupitia mpango mzima wa WORTH JINA LA BAWA LIBALIKIWE

Chanhamoto. Katika kila suala lolote la maendeleo katika jamii yote ile changamoto ni suala ambalo haliepukiki katika mtizamo wa mpango ambo ni yakinifu kwa usitawi wa maendeleo ya kijamii.

- Uelewa mdogo wa elimu kwa baadhi ya wanavikundi. Hapa wanavikundi wetu wengi hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya huduma zitilewazo na NSSF.

-Idadi ndogo ya wanavikundi wakati wa zoezi hili la kuelimisha na kuhamasisha jamii ijiunge na mfuko wa hifadhi ya jamii ya NSSF.

Suluhisho. Suala la elimu ni jambo muhimu sana kwa jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla. Kwani watu wawapo na afya zao njema kabisa hii itawasaidia pia hata wao kufanya kazi zao kwa ufanisi kwani watakuwa na afya njema. Kama shirika la AICT tutaendelea kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika kuisaidia jamii yetu hii haswa wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Mafanikio. Hakuna kitu kinachofanyika katikkak jamii yeyote ile kisicho kuwa namafaniokio ni jambo la kushukuru mungu kwa mafanikio ni makubwa sana kwa usitawi na maendeleo ya jamii.

- Idadi ya wanavikundi wote ni 464 ambapo ni jumla ya vikundi 27 toka katika kata zote tano za mpango wa WORTH. Ambapo ni watu 300 wameweza kujiunga na fuko wa hifadhi ya jamii ya nSSf kama wanachama mabao tunategemea watapata huduma ya matibabu katika hospitali mbalimbali  za hapa Tabora na kwingineko kulingana na tatizo husika pia zaidi ya watoto 2000 wataweza kunufaika kupitia mpango huu.

-Wanavikundi waliojitokeza wote walriweza kujiunga na kuwa wanachama wa NSSF ambapo kila mwanachama atachangia elf 16 kwa miezi mitatu tunaamini wataweza kwani WORTH itawasaidia kupitia vikundi vyao pia mkopo wa nssf utawasaidia katika kukuza mitaji ta biashara zao.

-Pia idadi ya wakina mama wengi zaidi wariweza kuhasika nakujiunga na mpango huu kupitia NSSF imetia hamasa kubwa sana takribani vikundi vinne vimeweza kuundwa kupitia mpango wetu huu ambapo mbugani vikundi viwili na ngambo kikundi kimoja pia isevya kikundi kimoja hii ni hamasa kubwa na jamii ineitikia vizueri.

-Suala la mkopo kupitia saccoss watakazo unda wanavikundi hii ni faida kwetu kwani hii itawasaidia kuongeza mitaji yao kwa ajiri ya buiashara zao pia wakitumi fursa ya vikundi vya WORTH ambavyo vitakuwa kama vikundi mama vya kuirea ile saccoss yako.

-Pia shirika la hifadhi ya la jamii limeweza kutupatia shiling lakini moja na nusu Tsh 1500000 kama mchango katika kusaidia jamii, kwani wamehamasika sana kupitia mchakato wetu huu kwa kupitia vikundi vya wORTH. Hii itakuwa ni njia nzuri kwa mashirika mengine kuhamasika pia na kutuunga mkono katika harakati zetu za kuona jamii inasaidiwa na iwe na maisha bora kupitia mradi wa pamoja tuwalee.

 

Mpango huu wa WORTH umelenga kushirikiana na wadau mabalimbali wa maendeleo kwa lengo la kuisaidia jamii inayoishi katika mazingira hatarishi. Tumeshirikiana na shirika la hifadhi ya jamii la NSSF lengo likiwa ni kuisaidia jamii kupitia vikundi vyetu vya WORTH ambapo tunalenga kuwasaidia akina mama wanaohudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wajiunge na NSSF ili waweze kupata sifa au vigevyo vya kuwa wanachama ambapo sasa wataweze kupata huduma ya matibabu  kupitia NSSF wao na familia zao.NSSF wanatoa huduma nyingi sana katika jamii lakini sisi tumelenga huduma chache ambazo ni faida kubwa kwetu kwa lengo la kiusaidia jamii ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi kupitia mpango wa WORTH.

Huduma ya matibabu: Hapa lengo kubwa ni kuona akina mama pamoja na familia zao wanapata huduma ya matibabu kwa haraka na bei nafuu zaidi kwa, kuchangia michango mitatu ya miezi ya kwanza. Hudumaa hii wataipata kupitia NSSF ambapo shirika hili limeingia mikataba na hospitali mabalimabali hapa nchini. Tabora ni pamoja na kitete hosipitali, St philipo hosipitali, St anna hosipitali, Urambo hospitali, Sikonge hospitali, Ndala hospitali, Nkinga hospitali hii itawasaidia wanachana wa WORTH kuchagua hospitali yeyote ili wapate maibabu. Pia endapo hospitali hizo zitashindwa kuwatibu basi watapewa rufaa kwenda hospitali kubwa mfano Buganda mwanza, k.c.m.c na mhimbili hospitali. Hii itatusaidia kama shirika katika kufikia watu wengi zaidi kwani huduma ya CHF kadi itabidi wale ambao hakuna mpango wa WORTH kupitia kaya zao watapata hizo kadi wakadi na tutakuwa tumevuka lengo la kuwapatia huduma watoto hao kupitia mpango wetu wa PAMOJA TUWALEE.

Msaada wa mshazi: Shirika la hifadhi ya jamii pia linatoa marejesho ya gharama za mazishi kwa wanachama wake, hii ina maana kwamba mwanachama atazikwa kwa heshima ya shirika la hifadhi ya jamii NSSF KWA KURUDISHA gharama za mazishi. Pesa hii italipwa ndani ya miezi miwili  yaani siku sitini 60 ambapo ndugu wa marehemu wanatakiwa wakatoe taarifa kwa shirika la NSSF.

Gharama za uzazi: Shirika la hifadhi pia linatoa mafao ya uzazi kwa wanachama wake,ambapo  mwanachama wake atalipwa pesa ya miezi mitatu. Mwanachama anatakiwa akatoe taarifa kwenye shirika tangu kungundulika kwa uja uzito ili sasa shirika ripange utaratibu wa kumpatia mafao ya matibabu kwa wakati. Hivyo mpango huu utakuwa ni msaada mkubwa kwa mabiti wanaolea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pia tutakuwa tumeipatia elimu kubwa jamii kupitia mradi wetu.

Mikopo kupitia SACCOSS. Shirika la hifadhi pia linatoa mikopo kwa saccoss ambazo zinatambulika kisheria. Suala hili kama maafisa wa shirika tumeona ni vyema wanavikundi waundi kikundi kimoja ambacho kitatengeneza SACCOSS ili NSSF watupatie mkopo ila suala la vikundi vya WORTH in lazima viendelee kama kawaida na kukuchangishana kupitia vikundi vyao. Mkopo ni msaada wa ziada ili umsaidie mwanachama wetu kuinua kipato chako lakini hatuna mpango wa kuuwa WORTH groups.  Wanachama vikundi wa WORTH watanufaika kwa namna moja au nyingine kwani mikopo hiyo itawasaidia katika kujinuria kipato

 

MUHUTASALI WA KIKAOO CHA USAIHILI WA WAWEZESHAJI KUTOKA KATA SABA ZA MANISPAA YA TABORA.

Kikao kilifunguliwa mida ya saa tatu asubuhi na mratibu wa mradi wa pamoja tuwalee kwa kuwakaribisha wafanyakazi wa shirika la Aict pamoja na Muwezeshaji kutoka pact tanzania, watendendaji wa kata saba za manispaa pamoja na afisa usitawi wa jamii manispaa ya tabora. Baada ya hapo muwezeshaji kutoka AICT pamoja tuwalee alisoma maada za kikao hicho kilichotanguliwa na kuuelezea maana nzima ya mpango wa worth, na baadaye zoezi la usaili.

AGENDA ZA KIKAO.

1.  Maana nzima ya mpango wa worth

2. Usaili wa wawezeshaji kutoka kata saba za manispaa ya Tabora.

3. Mengineyo.

Maana nzima ya mpango wa worth

Worth ni mpango wa dhamani ambao unalenga kuwainua wanawake kielimu na kiuchumi katika ngazi ya kaya au familia. Mpango huu unalenga zaidi kuwasaidia akina mama wanaoishi katika mazingira hatarishi na mpango huwa hautoi kianzio chochote kwa wanavikundi isipokuwa ni elimu tu kwa wanavikundi ni jinsi gani wataweza kujiunga na kujipatia kipato chao wenyewe, pasipo kutegemea msaada wowote ule. Worth kama mpango maalumu huwa una vyao vyake vya mapato ambapo mapato hayo yanatokana na makubaliano ya wanachama wenyewewe. Wanachama wa vikundi wawo wenyewe huuda vikundi na kuchagua uongozi wao wenyewe ambapo uongozi huwa na, Mwenyekiti wa kikundi, Katibu, mtundha hazina na mtdibiti wa fedha. Ambapo sasa kama kikundi hukubalia wao wenyewe kuwa kima chao cha chini kitakuwa shilingi ngapi kutegemeana na kipato na makubaliano ya wanachama. Mwezeshaji toka pact alienze kwa kiima kuwa vyazo vya mapato huwa vipo vya aina mbili kupitia kwa wanachama wenyewe ambavyo ni, akiba ya hiari na akiba ya lazima huwa kama mtaji wao kwa wanavikundi.

Akiba ya hiari hapa ni kwamba mwanchama mwenyewe anatoa pesa yeyote anayoona anaweza kuotoa kuiwekeza kwenye kikundi na kwa kuja kijitabu maalumu. Hapa mwanacha atakuwa anajua idadi ya pesa yake pia ana uhuru wa kuichukua pindi aihitajipo,

Akiba ya lazima. Kikundi hapa hupanga akiba ya lazima kwa kila mwanakikundi mabapo kila kikundi wakutanapo pesa hivyo hukusanywa na kuandikwa kwenye kujitabu maalumu kama akiba ya mwanachama. Na huo ndo huwa mtaji wao na pesa zote huhesabiwa mbele ya kikundi na wanavikundi hukopeshana pesa hiyo kw awamu kadiri ya mpango mzima na matakwa ya kikundi hussika,

Muwezeshaji toka pact pia alisisitisa watendaji wa mtaa wahusike sana na pia waujue mpango mzima wa worth na mtaalaum wa au msimamizi wa worth kutoka Aict alisisitiza pia kuwa watendaji wanao nafasi kubwa sana katika kusisitiza pia kuhamasisha wamama wanatoka mazingira hatarishi wajiunge na mpango huu wa worth.

2.Usaili wa wawezeshaji kutoka kata saba za manispaa ya Tabora.

Suala zima ririkuwa ni usaili wa hawa wawezeshaji wa katani katika kuhamasisha wamama wanaishi katika mazingira hatari. Mtalaamu wa au msimamizi wa mambo ya Woth kutoka shirika la AICT alitanabaisha mbele ya wanakikao kuwa jumla ya watu 60 waliomba kazi hiyo ya uwezeshaji. Lakini usaili wa awali uliofanywa kikamilifu na kwa kuzingatia sifa za vigezo jumla ya watu 21 walipita baada ya mchujo wa awali ambao ndio leo hii tutawafanyia usaili wa mwisho tupate watu saba tu kutoka watu 21. Hivyo basi zoezi la usali lilianza kwa watahiniwa wote 21 kufanya tena mtihani wa awali ambao ulikuwa ni wahesabu hapo watu 14 tu ndoo walikuwa wnatakiwa wawili wawili kutoka kila kata. Kigezo kilikuwa kila mtahiniwa apate juu ya alama thelathini ndoo aende kwenye usaili wa mahojiano.

Baada ya zoezi hili jula ya watu sita tu waliweza kupata alama juu ya thelathini ambapo walingia kwenye usaili wa mahajiano toka kata ya Gongoni, Kiloleni pamoja na mtendeni. Ndani ya mchakato huu aliweze kupatikana mtu mmoja tu toka kata ya Kiloleni aliyefuzu usaili wa mahojiano. Bi salima alionesha ukomavu na uelewa kwani alijibu maswali yake kwa ufasaha sana kuliko wezanke. Hivyo paneli nzima ya usaili ilikubali kuwa katika kata zote tatu mtahiniwa aliyesitahili ni moja ambaye anatoka kata ya kiloleni na walikubaliana kwa kuweka saihihi katika karatasi husika,

3. Mengineyo.

Wajumbe wote wlipendekeza watendaji wapewe japo nakala zinazoelezea maana ya worth ili iwe rahisi kwao kuielimisha jamii juu ya mpango mzima huu. Pia Mtendaji wa kata ya T/reli alipendekeza mpango huo pia ujumuishe hata watu ambao hawapo katika mazingira hatarishi lengo ni kuwainua wote kiuchumi na kipato.Pia wajumbe wote walikibaliana kwa kupitia watumishi wa shirika kuwa kata hizo sita mabazo ni kitete, malolo, Ipuli, Mtendeni T/reli pamoja na Gongoni itabidi watu waombe upya tena ambapo usaili wa wali tena utakuwa tarehe 4/09/2012

Hitimisho.

Kikao kilifunguwa na mtaalamu wa mambo ya worth kutoka shirika la aict kwa kuwapongeza na kuwashukuru wajumbe wote waliofika kwa ajiri ya zoezi zima la usaili na kwa ushirikiano wao mkubwa waliouonesha katika zoezi hilo.

 

 

 

Utambuzi wa watoto yatima

kazi za ofisini

kufuatilia maendeleo ya mradi pamoja na vikundi vya worth/, vyama vya kufa na kuzikana pamoja na club za michezo ya watoto.

shughuli za ofisini ikiwa ni pamoja na uandishi wa ripoti

kwa kutumia mvcc...wazazi na walezi wapwe mbinu juu ya uboreshaji uchumi katika familia zao kama vile kujiunga katika mpango wa worth(kuingia katika mpango wa worth) ili waweze kujiwekea akiba na kukopa na waweze kuanzisha biashara ndogo ndogo

 

shiriki

c)watoto wengi wana upunufu wa mahitaji muhimu kama vile, chakula, mavazi, vifaa vya shule na makazi yao sio mazuri

d)wananchi na jamii ishirikishwe (jamii ijihusishe) katika kutoa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi