Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

- kupeleka fomu za usajili wa familia zinazolea watoto walio katika mazingira hatarishi

-kufuatilia maendeleo na utendaji kazi wa kamati za watoto walio katika mazingira hatarishi na kuzijengea uwezo

-kutembelea na kuimarisha uhai wa vikundi vya worth na kuvijengea uwezo kiutendaji

 

kufuatilia shughuli zinazofanywa na kamati zinazo lea watoto yatima

(B)kufanya uhuishaji wa takwimu za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na mahitaji yao.Vilevile kujua ni watoto wangapi wamezidi umri wa chini ya miaka 18 na niwangapi wamesajiriwa kwa mara ya kwanza katika daftari la usajiri.

(C)Changamoto kubwa tuliokumbana nayo ni kutoka na geographia ya wilaya ya sikonge kuwa mbaya hivyo basi barabara nyingi zimekua zikipitika kwa shida sana .Vilevile kulingana na bajeti ya mradi posho iliyopangwa kwa wafunyakazi hazitoshi kabisa kulingana na halialisi ya kiuchumi na mazingira yakazi.

(D)Ningependa kuhushauri uongozi utpatie usafiri unao kidhi halialisi ya barabara  kulingana na geographia ya wilaya yetu.pia ningependa  kuushauri uongozi ujaribu kuongeza kiwango chaposho kwani kilicho pangwa  hakikidhi mahitaji kulinga na alialisi ya kiuchumi na mazingira yakazi.

(E)Kutokana na changamoto tulizo kumbanazo nimejifunza kutumia rasilimali zinzinizunguka kulingana na mazingila niliyopo.Vilevile kushirikiana na timu niliyonayo pale tatizolinapotokea hasa  kiutendaji.

(F) Posho aikidhi mahitaji kulinga na na mazingira ya kazi

-Usafiri aukidhi  mahitaji kulingana na geographia  ya barabara zetu.

(G)Kutokana na halialisi ya kiuchumi poshoingeongezwa kulingana na halialisi ya maisha na ugumu wa kazi.Vilevile tungepeda kutumia usafiri unao kidhimahitaji ya barabara zetu

(H)Pamoja na changamoto zotetulizokumbana nazotumefanikiwa kufikia kata nne kulingana na mgawanyo wa majukumu.Tumefanikiwa kuta mbulisha mradi mpya wa Pamoja Tuwalee katika kata na vijiji.

Tumefanikiwa kuwafikia wanakamati 64 kulingana  na kata,vijiji tulivyo tembelea.Vilevile tumefanikiwa kutoe mafunzo ya jinsi ya kujaza fomu za rufaa kwa watoto wanao ishi katika     mazingira hatarishi . pia tume toa  mafunzo juu ya jinsi ya kujaza fomu ya usajiri wa familia ,tathimini na mpangowa kutunza familia  yenye watoto wanao ishi kataka mazingira hatarishi na mahitaji yao.

-kuhuwisha takwimu za awali za watoto walio katika mazingira hatarishi

-kufanya usajili wa familia zinazolea watoto wenye uhitaji

-kutambulisha mradi wa pamoja tuwalee kutoka jali watoto

c)posho ya kujikimu wakati tunapokuwa field haitoshi

-usafiri haukidhi viwango kulingana na eneo husika la mradi

d)posho iongezwe kwa kufuata uahalisia wa eneo husika

-usafiri uboreshwe ili kuepuka usumbufu unasababisha kuchelewa kumaliza shughuli (kazi) kutokana na matatizo ya gari kama kuharibika tukiwa safarini kuelekea au wakati wa kurudi kutoka katika eneo la mradi

e)kutokana na kukutana na watu tofauti tofauti wenye mila na desturi tofauti nimeweza kujifunza namna ya kuishi au kufanya kazi na jamii moja au nyingine kwa kuendana na mazingira yao, mila na desturi zao. hii itanipa urahisi wa kufanya kazi zangu kwa kubadilika kulingana na eneo husika

f)posho

-usafiri

g)kwa upande wa posho tungependa iongezwe kwa kuangalia geografia ya wilaya yetu na ugumu wa kufikika..posho iliyopo sasa inatufanya tushindwe kufanya kazi vizuri kutokana na umbali wa maeneo yetu ya kazi, hivyo wakati mwingine tunalazimika kutumia siku nyingi katika eneo la mradi na kujikuta tunaishiwa fedha za kujikimu kabla ya kumaliza kazi (shughuli)

-usafiri-tungependa kuboreshewa chombo cha usafiri au kubadilishiwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kama gari kuharibika katikati ya safari, hii inachelewesha muda na pia kushindwa kumaliza kazi mapema kwa sababu zinazoweza kushughulikiwa.

 

h)kulingana na ukubwa wa shughuli ya kuhuwisha takwimu, usajili na utambulisho wa mradi wa pamoja tuwalee katika wilaya ya sikonge na kata zake, tumefanikiwa kutekeleza shughuli zote kana ilivyoainishwa pasipo kikwazo kikubwa chenye madhara kuacha matatizo madogo madogo yanayoweza kushughulikiwa.

katika shughuli zote zilizopangwa kutekelezwa kwa kipindi hiki hakukuwa na ugumu uliojitokeza ambao ungeweza kuleta kukwazo kwa namna moja au nyingine  jambo hili ni la kuleta faraja kwangu mimi katika utendaji wangu wa kazi za kila siku, kwa shirika, lakini pia kwa uongozi wa vijiji tulivyovitembelea na kamati za watoto walio katika mazingira hatarishi.

Aidha kwa kuonesha kuwa wapo mstari wa mbele katika kupiga vita umasikini kwa kukubali kwamba watoto wote ni wetu hivyo kwa pamoja tuwalee viongozi wa vijiji ameahidi kuwa pamoja na TYNF katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi wa Pamoja atauwalee wakiwa kama wadau ngazi za jamii.

Jambo hili ni ishara ya kwamba jamii sasa imeelewa kwamba mtoto ni wa kila mwanajamii na kwamba wanapaswa kusimamia haki za mtoto ikiwa ni pamoja na kumlinda. Haya ni mafanikio na dalili njema katiak juhudi za kutimiza malengo yetu ya kuona yale makundi yaliyosahaulika haswa watoto walio katika mazingira hatarishi wanapata elimu na wanakuwa na maisha bora.

 

-

Planned activities....actual implementation and comments

umejifunza nini..ainisha vipengele muhimu vya kufanyiwa marekebisho

FOMU YA TAARIFA YA MWEZI KUTOKA FIELD

1.Jina la shirika 2.jina la mradi 3.wilaya 4.imetayarishwa na 4.tarehe 5.imepitishwa na

-vijiji vilivyotembelewa, lengo la matembezi 3. changamoto zilizojitokeza 4. kutokana na changamoto hizo unapendekeza nini kifanyike? 5. ni jambo gani jipya ililojifunza? 6. ainisha vipengele muhimu vya kushughulikiwa 7.unafikiri liboreshwe vipi? 8. hadithi ya mafanikio

lengo la shirika letu ni kutokomeza vikwazo vya maendeleo na kuhakikisha kila binadamu anaishi maisha bora, hasa makundi yaliyosahaulika katika jamii na yanayoishi katika mazingira hatarishi.

ikiwa jamii inatambua ya kwamba watoto ni wetu sote kwanini isijitoe kuwalea? hii inaonesha kwamba jamii inathamini zaidi watoto wao wa kuwazaa na kuwaacha wengine wakitaabika hivyo kauli ya pamoja tuwalee inabaki kama msemo tu tena usio na faida yoyote kwa taifa, hii inafanya taifa kuzidi kuwa masikini kwani pengine hao tunaowaacha wangesoma wangeweza kuwa mawaziri au hata viongozi wakubwa katika ngazi za juu.

Kulingana na ukubwa wa tatizo la watoto walio katika mazngira hatarishi serikali na wadau wengine wametakiwa kufuatilia kwa ukaribu kumbkumbu za watoto waliosajiliwa awali ili kujiridhisha na usahihi wa takwimu za awali na takwimu mpya.