Log in
TANZANIA YOUTH NEW FASHION

TANZANIA YOUTH NEW FASHION

Tabora, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Mpango huu wa WORTH umelenga kushirikiana na wadau mabalimbali wa maendeleo kwa lengo la kuisaidia jamii inayoishi katika mazingira hatarishi. Tumeshirikiana na shirika la hifadhi ya jamii la NSSF lengo likiwa ni kuisaidia jamii kupitia vikundi vyetu vya WORTH ambapo tunalenga kuwasaidia akina mama wanaohudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wajiunge na NSSF ili waweze kupata sifa au vigevyo vya kuwa wanachama ambapo sasa wataweze kupata huduma ya matibabu  kupitia NSSF wao na familia zao.NSSF wanatoa huduma nyingi sana katika jamii lakini sisi tumelenga huduma chache ambazo ni faida kubwa kwetu kwa lengo la kiusaidia jamii ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi kupitia mpango wa WORTH.

Huduma ya matibabu: Hapa lengo kubwa ni kuona akina mama pamoja na familia zao wanapata huduma ya matibabu kwa haraka na bei nafuu zaidi kwa, kuchangia michango mitatu ya miezi ya kwanza. Hudumaa hii wataipata kupitia NSSF ambapo shirika hili limeingia mikataba na hospitali mabalimabali hapa nchini. Tabora ni pamoja na kitete hosipitali, St philipo hosipitali, St anna hosipitali, Urambo hospitali, Sikonge hospitali, Ndala hospitali, Nkinga hospitali hii itawasaidia wanachana wa WORTH kuchagua hospitali yeyote ili wapate maibabu. Pia endapo hospitali hizo zitashindwa kuwatibu basi watapewa rufaa kwenda hospitali kubwa mfano Buganda mwanza, k.c.m.c na mhimbili hospitali. Hii itatusaidia kama shirika katika kufikia watu wengi zaidi kwani huduma ya CHF kadi itabidi wale ambao hakuna mpango wa WORTH kupitia kaya zao watapata hizo kadi wakadi na tutakuwa tumevuka lengo la kuwapatia huduma watoto hao kupitia mpango wetu wa PAMOJA TUWALEE.

Msaada wa mshazi: Shirika la hifadhi ya jamii pia linatoa marejesho ya gharama za mazishi kwa wanachama wake, hii ina maana kwamba mwanachama atazikwa kwa heshima ya shirika la hifadhi ya jamii NSSF KWA KURUDISHA gharama za mazishi. Pesa hii italipwa ndani ya miezi miwili  yaani siku sitini 60 ambapo ndugu wa marehemu wanatakiwa wakatoe taarifa kwa shirika la NSSF.

Gharama za uzazi: Shirika la hifadhi pia linatoa mafao ya uzazi kwa wanachama wake,ambapo  mwanachama wake atalipwa pesa ya miezi mitatu. Mwanachama anatakiwa akatoe taarifa kwenye shirika tangu kungundulika kwa uja uzito ili sasa shirika ripange utaratibu wa kumpatia mafao ya matibabu kwa wakati. Hivyo mpango huu utakuwa ni msaada mkubwa kwa mabiti wanaolea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pia tutakuwa tumeipatia elimu kubwa jamii kupitia mradi wetu.

Mikopo kupitia SACCOSS. Shirika la hifadhi pia linatoa mikopo kwa saccoss ambazo zinatambulika kisheria. Suala hili kama maafisa wa shirika tumeona ni vyema wanavikundi waundi kikundi kimoja ambacho kitatengeneza SACCOSS ili NSSF watupatie mkopo ila suala la vikundi vya WORTH in lazima viendelee kama kawaida na kukuchangishana kupitia vikundi vyao. Mkopo ni msaada wa ziada ili umsaidie mwanachama wetu kuinua kipato chako lakini hatuna mpango wa kuuwa WORTH groups.  Wanachama vikundi wa WORTH watanufaika kwa namna moja au nyingine kwani mikopo hiyo itawasaidia katika kujinuria kipato

 

September 3, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.