Injira
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MDAHALO WA VIJANA WARUDI KWA KASI MPYA NA MAARIFA ZAIDI.

Timu iliyoundwa kufanya uzinduzi wa mdahalo wa vijana uliobadilisha vikao vyake kutoka kila jumamosi na kuwa mara moja kwa mwezi ilifanya vizuri kwa kufikia 60% ya malengo yaliyowekwa katika kikao cha kamati ya utendaji cha TEYODEN cha hivi karibuni.Mdahalo huu uliohudhuriwa na vijana wapatao 70 na kuwezeshwa na bwana Ismail Mnikite ulifana sana ingawa ulichelewa kidogo kuanza.Mada ya mdahalo ilikuwa ni Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo na mada ndogo juu ya masuala ya katiba.Katika mada ya ushirikishwaji vijana waliweza kubungua bongo,kukubaliana na kujifunza maana ya ushiriki,ushirikishwaji na maana ya uwajibikaji.Pia walifunza masuala ya msingi ambayo vijana wanapaswa kushiriki ipasavyo,stadi za kujenga ili kuimarisha ushiriki wenye tija na wenye matokeo.

Mwisho wa Mada washiriki na mwezeshaji walikubaliana kuhairisha mada ya katiba ili irudiwe katika mdahalo wa mwezi wa 3(machi)

mdahalo ulitanguliwa na ufunguzi wa mwenyekiti taratibu za kushiriki na masuala ya utangulizi kutoka kwa kamati ya maandalizi na katibu wa TEYODEN.

 

Pichani juu:Wanajamii wakipata maelezo kutoka kwa mweka hazina msaidizi wa TEYODEN bi Prisca Moses juu ya V.V.U/UKIMWI Katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika viwanja vya Zakhiem mbagala Charambe.Pichani chini:mama mwenye kofia Mgeni rasmi wa maadhimisho ya Ukimwi duniani Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke akipata maelezo ya shughuli za TEYODEN kutoka kwa afisa habari wa TEYODEN bwana Hamphrey Shao.

Vijana washiriki maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika tarehe 2 disemba 2011 viwanja vya Zakhiem Mbagala Charambe

Takribani vijana 60 wanachama  na Viongozi wa mtandao wa vijana Manispaa ya Temeke wameshiriki maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo mwaka huu yamefanyika katika viwanja vya Zakhiem kata ya Mbagala.Maadhimisho hayo yaliyopambwa kwa vikundi mbalimbali vya sanaa za ngoma na maigizo yanayolenga kuhimiza jamii dhidi ya hatua za kudhibiti maambukizi,kutoa hudua kwa waathiriwa na waathirika wa ukimwi,upimaji kwa hiari,matumizi ya kondom na hatua za uboreshaji wa sera zinazohusu ukimwi yalianza kwa maandamano mafupi yaliyopokelewa na mgeni rasmi Naibu meya wa Manispaa ya Temeke.

Kazi za TEYODEN

TEYODEN katika banda lake ilifanya kazi zifuatazo:-

  • Kuelimisha jamii hasa vijana juu ya umuhimu wa stadi za maisha kama nyenzo ya kubadili tabia hatarishi kwa vijana.
  • Kutoa huduma ya kondom bure
  • Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli za upunguzaji wa maambukizi na utoaji huduma kwa wagonjwa.
  • Kuhamasisha jamii juu upingaji wa unyanyasaji wa wanawake hasa vijana na kujenga uwezo wa kina mama wadogo kukabiliana na changamoto zitakazo wapelekea katika maambukizi ya ukimwi.

Mafanikio

  • Wanajamii 78 wakiwemo vijana 56 walitembelea banda na kujifunza masuala muhimu ya upunguzaji wa maambukizi na utoaji huduma kwa waathirika na waathiriwa wa ukimwi
  • Idadi ya kondom 371 zilisambazwa kwa vijana na wanajamii walioudhulia maadhimisho
  • vijarida 217 vilisambazwa kwa vijana na wanajamii waliohudhuria maadhimisho

Mwisho wa maadhimisho haya ni mwanzo wa michakato na mipango mipya juu ya uthibiti wa maambukizi mapya na huduma kwa waathiriwa na waathirika wa Ukimwi.Kila mtu achukue nafasi yake sasa hivi na hapo hapo alipo.Tusiufundishe ulimwengu kuimba tuonyeshe kwa vitendo.

Vijana kutoka TEYODEN wakiwa katika picha ya pamoja katika kikao cha Climate change Don Bosco upanga Dar-es-salaam

Vijana TEYODEN washiriki maadhimisho ya Climate Change Don Bosco,Upanga Dar-es-salaa.

Vijana 20 TEYODEN ( wanaume 10 na wasichana 10) washiriki katika Maadhimisho ya climate change Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya

Don Bosco Upanga   tarehe 8/11/2011

Lengo la mkutano wa Mabadiliko ya hali ya mazingira

  • Kuwaaga vijana wa kitanzania ambao wataambatana na vijana wenzao kutoka nchi 13 duniani kote na nchi zitakazo wakilishwa ni ;-Tanzania, Bangladesh,Botswana,Kenya, Uganda, Kongo drc, Zambia,South Africa,Norway, England, Nigeria, Senegar na Malawi.
  • Kukusanya matamko ya vijana wa kitanzania na yale yajumuiya ya dini ya kikristo pamoja na baraza kuu la waislam tanzania BAKWATA.
  • Kutiwa saini matamko au makubaliano hayo na makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal ambaye pia ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo.
  • Kuwatambulisha vijana wengine walio katika safari inayojukana kama Road to Durban watakaohudhulia mkutano mkuu wa climate change utakao fanyika Durban nchinia africa ya kusini .

Katika hotuba yake mgeni rasmi makamu wa raisi Dr Bilal alisema “ Wanadamu tumechafua nyumba zetu sisi wenyewe, hivyo basi nasisitiza kwamba kama tunataka mabadiliko ya kweli ni lazima tuanze kwa kusafisha nyumba zetu tulizo zichafua ndipo tusafishe mazingira yetu.”

Mkutano huu au maazimio uliudhuriwa na vikundi mbalimbali vya burudani navyo ni kikundi mcha sanaa za monesho ya jukwaani na televisheni cha FATAKI kikundi cha vijana wa kusheki mwanamuziki kutoka kenya anayejulikana kama Juliani ambao ni mmoja wa vijana walio katika safari ya road to Durban mwanamuziki wa Tanzania anayeimba mziki wake katika maadhi ya bongo flavour Mwasiti kikundi cha muziki kinacho julikana kama 10 Norway nacho pia kipo katika road to durban na kundi la ngoma ama muziki wa asili kutoka Botswana nao pia wapo katika Road to Durban

 

Zantel na TEYODEN wafanya programu ya ushirikiano ili kuwezesha vijana kuongeza kipato chao na kuwa na uwezo kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Vijana wa kata ya kilakala wamefanya kikao cha pamoja na katibu mtendaji wa TEYODEN na mhamasishaji jamii wa kampuni ya ZANTEL.Lengo la kikao ni kufanya majadiliano ya pamoja na kukubaliana juu ya ushirikiano wa pamoja kati ya pende hizo mbili.mhamasishaji wa ZANTEL alieleza kuwa vijana wanaweza kujiunga na kampuni hiyo ya simu na kupata faida ya asilimia zaidi 10 kwa uuzaji wa bidhaa za kampuni hiyo wakati pia wakiongeza pato lao kama kikundi.Akiongeza maelezo ya mhamasishaji bwana Katibu mtendaji wa TEYODEN bwana Yusuph Kutegwa aliwataka vijana wa Kilakala kuwa mfano kwa kulichukulia maanani suala hili la kijasiriamali ili kuleta tija kwa vituo kuliko kukaa na kuwezeshana kielimu pekee.Zoezi hili la Vikao na vijana litaendelea katika kata za Azimio,Mtoni,Mbagala,Toangoma,Kibada,Vijibweni na pemba mnazi.

TEYODEN yafanya mafunzo ya VICOBA kwa wasichana  80 waliozaa chini ya umri na waliosahalika na jamii (Ma mama wadogo) kutoka katika kata 4 za Azimio,Mtoni,Kibada na Vijibweni.Pamoja na walengwa hao walikuwepo mentors(walezi wa wasichana katika kata) 16 nao wakipata elimu hiyo ya VICOBA.Mafunzo hayo yalitanguliwa na mafunzo ya mafunzo ya siku 2 kuhusu stadi za maisha na elimu ya ujasiriamali yaliyofanyika kwa wasichana katika kata nne za mradi zilizotajwa hapo awali.Akifungua mafunzo afisa wa maendeleo ya vijana wa Manispaa ya Temeke aliwataka vijana kuwa watulivu na wasikivu na kuyafanyia kazi mafunzo watakayopata ili waweze kuibua miradi katika vikundi vya watu 10 ambavyo vitawezeshwa mitaji na ofisi ya TEYODEN.

"Nawapongeza sana TEYODEN kwa kuwa na wazo la kubuni mradi huu kwa kuwa mwanzoni katika vikao vyao vya miradi iliyopita niliwasahuri kufanya mradi tangible(wenye matokeo ya kuonekana) haya ni matokeo ya kuufanyia kazi kwa vitendo ushauri niliyowapa."alisema bi Afisa vijana bi Anna Marrica

 "Mradi huu wa mama wadogo waliosahaurika utawawezesha wasichana husika kupata elimu,kujadili changamoto za maisha yao ya kila siku na baadae kupatiwa mitaji kwaajili ya miradi yao itakayoibuliwa katika vikundi.Mtumie mitaji kwa shughuli zilizokusudiwa na si vinginevyo."aliongeza bi Anna Marrica

Wawezeshaji katika mafunzo haya walikuwa ni bwana Issa Tunduguru ambae ni Mkurugenzi wa Shirika la Poverty Fighting Tanzania na bwana Ally Manjasi ambae ni mkurugenzi wa Fedha wa shirika hilo.

Katika mafunzo hayo pia tulipata wageni kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam na mwanafunzi kutoka ujerumani ambae yupo Tanzania kujifunza kwa vitendo kazi za kijamii.

 

MENTORS(walezi) wa wasichana wa mradi wa kujenga uwezo wa wasichana waliosahaurika wakiwa katika picha ya pamoja na msimamizi wa mradi,mratibu na wawezeshaji wa mafunzo hayo large.jpg