Parts of this page are in Swahili. Edit translations
-
HISTORIA NA KUANZISHWA KWA TEYODEN
Vijana nje ya shule Duniani kote na Tanzania ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa V.V.U.Sababu hasa zinatokana na mazingira wanayoishi.Lakini pia vijana wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kutokana na kutokuwa na mbinu na uelewa wa kutosha wa kupambana na changamoto za makuzi yao.Matokeo ya hayo yote ni maambukizi ya V.V.U.
Kadili vijana wanavyoambukizwa V.V.U na kuwa wagonjwa ndivyo familia zao zinavyozidi kupoteza nguvu kazi.
Suluhisho la haya yote ni kuwapa vijana stadi za kukabiliana na changamoto za kila siku katika makuzi yao.Kwa maneno mengine kuwapa vijana elimu ya stadi za maisha.
-
PROGRAMU YA VIJANA NJE YA SHULE NA KUUNDWA KWA TEYODENProgramu ya vijana nje ya shule ni mradi uliofahiliwa UNICEF na kutekelezwa na wilaya 19 nchini Tanzania, Temeke ikiwa ni moja kati ya wilaya hizo.Mwaka 2001 TEYODEN ilianzishwa kama matokeo ya programu hiyo.TEYODEN ni kifupi cha maneno Temeke Youth Development Network.TEYODEN ilisajiliwa chini ya Majina ya Makampuni mwaka 2003 na mwaka 2007 imesajiliwa katika Ofisi ya Makamo wa Raisi.Mtandao unaratibu kazi zake katika vituo 24 vya vijana Manispaa ya Temeke.Kwa sasa Manispaa ya Temeke imeongeza kata 6 na hivyo kufanya idadi ya kata 30.TEYODEN inapanga kutanua wigo wake wa kazi na kuzifikia kata zote 30.