FCS Narrative Report
Introduction
Dates: 24DEC 2010-24 FEB 2011 | Quarter(s): 1 |
Project Description
Lengo la TEYODEN katika mradi huu ni kuongeza uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kupata haki zao za kushiriki katika shughuli za kijamii na za kimaendeleo katika ngazi ya kata na wilaya.Hatua hii itawafanya vijana kuwa na mchango katika maendeleo ngazi kata,wilaya na taifa kwa ujumla.
Region | District | Ward | Villages | Total Beneficiaries |
---|---|---|---|---|
Dar es Salaam | AZIMIO | AZIMIO | 42 | |
TEMEKE | SANDALI | SANDALI | 27 | |
MJIMWEMA | MJIMWEMA | 45 | ||
KIBADA | KIBADA | 22 | ||
YOMBO VITUKA | YOMBO VITUKA | 30 | ||
CHANG'OMBE | CHANG'OMBE | 10 | ||
CHARAMBE | CHARAMBE | 32 | ||
TANDIKA | TANDIKA | 32 | ||
MAKANGARAWE | MAKANGARAWE | 45 | ||
VIJIBWENI | VIJIBWENI | 13 | ||
KIMBIJI | KIMBIJI | 45 | ||
SOMANGILA | SOMANGILA | 23 |
Direct Beneficiaries | Indirect Beneficiaries | |
---|---|---|
Female | 22 | 164 |
Male | 19 | 205 |
Total | 41 | 369 |
Project Outputs and Activities
1.2 Kuendesha mafunzo ya siku 6 ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana kwa vijana 40 kutoka kata 12 za Manispaa ya Temeke.
1.3 Kufanya ufuatiliaji wa matokeo na ukusanyaji takwimu
2.) Warsha ya siku 6 ya sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na stadi za maisha kwa vijana 40 kutoka kata 12 za Manispaa ya Temeke ilifanyika kuanzia tarehe 8-13 jan 2011 katika ukumbi wa Amka Youth Centre Temeke Dar-es-salaam
3.) Ziara ya ufuatiliaji katika vituo 12 vya vijana katika kata 12 za mradi.wafuatiliaji waliangalia shughuli za mirejesho ya elimu ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana,walipata,mafanikio,changamoto na mapendekezo ya vijana kuhusu shughuli zijazo za mradi.
2.)Mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 -sh 6,602,000.00
3.)Shughuli ya ufuatiliaji wa matokeo ya mradi na kukusanywa takwimu -kiasi cha 738,000.00
Project Outcomes and Impact
patikana kama yalivyopangwa pamoja na kwamba ucheleweshwaji wa fedha umefanya mradi kutovuka malengo yake kwa kiasi kikubwa.
Lessons Learned
Explanation |
---|
Viongozi wa serikali wanatoa mchango mkubwa wa mawazo na nguvu zao kama wanashirikishwa vyema katika mradi kuanzia hatua za mwanzo za mradi. |
Kuna faida kubwa kufanya kazi kama timu katika utekelezaji wa miradi.Sio mtu mmoja katika asasi kuhodhi kazi zote za mradi. |
Vijana wakiwezeshwa na wakijiwezesha wanaweza kutoa machango mkubwa na kuchangia maendeleo ya Taifa. |
Vijana wana ari na moyo kutaka kuzitambua haki zao na kuzifuatilia ila huwa wanasubili kuanzishiwa mambo ili wao waendelee na tunaamini mwanzo umepatikana. |
Challenges
Challenge | How it was overcome |
---|---|
Kucheleweshwa kwa fedha kumeshusha mori wa walengwa kwa kiwango fulani. | Tumejitahidi kupandisha mori wa vijana na kupanga upya mikakati ykwa vijana ya kuhaikikisha wanashiriki vyema katika michakato ya maendeleo |
Ushiriki mdogo wa jinsia ya kike na mwamko wao katika kuchangia masuala ya kimaendeleon aya kijamii umekuwa mdogo ukilinganisha na wanaume tulitegemea 50%. | Tumepanga katika hatua nyingine kuhusisha zaidi jinsi ya kike. |
Kasi ya vijana kujiunga kama timu na kuanza kujenga hoja imekuwa ndogo ukilinganisha na mawazo ya awali wakati wa mafunzo. | Tuliwaunganisha vijana na kuwasisitiza kujenga hoja kama timu ili kubadilisha mifumo kandamizi na kuchochea maendeleo. |
Linkages
Stakeholder | How you worked with them |
---|---|
1.) TAMASHA | •Tulitumia mwezeshaji kutoka kwenye taasisi hii •Ushauri wa namna ya kutekeleza mradi kwa ufanisi •Kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa miradi |
2) WIZARA KAZI AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA | •Tumetumia mwezeshaji kutoka kwenye taasisi hii •Ushauri kuhusu ushiriki na ushrikishwaji wa vijana |
3. TBC 1 | •Tuliaandaa kipindi cha vijana kuzungumzia ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kimaendeleo. |
4.)Tanzania Daima | Kuandika taarifa ya shughuli za TEYODEN katika Gazeti |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE | •Ushauri wa namna ya utekelezaji wa mradi na ushiriki wa vijana |
Future Plans
Activities Planned | 1st Month | 2nd Month | 3rd Month |
---|---|---|---|
1.)Kutengeneza majukwaa 12 ya vijana katika kata 12 za mradi Temeke. | X | ||
2.)Kufanya midahalo 4 ya kujadili changamoto na kuweka mikakati ya kutatua. | X | ||
3.)Kufanya ufuatliaji wa matokeo na kukusanya takwimu za matokeo katika kata 12 za mradi Manispaa ya Temeke. | X |
Beneficiaries Reached
Direct Beneficiaries | Indirect Beneficiaries | ||
---|---|---|---|
Widows | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
People living with HIV/AIDS | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
Elderly | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
Orphans | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
Children | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
Disabled | Female | (No Response) | (No Response) |
Male | (No Response) | (No Response) | |
Total | (No Response) | (No Response) | |
Youth | Female | 22 | 205 |
Male | 19 | 164 | |
Total | 41 | 369 | |
Other | Female | 6 | (No Response) |
Male | 12 | (No Response) | |
Total | 18 | (No Response) |
Events Attended
Type of Event | When | Lessons | Actions Taken |
---|---|---|---|
Tamasha la Azaki za kiraia | 27-29 OCT 2009 | 1.)Uwajibikaji na uwazi katika uendeshaji asasi za kiraia | .)Kuongeza uwazi na uwajibikaji Kutekeleza mradi wa ari ya uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wa vijana. |
Mafunzo ya usimamizi wa fedha | 28SEPT2009 | 2.)Kuongeza uwezo wa mhasibu katika usimamizi na utunzaji wa fedha. | 2.)Kufanya usimamizi wa fedha na utunzaji wa kumbukumbu za fedha katika asasi ya TEYODEN. |
Mafunzo ya usimamizi wa ruzuku | 2 FEB 2010 | 3.)Kuongeza uwezo katika usimazi na fedha za ruzuku. | 3.)Kufanya utekelezaji wa mradi wa ari ya uwajibikaji,ushriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii na maendeleo. |
Mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini | MACHI 2010 | 4.)Mbinu na taratibu za kufanya tathmini na ufuatiliaji | 4.)Kuboresha shughuli za Taasisi na miradi ya TEYODEN katika ufuatiliaji na tathmini. |
Attachments
TEYODEN yakamilisha shughuli ya ufuatiliaji wa shughuli za vijana katika vituo 7 vya vijana kati ya vituo 12 vya mradi manispaa ya Temeke.
- UTANGULIZI
TEYODEN ipo katika kipindi cha utekelzaji wa mradi wa kuinua ari ya uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kimaendeleo na za kijamii.Mradi huu unafanyika katika kata 12 za Manispaa ya Temeke.Katika robo hii ya kwanza ya mradi shughuli 2 zimefanyika ambazo ni utambulisho wa mradi kwa wadau wa maendeleo 26 Manispaa ya Temeke na Mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwa vijana 40,24 kutoka vituo vya vijana, 12 vya kata na 12 kutoka asasi za vijana na 8 taasisi nyingine zilizopo Manispaa ya Temeke.Taarifa hii inatoa picha halisi ya mwendelezo wa mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana kwa vijana wengine katika kata kama matokeo ya mafunzo yaliyoendeshwa na makubaliano ya waandaaji wawezeshaji na vijana 40 walioshiriki mafunzo hayo.Hii ni taarifa ya shughuli ya ufuatiliaji katika kata 7 ambazo ni:- Sandali, Azimio, Vijibweni, Somangila, Kimbiji, Charambe na Yombo vituka.
- LENGO LA ZIARA YA UFUATILIAJI
-Lengo la shughuli hiini kupata takwimu na taarifa za vijana juu ya usambazaji wa sera ya vijna na stadi za maisha kwa vijana wengine katika kata.
Lakini pia kuweka mazingira mazuri ili vijana waweze kupokea jukwaa la vijana katika kata husika.
- KATA ZA MRADI ZILIZOTEMBELEWA
Tarehe |
kata |
Tarehe |
Kata |
29/1/2011 |
Somangila |
4/2/2011 |
Vituka |
29/1/2011 |
Vijibweni |
5/2/2011 |
Charambe |
30/2/2011 |
Kimbiji |
13/2/2011 |
Azimio |
31/1/2011 |
Sandali |
|
|
- KATA AMBAZO BADO HAZIJATEMEBELEWA
Tarehe |
kata |
Tarehe |
Kata |
|
Makangarawe |
|
Mjimwema |
|
Tandika |
|
Chang’ombe |
|
kibada |
|
|
- SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
- Vikao vya vijana vya kituo
- Vikao vya mrejesho vya vijana
- IDADI YA VIJANA WALIOFIKIWA
Kata |
Idadi ya vijana waliofikiwa |
Idadi ya wawezeshaji wanaoendelea |
|||
|
Me |
Ke |
Jumla |
|
|
Somangila |
9 |
14 |
23 |
3 |
- |
Azimio |
30 |
12 |
42 |
3 |
- |
Charambe |
20 |
12 |
32 |
3 |
- |
Sandali |
16 |
11 |
27 |
1 |
2 |
Kimbiji |
20 |
25 |
45 |
3 |
- |
Vijibweni |
7 |
3 |
10 |
2 |
1 |
Vituka |
16 |
14 |
30 |
3 |
- |
Jumla |
118 |
91 |
209 |
18 |
3 |
- MADA AMBAZO VIJANA WAMEZUNGUMZIA KATIKA MIJADALA NA VIKAO VYAO
- Sera ya vijana,stadi za maisha na umuhimu wa jukwaa la vijana.
- ZANA ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA VIJANA
- Chaki,bao na vitini
- MBINU ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA VIJANA ZA KATA
- Majadiliano shirikishi
- Maswali na majibu na visa mkasa
- JINSI MBINU ZILIZOTUMIKA ZILIVYOFAA
- Mbinu shirikishi husaidia vijana kila mmoja kushiriki katika kupanga jambo.
- Mbinu zilizotumika zinaibua hisia za vijana hasa kuzungumzia matatizo yao.
- MAMBO YALIYOIBULIWA KATIKA MIJADALA YA VIJANA
- Vijana hawajui namna ya kujiunganisha ili kujenga timu jambo ambalo ni muhimu sana katika kufanya jambo Fulani libadilike.
- Vijana hawana mbinu za namna ya kujenga hoja zenye ushirikiano wa pamoja ili waweze kusikilizwa.Imeonekana kuwa lazima vijana wawezeshwe kuona umuhimu wa dahana ya kuwa na hoja zenye ushahidi na tija mbazo wakizisimamia watoa maamuzi wataziweka katika mipango ya utekelezaji.
- Umuhimu wa vijana kushiriki katika michezo na burudani limeonekana kuwa ni jambo ambalo litafanya vijana kuwa pamoja na kushirikiana.
- Vijana kuwa na miradi ya pamoja ya uchumi na kuwezeshwa kupata mikopo itakuwa ni njia ya kuwafanya waweze kuitegemea ki uchumi.
- Upatikanaji wa sera ya maendeleo ya vijana ni jambo ambalo vijana wamelisisitiza kwa kuelewa sera itawafanya wawe kwenye nafasi nzuri ya kutetea haki zao.
- MAONO YA VIJANA KUHUSU MRADI WA KUINUA ARI UWJIBIKAJI NA USHIRIKI
- Vijana wanaunga mkono mpango kwa kuwa utawezesha vijana kujitambua,kuwa wathubutu na wenye kuleta tija.
- Vijana wanaona mpango huu utawezesha vijana kushriki kwenye ngazi mablimbali za maamuzi kutoka mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi ngazi ya taifa.
3. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA
- Viwango tofauti vya uelewa wa vijana katika masuala ya kijamii na kikaendeleo vinapunguza kasi ya mpango wa uwajibikaji na ushiriki kufanya kazi ipasavyo.
- Vijana wa mitaa michache wameshirikishwa katika hatua za awali za mpango
- Dhana ya kutojiamini miongoni mwa vijana.imejionyesha katika baadhi ya kata pamoja na kuwezeshwa kwa muda wa siku 6 bado baadhi ya vijana wameshindwa kufanya uwasilishaji wa mada ipasavyo kwa vijana wenzao
- Ukosefu wa vindea kazi umefanya uwaslishaji wa elimu kwa vijana kuwa mgumu kiasi.
- Kasi ya vijana kujiunga kama timu na kuanza kujenga hoja imekuwa ndogo ukilinganisha na mawazo ya awali wakati wa mafunzo.
- Ushiriki mdogo wa vijana katika baadhi ya kata mfano kata ya Vijibweni vijana 10 tu walishriki badala ya wastani wa vijna 30 kwa kila kata.
- Ushiriki mdogo wa jinsia ya kike na mwamko wao katika kuchangia masuala ya kimaendeleon aya kijamii umekuwa mdogo.
- MAPENDEKEZO YA NAMNA YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
- Kutoa taarifa kwa uongozi wa kata kabla ya kuanza shughuli za vijana katika kata.Hii itasaidia kupata ushiriki wa vijana kutoka mitaa yote ya kata husika.
- Kushirikisha vijana katika mitaa yote ya kata husika katika shughuli zao ili kuleta maamuzi ya pamoja.
- Wahusishe hata kempu za vijana na maendeo mengine ili kupata idadi kubwa ya vijana katika kata.
- Ofisi ya mtandao iwe na programu maalumu ya kutembelea kataza mradi ili kuwaongezea kujiamini vijana.
- Ofisi ya mtandao kua na mawasiliano ya moja kwamoja na mtendaji wakata ili kujua kama yapo mahusinao ya karibu n kubadilishana mawazo na vijana.
- Katika kipindi kijacho cha mradi wasichana watiliwe mkazo zaidi ili kuleta usawa wa kijinsia.
- JINSI MAFUNZO YALIVYOSAIDIA VIJANA
Pamoja na madhaifu madogo madogo yaliyojitokeza kwa baadhi ya kata za mradi
Yapo mafanikio makubwa yaliyotokana na mafunzo na shughuli za mradi.
- Mafunzo yamefanya vijana waliyoyapata kuamsha ari kwao katika kujitambua na kufahamu haki zao pamoja na kujenga hoja.
- Mawasiliano mazuri kati ya viongozi kata na vijana mfano katika kata ya azimio mtendaji wa kata hiyo anafanya vikao na vijana kama hatua ya kutambua na kufanikisha shughuli za vijanan hao.
- Zipo kata ambazo kumekuwa na mwamko wa vijana yaliyovuka kiwango cha makadilio ya vijana yaliyowekwa mafano kata ya kimbiji na azimio.
- HADITHI MAFUNZO
Mpaka katika hatua hii ya mwanzo ya ufuatiliaji bado kulikuwa hakuna kisa mafunzo ha kusisimua kilichoweza kulekodiwa kutoka katika kata za lengwa za mradi lakini tunategemea kupata mengo kutoka katika kata hizo.
- HITIMISHO
Zoezi la ufuatiliaji katika kata 7 za awali ni hatua moja kuelekea katika kumalizia kata nyingine 5 za mradi tunatemea zoezi hili litakamilika mpaka kufikia katikati ya mwezi februari hatua itayotoa picha halisi ya matokeo ya awali katika kipindi hiki cha robo ya kwanza ya mradi.Picha hii imetupa mafunzo makubwa katika kubadili mbinu na taratibu za mradi katika kipindi kijacho cha mradi na ni matumaini yetu makubwa kuwa mrdi utafanya vizuri katika kuzifanya ndoto za vijana kuwa kweli.Ni matumaini yetu kuwa kila ngazi itawajibika vya kutosha katika kuhakikisha ndoto ya mradi huu inakuwa kweli.
TEYODEN yafanya ufuatiliaji katika vituo vya vijana vya kata,zoezi linalokamilisha robo ya kwanza ya mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika shughuli
kijamii na maendeleo manispaa ya Temeke.
TEYODEN wafanya mkutano na wadau wa maendeleo ya vijana manispaa ya Temeke
Katika kujiandaa na utekelezaji wa mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji katika shughuli za kijamii na kimaendeleo ,leo TEYODEN imeanza utekelezaji huo kwa kufanya kikao na wadau wa maendeleo ya vijana katika manispaa ya Temeke,ambapo jumla ya washiriki 26 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho wote walihudhuria.Kulikuwa na maafisa wanne kutoka manispaa ya Temeke,maafisa watendaji 12 kutoka kata 12 za mradi huu na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata walioalikwa miongoni mwa kata hizo za mradi,walikuwa 4.
Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miezi 12 na jumla ya shughuli 10 zitatekelezwa,ambazo ni pamoja na kikao hiki ambacho tayari kimefanyika leo,mafunzo kwa vijana 40 kutoka katika kata 12 juu ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007,ufuatiliaji na ukusanyaji takwimu za matokeo ya mradi,kutengeneza majukwaa 12 ya vijana,kuendesha midahalo 4 ya vijana ambayo itaibua changamoto zinazowakabili,kufanya ufatiliaji wa shughuli hizona ukusanyaji wa matokeo ya mradi,uanzishwaji wa kizio cha kumbukumbu(database),utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi elimishi,uendeshaji wa matamasha 4 ya wazi(road show) juu ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo na ufanyaji wa tathmini ambayo itafanywa na mtathmini wa nje (external evaluator).
Mradi huu utatekelezwa katika vipindi vinne yaani miezi mitatu mitatu.Mradi huu umefadhiliwa na The Foundation for Civil Society(FCS) na utagharimu shilingi milioni 35 katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.
TEYODEN yaendesha mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007
Katika kutekeleza mradi wa ukuongeza ari kwa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii,TEYODEN inaendesha mafunzo ya siku sita kwa vijana wawakilishi kutoka kata 12 za mradi huu ambao umefadhiliwa na The Foundation for Civil Society wenye thamani ya shilingi miliono 35 na mradi huo utakuwa na shughuli takribani kumi za kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja.
TEYODEN wafanya mkutano na wadau wa maendeleo ya vijana manispaa ya Temeke
Katika kujiandaa na utekelezaji wa mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji katika shughuli za kijamii na kimaendeleo ,leo TEYODEN imeanza utekelezaji huo kwa kufanya kikao na wadau wa maendeleo ya vijana katika manispaa ya Temeke,ambapo jumla ya washiriki 26 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho wote walihudhuria.Kulikuwa na maafisa wanne kutoka manispaa ya Temeke,maafisa watendaji 12 kutoka kata 12 za mradi huu na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata walioalikwa miongoni mwa kata hizo za mradi,walikuwa 4.
Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miezi 12 na jumla ya shughuli 10 zitatekelezwa,ambazo ni pamoja na kikao hiki ambacho tayari kimefanyika leo,mafunzo kwa vijana 40 kutoka katika kata 12 juu ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007,ufuatiliaji na ukusanyaji takwimu za matokeo ya mradi,kutengeneza majukwaa 12 ya vijana,kuendesha midahalo 4 ya vijana ambayo itaibua changamoto zinazowakabili,kufanya ufatiliaji wa shughuli hizona ukusanyaji wa matokeo ya mradi,uanzishwaji wa kizio cha kumbukumbu(database),utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi elimishi,uendeshaji wa matamasha 4 ya wazi(road show) juu ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo na ufanyaji wa tathmini ambayo itafanywa na mtathmini wa nje (external evaluator).
TEYODEN yashiriki kwenye mkutano wa wadau Morogoro
Hivi karibuni ulifanyika mkutano wa awadu nwa maendeleo ya vijana pale mjini Morogor wakiupitia mkataba wa vijana wa Afrika na mkakati wa ushiriki na ushikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii.
Katika mkutano huo jumla ya washiriki 30 kutoka asasi za vijana na wawakilishi kutoka wizara za maendeleo ya jamii,jinsia na watto,wizara ya kilimo na wizara ya elimu na mafunzo walihudhuria mkutano huo.
Wadau waliupitia mkataba huo na kutoa mapendekezo ya kuuboresha ili uweze kuendana na mahitaji ya vijana wa kitanzania na mkakati huo pia.