SHIRIKA LA MAENDELEO NA SERA TANDAHIMBA (SHIMASETA) ni Asasi ya kiraia iliyoasisiwa mwaka 2008, na kuanza shughuli zake mnamo mwaka 2009. Ofisi za makao makuu, zipo katika kijiji cha Chaume, Kata ya Chaume, wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara - Tanzania. Shimaseta ni shirika lisilo la kiserikali ambalo halilengi kupata faida "Azak" lililosajiliwa chini ya Sheria Na. 24 ya usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali, katika Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto. Kazi ambazo SHIMASETA hufanya, ni pamoja na kuijengea jamii uelewa kuhusu mambo ya Mazingira, Afya, ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma na wajasiliamali, kwa njia ya kufanya mafunzo/warsha, makongomano na midahalo kwa kushirikiana na wananchi, viongozi, Asasi za kiraia, vyombo vya habari, wafadhili wa nje na ndani na wadau mbalimbali. SHIMASETA Hufanya shughuli zake kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, Sheria, Katiba, kanuni na miongozo ya shirika kwa ujumla wake. Shirika linao watumishi wanne (4) wa kujitolea.