HISIA CULTURAL TROUPE-HCT IMEFUNGUA OFISI MPYA YA KUDUMU BAADA YA KUWA KATIKA HEKA HEKA ZA KUHAMA MARA KWA MARA
TUPO MAKUTANO YA MTAA WA JANGWANI NA MTWA, IRINGA MJINI
KARIBUNI SANA
KONGAMANO LA SANAA
WASANII wote mnaalikwa katika kongamano la sanaa za maonesho linalotarajiwa kufanyika Juni 15, 2013 hapa mkoani Iringa kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.
Kongamano litakuwa la siku moja na washiriki wanaomba kujigharamia kwa 100%. Pamoja na mada, kongamano litapambwa na burudani za sanaa za maonesho.
Watakaopenda kujitolea kuendesha mada na wale watakaopenda kuonesha sanaa zao katika kongamano hilo wajiandikishe mapema kabla ya Februari 2012.
Uratibu wa kongamano utagharamia chai na chakula cha mchana kwa washiriki wote katika siku ya kongamano.
Wasanii wote mnakaribishwa!
Limeandaliwa na:-
Hisia Cultural Troupe
S.L.P 436 Iringa
0754439740
Hisia tumehudhuria workshop ya wadau wa VVU/UKIMWI iliyofanyika manispaa ya Iringa. Pamoja na mambo mengine tumeweza kubadilishana uzoefu na asasi nyingine. Ni fursa nzuri za kujifunza ambazo tunazihitaji sana!
TUNAOMBA KUPATA MTAALAMU WA KUJITOLEA AWEZE KUTUANDIKIA ANDIKO LA MRADI KUHUSU UHAMASISHAJI WA TOHARA KWA WANAUME. ANDIKO HILO LINATAKIWA KUWASILISHWA KWA MFADHILI KABLA YA TAREHE 31 AUGUST 2012. TAFADHALI SANA ALIYE TAYARI KUTUSAIDIA KWA HILI AWASILIANE NASI KUPITIA KWA:
Mkurugenzi Mtendaji
Hisia Cultural Troupe
Emai: hisiaone @yahoo.com
Cell: 0715 439740