How has the quality of the water where you live been affected by the flooding?
siku zote natumia maji ya bomba kutoka keko juu ila kwa watumiaji wa maji ya visima vyanzo vyao vimeathiriwa na vyoo vilivyo bomoka
maji kwa sasa si salama vyoo na visima vilibomoka kwa pamoja na kuchanganyikana ,hivyo kusababisha watumiaji kukosa maji salama
Maji kwa ujumla si salama wakati wa mafuriko watu walitumia nafasi hii kutapisha vyoo vyao ambapo uchafu huo ulikutana na visima vilivyo bomoka na kuchanganyikana
eneo hili linategemea visima kwa maji ya matumizi ya kawaida na kwa kunywa tunachota kwenye mabomba ambayo yapo keko juu ,hivyo maji ya visima kwa sasa si salama kwani maji taka kutoka maeneo yote yalifunguliwa na kuchanganyika na maji ya visima.
Mtaa mzima visima vilichanganyika na maji taka, ukizingatia maji ya visima ndiyo yanayotumiwa na wengi kwani si kila mwananchi ana ewezo wa kununua maji ya bomba
mabomba yote yaliyokuwa eneo hili yalisombwa na maji ,visima vingi vilibomoka na kuruhusu maji taka kuingia,wanaokaa maeneo ya juu walifungulia na kutapisha vyoo vyao hivyo kuingiliana na visima vyetu
No pure water which is sufficient to human consumption.
siku zote natumia maji ya bomba kutoka keko juu lakini kwa wenye visima havifai tena kwani si rahisi kutofautisha maji safi na taka
Maji ni ya visima tu ndiyo yanayotumika baada ya mabomba yote kusombwa na mafuriko, maji hayana usalama kabisa, na kuhofia kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Baada ya kisima kubomoka maji yalijaa sana kitu kinachoashiria maji hayo kuchanganyika na mji taka
Mabomba yote ya maji masafi yamesombwa na mafuriko, maji tunayotumia sasaivi ni ya visima, na hayana usalama kwa matumizi ya binadamu.
maji kwa ujumla ni machafu kutokana na kuchanganyikana na maji taka ,hivyo maji ya matumizi ya kawaida si salama ,tunalazimika kununua maji ya bomba kutoka Keko juu ambayo kwa hali yangu sitaweza kumudiu itabidi nitumie maji hayo ya taka sina jinsi
Maji yanayotumika ni machafu kwani mabomba yamapasuliwa na mafuriko.
Maji safi na salama hauna
Maji safi na salama hakuna
Hakuna maji safi na salama
Maji sio salama
Maji sio salama kwa sababu ya mitaro michafu
Maji hakuna
Maji sio salama
« Back to report