Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sasa?

vyandarua, mitaro isafishwe kwa dawa ili kuua wadudu , tuboreshewe mazingira kwa kujengewa mitaro ,makaravat yajengwe kwenye mfereji mkubwa, nyumba zetu zilizobomoka zikarabatiwe,
tutafutiwe maeneo maalum ya kuhifadhi taka ili zisitupwe ovyo kwenye njia za maji,mitaro midogo midogo ijengwe kati ya nyumba na nyumba ili maji yasituame,tuwekewe vifusi kwenye maeneo haya yaliyomomonyolewa na maji
vyandarua, dawa ya kuua wadudu kwa sababu maji bado yametuama,tujengewe na kuzibuliwa mitaro ili maji yasituame ,nyumba zilizojengwa holela zibomolewe ili ziruhusu maji yapite kwa urahisi.
unahitaji maji safi, tupate mabomba yatakayotoa maji safi tofauti na yale ya ya visima tunayotumia, tupatiwe dawa ya kusafishia mazingira yetu, mitaro midogo ijengwe ,mfereji mkubwa upanuliwe kutoka ulipoanzia mpaka unapoishia
kufanyiwe fumigation kwani maji bado yametuama hivyo kuua wadudu , kujengwe mitaro midogo itakayo ruhusu maji kupita kutoka eneo maja hadi jingine ,mfereji mkubwa upanuliwe na kuhakikisha ni safi kila wakati .
Vifusi vya kuinua maeneo yetu,Mfereji mkubwa wa kutoka darajani mpaka keko chini utengenezwe kwa kuwekewa makaravati , kuta au nyumba zilizojengwa kando kando ya mfereji mkubwa zibomolewe na watu wapewe maeneo.
New infrastructure, Social Services, New permanent settlement, School equipment and clothes.
kusafisha na kutengeneza mitaro midogo midogo itakayo tiririsha maji kwenye mfreji mkubwa ,kuta zilizojengwa holela na kuziba maji zibomolewe ,mfereji mkubwa ukarabatiwe ili usaidie maji kupita kwa urahisi, tupatiwe vifusi vya kuinua maeneo yetu
Kusafishwe mitaro kwani mpaka sasa maji bado yametuama,kuletwe dawa ya kuua wadudu ya kupulizwa{,fumigation} takataka zilizokwama kwenye mitaro mpaka sasa zitolewe ,vyadarua kwa ajiil ya malaria kutokana na mbu kuwa wengi sana.
Miundombinu ya maji, barabara, madaraja na mawasiliano kwa ujumla.
kujengwe mitaro na mifereji midogo midogo itakayoruhusu maji kupita kwa urahisi kati ya nyumba na nyumba .
Mfereji mkubwa wa kutoka darajani mpaka barabara ya kilwa shell ya Ruby utengenezwe ili kuruhusu maji kupita kipindi cha mvua
Kujenga upya miundombinu muhimu, ili kurejesha mawasiliano.
« Swali lililotanguliaSwali lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti