MIPANGO KAZI YA UMOJA WA WAZEE NA MAENDELEO TANZANIA
MIPANGO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU KUANZIA JANUARY 2013
- MIPANGO KAZI YA MUDA MFUPI ENDELEVU
AA- Umoja wa wazee na maendeleeo Tanzania inawatafuta na kuwaomba wa binafsi;makampuni binafsi ;mashirika ya umma;mashirika ya kidini;n.k.nchini na nje ya nchi watakaoguswa na umoja huu watusaidie wazee ili wasiwe tegemezi. Tunawaomba misaada ya hali na mali ili wazee tujitegemee.
BB-Tokea 28/04/2014 kwa michango ya wanachama wenyewe,biashara ndogo ya kuuza maji ya kunywa ya chupa na soda.(mradi wenyewe ni mdogo sana) tunaomba mtusaidie.
CC-Tunaendelea kuwaomba wafadhili mbalimbali nchini na nje ya Tanzania NGO’s n.k mtusaidie fedha au bidhaa soda na maji ya chupa ya kunywa na vinavyofanana na hivyo.
DD-Yeyote atakaetusaidia hatajutia fedha au mali yake,kwani uongozi umekamilika.
i. Mwenyekiti
ii. Makamu mwenyekiti
iii. Katibu
iv. Naibu katibu
v. Muweka hazina
vi. Kamati ya utendaji
vii. Kamati ya uchumi
- Kamati ya utawala,maadili ya Uongozi na usalama upo.
EE-Kauli mbiu ya wazee (Mission)
“wazee ndugumbi tumeanza tuungeni mkono tusonge mbele”