Injira
UMOJA WA WAZEE NA MAENDELEO TANZANIA

UMOJA WA WAZEE NA MAENDELEO TANZANIA

Kinondoni, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MIPANGO KAZI YA WAZEE YA MUDA MREFU

Tukifanikiwa kupata wafadhili,wahisani wa kutupatia fedha au vifaa n.k.mipango yetu ni kama ifuatavyo:

AA-Tunakusudia kutafuta ardhi ili tulime mashamba nje ya Dare es salaam ili tuanzishe shughuli za kilimo.

BB-Kuanzisha vitalo vya kupanda mti sehemu mbalimbali nchini.

CC-Kuchimba visima vya maji safi na salama katika sehemu zenye shida kubwa ya maji na kuyauza kwa bei poa nafuu.(hususani vijijini).

DD-Kusaidia watoto yatima na walemavu popote walipo nchini pia na maskini.

EE-Tutashirikiana kwa hali na mali marafiki,majirani na jamii kwa ujumla nchini na nje ya nchi.

Kwa sasa tuna marafiki shiriki hawa:

1)      MOHISPAC FOUNDATION

P.O BOX 77624

DAR ES SALAAM

e-mail. Pvn.ziacharo@yahoo.com

mobile 0716-876742

mkurugenzi mchungaji ziacharo makenya.

2)      Mr. Remmy Raphael

e-mail. remmyraphael@yahoo.com

Ngerengere Bwawani

Pwani.

FF-Uchumi wa wazee ukikomaa kiuchumi na kimapato tutanunua mabasi hususani katika jiji la Dar es salaam Tanzania,kwa kuwabeba wanafunzi,watoto wa kawaida,walemavu na kinamama kwa bei nafuu tutakayo pangiwa na serikali.

GG-Umoja huu wa wazeeTanzania utaendelea kutoa Elimu ili wazee wajue haki zao Tanzania.

HH-Pia kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwatumia madaktari na wataalam katika magonjwa hatari kama Ukimwi.n.k

II-Tunawaomba watu binafsi,mashirika ya umma,Taasisi za umma,NGO’s(makampuni binafsi) na wengine wote mtakaoguswa na matatizo ya wazee tunaomba watusaidie popote walipo nchini Tanzania au nje ya Tanzania, na wazee tupo tayari kushirikiana na yeyote.

JJ-Umoja wa wazee na maendeleo Tanzania upo imara kwani ina katiba/kanuni yake ambayo ndio muongozo wa umoja huu na board yake.

KAULI MBIU YETU

wazee ndugumbi tumeanza tuungeni mkono tusonge mbele”

Mwenyekiti

IDDI   A. MSUMAGILLO

UMOJA WA WAZEE NA MAENDELEO TANZANIA

 

 

4 Mata, 2015
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.