Wazee wana uhitaji mkubwa wakusaidika hivyo tunatoa rai kwa watu mbalimbali wenye mapenzi mema na wazee wajitolee kushirikiana nasi katika kukamilisha malengo yetu katika changamoto zinazotukabili katika masuala ya afya, elimu, wataalamu wakuandika miradi na taaluma yoyote ambayo unadhani kuja kwako kwetu inaweza kutusaidia kuvuka mbele zaidi ya hapa tulipo.Tunawakaribisha makabila yote, dini zote kufanya kazi nasi kutoka ndani na nje ya nchi. Kwa pamoja tutaleta mabadiliko katika jamii ya Tanzania na ulimwengu kwa ujumla.