Fungua

/TEYODEN/news: Kiswahili: WI0009BA39E1BA0000088794:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiswahili) Kiswahili

Vijana washiriki maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika tarehe 2 disemba 2011 viwanja vya Zakhiem Mbagala Charambe

Takribani vijana 60 wanachama  na Viongozi wa mtandao wa vijana Manispaa ya Temeke wameshiriki maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo mwaka huu yamefanyika katika viwanja vya Zakhiem kata ya Mbagala.Maadhimisho hayo yaliyopambwa kwa vikundi mbalimbali vya sanaa za ngoma na maigizo yanayolenga kuhimiza jamii dhidi ya hatua za kudhibiti maambukizi,kutoa hudua kwa waathiriwa na waathirika wa ukimwi,upimaji kwa hiari,matumizi ya kondom na hatua za uboreshaji wa sera zinazohusu ukimwi yalianza kwa maandamano mafupi yaliyopokelewa na mgeni rasmi Naibu meya wa Manispaa ya Temeke.

Kazi za TEYODEN

TEYODEN katika banda lake ilifanya kazi zifuatazo:-

  • Kuelimisha jamii hasa vijana juu ya umuhimu wa stadi za maisha kama nyenzo ya kubadili tabia hatarishi kwa vijana.
  • Kutoa huduma ya kondom bure
  • Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli za upunguzaji wa maambukizi na utoaji huduma kwa wagonjwa.
  • Kuhamasisha jamii juu upingaji wa unyanyasaji wa wanawake hasa vijana na kujenga uwezo wa kina mama wadogo kukabiliana na changamoto zitakazo wapelekea katika maambukizi ya ukimwi.

Mafanikio

  • Wanajamii 78 wakiwemo vijana 56 walitembelea banda na kujifunza masuala muhimu ya upunguzaji wa maambukizi na utoaji huduma kwa waathirika na waathiriwa wa ukimwi
  • Idadi ya kondom 371 zilisambazwa kwa vijana na wanajamii walioudhulia maadhimisho
  • vijarida 217 vilisambazwa kwa vijana na wanajamii waliohudhuria maadhimisho

Mwisho wa maadhimisho haya ni mwanzo wa michakato na mipango mipya juu ya uthibiti wa maambukizi mapya na huduma kwa waathiriwa na waathirika wa Ukimwi.Kila mtu achukue nafasi yake sasa hivi na hapo hapo alipo.Tusiufundishe ulimwengu kuimba tuonyeshe kwa vitendo.

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe