Log in
Society for Women and AIDS in Africa

Society for Women and AIDS in Africa

Misufini mtaa wa police, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

large.jpg

Mwenyekiti wa SWAA akitoa mafunzo ya mada kuhusu elimu ya ukimwi na afya kwa mtoto wa kike katika shule ya sekondari Mnziha 2011.

large.jpg

Cheti usajili shilika la SWAA

large.jpg

watoto waliopata mavazi katika shule ya msingi kisaki kituoni wilaya ya morogoro vijijini kwa ufadhili wa TAKIAIDS 2008.

large.jpg

mwenyekitri wa shirika la SWAA ( Mrs. Hellen Mbezi) akijadiliana na viongozi wa kabila la masai kijiji cha Dakawa kuhusu elimu ya malezi na makuzi kwa watoto wa kike wakati wa kuhamasisha uwekaji wa maji salama kijijini kwao kwa ufadhili harimashauli ya wilaya ya Mvomero - Tanzania 2009.

large.jpg

Hawa ni vijana wa tarafa Ngerengere waliopata elimu ya ukimwi na matumizi bora ya utumiaji wa kondomu kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society 2005.

large.jpg

Walezi wa watoto yatima na wale wahishiyo kwenye mazingira magumu (kijiji cha Matombo) waliopata mafunzo ya elimu ya saikolijia kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society 2008

large.jpg

kipeperushi cha shirika la SWAA kinachoonyesha nembo ya SWAA na kuonyesha picha za mafunzo ya elimu ya saikolojia kwa walezi wa watoto yatima na wale waishiyo katika mazingira magumu.

 

KATIBA YA SWAA-MOROGORO TANZANIA

 

1.0  SEHEMU YA KWANZA

 

1.1  JINA    SOCIETY FOR WOMWEN AND AIDS IN AFRICA – (SWAA)

1.2  ADDRESS   P.O. BOX 762    MOROGORO

1.3  OFISI KUU:   MOROGORO MANISPAA

1.4  MMILIKI   WANACHAMA WA SWAA

 

1.1  Wanachama wa kuchaguliwa waliotokana na shirika anzilishi liliitwalo Society for women and AIDS in Africa (SWAA-T)

 

2.0  SEHEMU YA PILI

 

2.1  Ufafanuzi

-        Shirika hili litajishughulisha na masuala yote ya kijinsia.

-        Shirika limesajiliwa kwa mara ya pili  hapa TANZANIA wa shughuli zake na kubadili katiba ya awali iliyokuwa inashughulikia UKIMWI tu na sasa  baada ya kupanua wigo shughuli zake kwa mujibu wa sheria ya usajili litafanya kazi nchi nzima kama ruzuku itakayo ombwa na kupatikana bila kipingamizi chochote. Shirika litapenda kufanya kazi na mashirika mengine ndani ya nchi na nje ya nchi na kupokea wageni nje ya nchi wanaopenda kufanya kazi na shirika letu kwa Nyanja yoyote wanayotaka.

Maombi yoyote yatakayotumwa nje na ndani ya nchi yatakuwa na jina la jina la chama na mawasiloiano yatakuwa yanafanyika na watu wawili ambao ni Priscar D. Mbezi afisa uhusiano simu no 0713 249298 email yake ni  prissdavid@yahoo.com.

 

 

2.2  LENGO

-        Kutoa mafunzo mbalimbali kwa njia ya nadharia na sanaa za jukwaani (shirikishi) katika nyanja zote kulingana na mahitaji yaliyopo.

 

2.3  DIRA

-        Ifikapo mwaka 2025 viongozi wa shirika  na  jamii iishiyo Morogoro itaweza/ wataweza kusimamia rasilimali zinawazunguka na kuzilinda. Pia kuzijua sheria za nchi  ikiwepo katiba ya nchi ya Tanzania na kuzisimamia.

 

2.4  MADHUMUNI

-        Kuunganisha jamii katika jukumu la kulinda rasilimali walizonazo na kuweza kuzitumia vema ili kuondoa umaskini. Pia kuelimisha kuhusu  maswala ya utawala bora na sheria za nchi.

-        Kuiwezesha jamii yote  iishiyo Morogoro kwa sasa katika kutambua sheria zinazosimamia mirathi hasa kwa wanawake  na kufanya tafiti mbalimbali kulingana na shughuli itakayokuwa inahitajikamkwa vipindi vya mpito  mfano  sheria za chaguzi mbalimbali,  Sensa ya watu, na elimu kwa umma.

-        Kutoa elimu ya ujasiria mali na huduma ya ardhi inayowazunguka hasa kupinga mikataba isiyo rasmi, kuhusiana na mali asili zinazoizunguka jamii ikiwepo misitu.

-        Kulinda wanyama wanaishi katika misitu ya asili na kupiga vita uchomaji moto misitu yetu.

 

-        Kuunda vikundi kazi vya vijana walio nje ya shule na ndani ya shule vitakavyo pokea mafunzo na kuyafanyia kazi.

-        Kujengea uwezo jamii iishiyo vijijini katika kuongeza kipato kutokana na misitu kama vile kufuga nyuki, na kurina asali.

-        Kutembelea familia zenye mazingira magumu na kushauri upatikanaji wa sare za shule za  za msingi na sekondari, za kata ambazo zinaishi watu wenye maisha magumu.

 

2.5  SHUGHULI

a)      Kuhamasisha Jamii kufanya shughuli za ujasiriamali katika maeneo maalumu hasa katika kingo za misitu, mito ili  kuongeza kipato chao mfano ufugaji, wa nyuki na kilimo cha miwa, migomba,  alizeti n.k.

b)     Kuhamasisha jamii na taasisi za uma kuhusu dhana ya utawala Bora, katiba nk.

c)     Kufanya uhamasishaji  kuacha ulimaji wa  kilimo kisicho rasmi kinachoweza kuharibu misitu yetu na vyanzo vya mito.

d)     Kusimamia vikundi vilivyoundwa katika jamii shughuli mbalimbali vya kazi ili kuondoa umaskini.

e)     Kubuni miradi mbalimbali itakayoshirikisha makundi mengine wakiwepo vijana, wanaume ili kuboresha maisha yao.

f)      Kupiga vita taratibu zote zinazokwenda kinyume na hali za binadamu

g)     Kushawishi vyombo vya vya habari na  serikali kufanya kazi na shirika hili ili kuifikia jamii mapema katika shughuli zote zitakazohusu jamii moja kwa moja.

h)     Kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kuzalisha mazao bora ili kuinua kipato chao.

 

3.0SEHEMU YA TATU 

3.1  MASHARTI / SIFA ZA WANACHAMA

-        Mwanaume na mwanamke yeyote aliye na umri kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea

-        Wataalamu wa mambo ya jenda na misitu.

-        Mwanachama  mwenye nia ya   kujitolea na wenye  utaalamu, ili utalaamu  wake ufaidishe   wengine  tukiwakaribisha watu wenye nia ya kujitolea nje na ndani ya nchi yetu.

 

3.2  SEHEMU YA TATU

Kutakuwa na aina mbili za uanachama

a)     Wnachama wa kudumu

b)     Wanachama wa heshima

 

-        Wanachama wa kudumu ni wale ambao kwa hiyari yao wameomba uanachama na kukubaliwa kwa mujibu wa katiba.

-        Wanachama wa (Heshima) ni wale kwa utaalamu wao na wadhifa wao wamekubali kujitoa kwa hali na mali kujiunga kuendeleza shirika kwa hali na mali pia kitaaluma

 

3.3  UTARATIBU WA KUJIUNGA

            i.          Kutakuwa na fomu  maalumu  za maombi ya uanachama ambazo  zitalipiwa shilingi 20,000/=  ambazo hazitarudishwa,  kama mwombaji  amekubaliwa au amekataliwa.

          ii.          Fomu itajazwa na mwenyewe kuomba uanachama kisha itapelekwa kwenye kamati ya utekelezaji.

        iii.          Itajadiliwa katika kamati ya utekelezaji na kutoa mapendekezo yake hatimaye kupelekwa kwenye mkutano mkuu kwa kuthibitisha.

        iv.          Akikubaliwa atapaswa kulipa kiingilio cha shilingi 30,000/= na ada ya kila mwaka Tshs 20,000/=  jumla shilingi 50,000/=

 

3.4  HAKI NA WAJIBU

a)     HAKI

-        Mwanachama anayo haki kujiunga na vikundi vingine

-        Anayo haki kuchagua kuchaguliwa

-        Kudhamini kitu kadri anavyojiamini

-        Akiacha uanachama kwa sababu za msingi uongozi utakutana kujadili kuwa ni haki gani anayostahili kupewa.

-        Akipata tatizo yeye mwenyewe shirika linaweza kumsaidia endapo hali itaruhusu.

-        Anayo haki kusiriki au kushirikishwa katika shughuli zote.

 

3.5  KUACHA UANACHAMA

                     i.  Mwanachama ataacha uanachama kwa:-

                   ii.  Kujitoa yeye mwenyewe

                 iii.  Kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu

                 iv.  Kifo au kuvunjika kwa kikundi

                   v.  Kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa ya maandishi.

                 vi.  Kutotimiza taratibu zilizowekwa kikatiba

 

4.0  SEHEMU YA NNE

4.1  UONGOZI

Viongozi wafuatao ambao watachaguliwa na mkutano mkuu:

            i.          Mwenyekiti na msaidizi wake.

          ii.          Katibu na msaidizi wake.

        iii.          Mratibu wa mipango

        iv.          Mratibu wa fedha

          v.          Mratibu wa Elimu

 

4.2  SIFA ZA UONGOZI

i.                 Mwenye uwezo wa kuongoza

ii.               Mwenye uwezo wa kusuluhisha migogoro ndani na nje ya shirika

iii.             Mwenye uwezo wa kugundu matatizo kuyatafutia ufumbuzi wa haraka

iv.             Mwenye kupanga mipango na kutekeleza

v.               Mvumilivu, mpole mnyenyekevu na asiye kata tamaa

vi.             Mwenye uwezo wa kujieleza, kushawishi, mkweli,  na anayekubalikubadilika.

 

4.3  WAJIBU WA VIONGOZI

i.                 Mwenye uwezo wa kuongoza

ii.               Mwenye wa kusuluhisha migogoro ndani ya nje ya shirika

iii.             Mwenye uwezo wa kugundua matatizo kuyatafutia ufumbuzi wa haraka

iv.             Mwenye kupanga mipango na kuteleza

v.               Mvumilivu, mpole, mnyenyekevu na asiye kata tama

vi.             Mwenye uwezo wa kujieleza kushawishi na anayekubalika.

 

4.4  WAJIBU WA VIONGOZI

  1. Mwenyekiti

Atachaguliwa na mkutano mkuu wa atakuwa na majukumu yafuatayo:-

a)     Atakuwa Mwenyekiti wa mikutano kamati ya utekelezaji

b)     Atakuwa msemaji mkuu wa shirika

c)     Atalinda sera kanuni na katiba

d)     Atasimamia majukumu ya shughuli za kila siku

e)     Mpango wa kazi wa mwaka

 

II. KATIBU MIPANGO

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa na kazi zifuatazo:

a)     Atakuwa Mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha

b)     Atakuwa mbunifu na muandaaji wa mipango ya awali ya miradi ya maendeleo

c)     Atamsaidia mratibu wa fedha kubui na kutafuta vyanzo vya mapato

d)     Atasimamia miradi ya maendeleo

 

 

III. MRATIBU WA FEDHA

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atkuwa na kazi zifuatazo:-

a)     Atakuwa katibu wa kamati ya mpango na fedha

b)     Atatunza kumbukumbu zote za fedha

c)     Atabuni na kutafuta vyanzo vya mapato akisaidiwa na mratibu wa mipango / afisa mradi

d)     Atakuwa mshauri wa mambo ya fedha.

 

IV. MRATIBU WA ELIMU

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa na kazi zifuatazo

a)     Atashughulikia mipango ya elimu na mafunzo.

b)     Mtekelezaji msaidizi wa mipango ya elimu na mafunzo

c)     Atakuwa mratibu wa taratibu zote za utoaji na mafunzo.

d)     Atakuwa mratibu wa taratibu zote za utoaji wa elimu na mafunzo.

e)     Atakuwa mjumbe mshauri wa kamati ya mipango ya fedha.

 

4.4 MUDA WA UONGOZI

Muda wa uongozi utakuwa miaka mitatu lakini kiongozi aliyemaliza muda wake anaweza kuchaguliwa tena, bila ukomo kama anafaa.

 

5.0  SEHEMU YA TANO

5.1 AINA ZA VIKAO

Kutakuwa na aina tatu za vikao kama ifuatavyo:-

i)      Mkutano mkuu

     ii)    Kamati ya utekelezaji

iii)            Kamati ya mipango na fedha

 

5.2 WAJUMBE WA VIKAO

I. MKUTANO MKUU

Mkutano mkuu utakuwa na wajumbe wafuatao:

-        Mwenyekiti

-        Katibu

-        Wajumbe wawakilishi wa kamati zote.

-        Wanachama wote.

 

II. KAMATI YA UTEKELEZAJI

-        Mwenyekiti

-        Katibu

-        Mtunza Hazina

-        Wajumbe 3

 

III. KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA

-        Mwenyekiti

-        Katibu

-        Mweka Hazina

-        Wajumbe 3

 

 

 

5.3. MUDA WA VIKAO NA IDADI YA WAJUMBE

I. MKUTANO MKUU

Mkutano mkuu utafanyika mara moja kila mwaka lakini unaweza kufanyika wakati wowote kwa dharura. Ili kikao kiwe halali wajumbe wasipungue theluthi mbili ⅔.

 

 

II. KAMATI YA UTEKEZAJI  

a)     Kutoa mapendekezo juu ya miradi inayoendeshwa

b)     Kusaidia kusimamia na kutoa ushauri juu ya miradi inayoendesha

c)     Kusimamia shughuli za kila siku

d)     Kuandaa taarifa ya utekelezaji

e)     Kujadili na kutoa mapendekezo ya wanachama wapya

f)      Kutafuta wahisani kufanya tafiti na kusimamia shughuli zote.

g)     Kupitisha rasimu ya mipango ya maendeleo na kufanya marekebisho kabla haijafikishwa kwenye mkutano mkuu.

h)     Kuandaa mpango wa kazi unaofuata

i)      Kusimamia sera kanuni na katiba.

 

III. KAMATI YA UTEKELEZAJI

Kamati ya utekelezaji itakutana mara moja kwa kila miezi miwili lakini inaweza kukutana wakati wowote kwa dharura

 

IV. KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA

Kamati ya mipango na fedha itakutana mara moja kwa kila miezi miwili inaweza kukutana wakati wowote kwa dharura

 

5.4 KAZI ZA VIKAO

I. MKUTANO MKUU

a)     Kupokea kujadili kupitisha au kutopitisha taarifa ya mwaka

b)     Kila baada ya miaka mitatu kutakuwa na mkutano mkuu wa uchaguzi

c)     Kupitisha taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka uliopita mpango mpya wa matumizi na mapato.

d)     Kutathmini uendeshaji wa utekelezaji wa shughuli za shirika

e)     Kuwathibitisha wanachama wapya

 

Swaa-morogoro wapo hewani wakisubiri wabia kokote duniani shirika lolote ambalo lingependa kuungana nasi tunawakaribisha

HELLEN mbezi
MWENYEKITI
SWAA-MOROGORO