Log in
Society for Women and AIDS in Africa

Society for Women and AIDS in Africa

Misufini mtaa wa police, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Kutoa mafunzo ya elimu inayohusiana na ukimwi na ujasiriamali kwa jamii ya watu waishiyo Morogoro.

Latest Updates
Society for Women and AIDS in Africa added a News update.
Hawa ni watoto yatima wanaoishi katika wilaya ya mvomero katika kata ya turian, shirika limechukua hatua ya kuwasomesha kwa sababu wanaishi na bibi yao ambaye hana uwezo wa kuwasomesha. baba yao aliye wazaa yupo hai lakini naye hajiwezi kwa sababu ni mlemavu wa miguu. Mwananchi yeyote ambaye ameguswa na hili na... Read more
February 14, 2013
Society for Women and AIDS in Africa created a Volunteer page.
Shirika la SOCOETY FOR WOMEN AND AIDS INA AFRICA (SWAA) linapenda kufanya kazi na watu mbalimbali wa kujitolea maeneo ya vijijini hasa wilaya ya Mvomero Wilaya hii ipo katika mkoa wa Morogoro, na kwa sasa shrika linaendesha mafunzo juu ya Haki za Binadamu hususani sheria za watoto. Elimu hii kwa sasa inatolewa katika kamati za shule, wazazi... Read more
November 11, 2012
Society for Women and AIDS in Africa added 3 News updates.
Wanafunzi wa Sekondari ya Mziha wakisikiliza mragibishi akitoa elimu ya usafi na Uzazi kwa wanafunzi wa kike na wakiume mwezi wa tatu mwaka 2012 kama mpango wa kuelimisha jamii.
April 8, 2012
Society for Women and AIDS in Africa added 4 News updates.
Mr. kervin kutoka (The Faundation For Civil Society) akiwapa maelekezo wawakilishi wa asasi ya (SWAA-MO).
September 13, 2011
Society for Women and AIDS in Africa created a Team page.
MUUNDO WA SHIRIKA LETU – Mkutano mkuu- kikao kinafanyika mara moja kwa mwaka – Kamati ya utendaji- kikao hufanyika kila miezi mitatu – Kamati ndogo ambazo ni ya fedha, mipango na kamati kuu inayo unganisha wenyeviti na makatibu wote wa kamati ndogo. ... Read more
September 12, 2011
Society for Women and AIDS in Africa added 2 News updates.
September 4, 2011
Sectors
Location
Misufini mtaa wa police, Morogoro, Tanzania
See nearby organizations
constitition

KATIBA

 

 1. SEHEMU YA KWANZA

  1. JINA – SOCIETY FOR WOMWEN AND AIDS IN AFRICA – (SWAA)

  2. ADDRESS: P.O. BOX 762 – MOROGORO

  3. OFISI KUU: MOROGORO MANISPAA

  4. MMILIKI

 

  1.1 Wanachama wa kuchaguliwa waliotokana na shirika anzilishi liliitwa Society for women and   AIDS in Africa (SWAA)

 

2.0 SEHEMU YA PILI

2.1 Ufafanuzi

 • Shirika hili litajishughulisha na masuala yote ya kijinsia.

 • Shirika limesasajiliwa kwa mara ya pili kwa baada ya kupanua wigo shughuli zake kwa mujibu wa sheria, na sasa linaitwa SOCIETY FOR WOMWEN AND AIDS IN AFRICA – (SWAA) na uongozi ni wa kuchaguliwa.

 2.2 LENGO

 • Kutoa mafunzo mbalimbali kwa njia ya nadharia na sanaa za jukwaani (shirikishi) katika nyanja zote kulingana na mahitaji yaliyopo.

 2.3DIRA 

 • Ifikapo mwaka 2020 jamii iishiyo Morogoro itaweza/ wataweza kusimamia rasilimali zinawazunguka na kuzilinda. Pia kuzijua sheria za nchi na kuzisimamia.

 

2.4 MADHUMUNI

 • Kuunganisha jamii katika jukumu la kulinda rasilimali walizonazo na kuweza kuzitumia vema ili kuondoa umaskini. Pia kuelimisha kuhusu utawala bora na sheria za nchi.

 • Kuiwezesha jamii yote katika kutambua sheria zinazosimamia mirathi na kufanya tafiti mbalimbali kulingana na shughuli itakayokuwa inahitajika mfano Uchaguzi Mkuu, Sensa ya watu, na elimu kwa ujumla.

 • Kulinda ardhi inayowazunguka hasa kupinga mikataba isiyo rasmi.

 • Kulinda wanyama wanaishi katika misitu ya asili na kupiga vita uchomaji moto misitu yetu.

 • Kusimamia uoteshaji miti ya mbao ili kupunguza umaskini.

 • Kuunda vikundi kazi vya vijana walio nje ya shule na ndani ya shule vitakavyo pokea mafunzo na kuyafanyia kazi.

2.5SHUGHULI

 1. Jamii kufanya shughuli za ujasiriamali katika maeneo maalumu hasa katika kingo za misitu, mito za kuongeza kipato chao mfano ufugaji, wa nyuki na kilimo cha alizeti.

 2. Kuhamasisha jamii na taasisi za uma kuhusu dhana ya utawala Bora.

 3. Kufanya uhamasishaji wa kilimo kisicho rasmi kinachoweza kuharibu misitu yetu na vyanzo vya mito.

 4. Kusimamia vikundi vilivyoundwa katika jamii shughuli mbalimbali vya kazi ili kuondoa umaskini.

 5. Kubuni miradi mbalimbali itaakAyoshirikisha makundi mengine wakiwepo vijana na wanaume ili kuboresha maisha yao.

 6. Kupiga vita taratibu zote zinazokwenda kinyume na hali za binadamu

 7. Kushawishi vyombo vya serikali kufanya kazi na shirika hili ili kuifikia jamii mapema katika shughuli zote zitakazohusu jamii moja kwa mja.

 8. Kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kuzalisha mazo bora ili kuinua kipato chao.

 9. KUPOKEA WAGENI WAKUJITOLEA(VOLUNTIES) NDANI NA NNJE WENYE NIA NA MADHUMUNI YA KUFANYA KAZI ZINAZOFANANA NA SHIRIKA HILI.

 

3.0 SEHEMU YA TATU

3.1 MASHARTI / SIFA ZA WANACHAMA

 • Mwanaume na mwanamke yeyote aliye na umri kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea

 • Wataalamu wa mambo ya jenda na misitu hasa wanawake

 • Mwanachama awe na uwezo wa kazi za kujitolea na akuali utaalamu wake utumike na wengine

3.2SEHEMU YA TATU

Kutakuwa na aina mbili za uanachama

 1. Wnachama wa kudumu

 2. Wanachama wa heshima 

 • Wanachama wa kudumu ni wale ambao kwa hiyari yao wameomba uanachama na kukubaliwa kwa mujibu wa katiba.

 • Wanachama wa (Heshima) ni wale kwa utaalamu wao na wadhifa wao wamekubali kujitoa kwa hali na mali kujiunga kuendeleza shirika kwa hali na mali pia kitaaluma

3.3 UTARATIBU WA KUJIUNGA

  1. Kutakuwa na fomu maalum ya maombi ya uachama ambayo utalipiwa shilingi 20,000/= na ambayo hazitarudishwa, bila ya kujali umekubaliwa au umekataliwa.

  2. Fomu itajazwa na mwenyewe na ya kuomba uanachama kasha itapelekwa kwenye kamati ya utekelezaji.

  3. Itajadiliwa katika kamati ya utekelezaji na kutoa mapendekezo yake hatimaye kupelekwa kwenye mkutano mkuu kwa kuthibitisha.

  4. Akikubaliwa atapaswa kulipa kiingilio cha shilingi 30,000/= na ada ya kila mwaka Tshs 20,000/=

3.4 HAKI NA WAJIBU

a) HAKI

 • Mwanachama anayo haki kujiunga na vikundi vingine

 • Anayo haki kuchagua kuchaguliwa

 • Kudhamini kitu kadri anavyojiamini

 • Akiacha uanachama kwa sababu za msingi uongozi utakutana kujadili kuwa ni haki gani anayostahili kupewa.

 • Akipata tatizo yeye mwenyewe shirika linaweza kumsaidia endapo hali itaruhusu.

 • Anayo haki kusiriki au kushirikishwa katika shughuli zote.

3.5 KUACHA UANACHAMA

 1. Mwanachama ataacha uanachama kwa:-

 2. Kujitoa yeye mwenyewe

 3. Kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu

 4. Kifo au kuvunjika kwa kikundi

 5. Kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa ya maandishi.

 6. Kutotimiza taratibu zilizowekwa kikatiba

 

4.0 SEHEMU YA NJE

4.1 UONGOZI

Viongozi wafuatao ambao watachaguliwa na mkutano mkuu:

  1. Mwenyekiti

  2. Mratibu wa mipango

  3. Mratibu wa fedha

  4. Mratibu wa Elimu

4.2 SIFA ZA UONGOZI

 1. Mwenye uwezo wa kuongoza

 2. Mwenye uwezo wa kusuluhisha migogoro ndani na nje ya shirika

 3. Mwenye uwezo wa kugundu matatizo kuyatafutia ufumbuzi wa haraka

 4. Mwenye kupanga mipango na kutekeleza

 5. Mvumilivu, mpole mnyenyekevu na asiye kata tama

 6. Mwenye uwezo wa kujieleza kushawishi na anayekubalika

4.3 WAJIBU WA VIONGOZI

 1. Mwenye uwezo wa kuongoza

 2. Mwenye wa kusuluhisha migogoro ndani ya nje ya shirika

 3. Mwenye uwezo wa kugundua matatizo kuyatafutia ufumbuzi wa haraka

 4. Mwenye kupanga mipango na kuteleza

 5. Mvumilivu, mpole, mnyenyekevu na asiye kata tama

 6. Mwenye uwezo wa kujieleza kushawishi na anayekubalika.

4.3 WAJIBU WA VIONGOZI

 1. Mwenyekiti

Atachaguliwa na mkutano mkuu wa atakuwa na majukumu yafuatayo:-

 1. Atakuwa Mwenyekiti wa mikutano kamati ya utekelezaji

 2. Atakuwa msemaji mkuu wa shirika

 3. Atalinda sera kanuni na katiba

 4. Atasimamia majukumu ya shughuli za kila siku

 5. Mpango wa kazi wa mwaka

II. KATIBU MIPANGO

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa na kazi zifuatazo:

 1. Atakuwa Mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha

 2. Atakuwa mbunifu na muandaaji wa mipango ya awali ya miradi ya maendeleo

 3. Atamsaidia mratibu wa fedha kubui na kutafuta vyanzo vya mapato

 4. Atasimamia miradi ya maendeleo

III. MRATIBU WA FEDHA

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atkuwa na kazi zifuatazo:-

 1. Atakuwa katibu wa kamati ya mpango na fedha

 2. Atatunza kumbukumbu zote za fedha

 3. Atabuni na kutafuta vyanzo vya mapato akisaidiwa na mratibu wa mipango / afisa mradi

 4. Atakuwa mshauri wa mambo ya fedha. 

IV. MRATIBU WA ELIMU

Atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa na kazi zifuatazo

 1. Atashughulikia mipango ya elimu na mafunzo.

 2. Mtekelezaji msaidizi wa mipango ya elimu na mafunzo

 3. Atakuwa mratibu wa taratibu zote za utoaji na mafunzo.

 4. Atakuwa mratibu wa taratibu zote za utoaji wa elimu na mafunzo.

 5. Atakuwa mjumbe mshauri wa kamati ya mipango ya fedha. 

4.4 MUDA WA UONGOZI

Muda wa uongozi utakuwa miaka mitatu lakini kiongozi aliyemaliza muda wake anaweza kuchaguliwa tena, bila ukomo kama anafaa.

 

5.0 SEHEMU YA TANO

5.1 AINA ZA VIKAO

Kutakuwa na aina tatu za vikao kama ifuatavyo:-

  i)Mkutano mkuu

  ii) Kamati ya utekelezaji

  iii)Kamati ya mipango na fedha

5.2 WAJUMBE WA VIKAO

I. MKUTANO MKUU

Mkutano mkuu utakuwa na wajumbe wafuatao:

 • Mwenyekiti

 • Katibu

 • Wajumbe wawakilishi wa kamati zote.

 • Wanachama wote.

II. KAMATI YA UTEKELEZAJI

 • Mwenyekiti

 • Katibu

 • Mtunza Hazina

 • Wajumbe 3

III. KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA

 • Mwenyekiti

 • Katibu

 • Mweka Hazina

 • Wajumbe 3

5.3. MUDA WA VIKAO NA IDADI YA WAJUMBE

I. MKUTANO MKUU

Mkutano mkuu utafanyika mara moja kila mwaka lakini unaweza kufanyika wakati wowote kwa dharura. Ili kikao kiwe halali wajumbe wasipungue theluthi mbili ⅔.

 

II. KAMATI YA UTEKEZAJI

 1. Kutoa mapendekezo juu ya miradi inayoendeshwa

 2. Kusaidia kusimamia na kutoa ushauri juu ya miradi inayoendesha

 3. Kusimamia shughuli za kila siku

 4. Kuandaa taarifa ya utekelezaji

 5. Kujadili na kutoa mapendekezo ya wanachama wapya

 6. Kutafuta wahisani kufanya tafiti na kusimamia shughuli zote.

 7. Kupitisha rasimu ya mipango ya maendeleo na kufanya marekebisho kabla haijafikishwa kwenye mkutano mkuu.

 8. Kuandaa mpango wa kazi unaofuata

 9. Kusimamia sera kanuni na katiba.

III. KAMATI YA UTEKELEZAJI

Kamati ya utekelezaji itakutana mara moja kwa kila miezi miwili lakini inaweza kukutana wakati wowote kwa dharura

 

IV. KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA

Kamati ya mipango na fedha itakutana mara moja kwa kila miezi miwili inaweza kukutana wakati wowote kwa dharura

 

5.4 KAZI ZA VIKAO

I. MKUTANO MKUU

 1. Kupokea kujadili kupitisha au kutopitisha taarifa ya mwaka

 2. Kila baada ya miaka mitatu kutakuwa na mkutano mkuu wa uchaguzi

 3. Kupitisha taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka uliopita mpango mpya wa matumizi na mapato.

 4. Kutathmini uendeshaji wa utekelezaji wa shughuli za shirika

 5. Kuwathibitisha wanachama wapya

 6. Kupitisha mpango wa kazi wa mwaka

 7. Kujadili na kutoa mapendekezo juu ya wanachama waliokwenda kinyume na taratibu.

 8. Kupitisha miradi ya maendeleo.

II. HIFADHI

Fedha za chama zinahifadhiwa kwenye benki ya NMB itakayokubaliwa na wanachama. Jina laakaunti litakuwa SOCIETY FOR WOMWEN AND AIDS IN AFRICA – (SWAA)) fedha itawekwa na mtu yeyote kwa jina la akaunti ya (SWAA) NMB – Wami – Morogoro.

 

III. UTOAJI WA FEDHA BANK

Fedha zitatolewa kwa saini ya watu watatu kama ifuatavyo:

 • Mwenyekiti

 • Katibu

 • Mweka Hazina

 • Wawili kati ya hawa wanaweza kuchukua fedha.

IV. UTHIBITI WA FEDHA

Kila mwaka kutakuwa na wakaguzi wa ndani na nje endapo kutakuwa na fungu la kugharamia kazi hiyo.

III. MWAKA WA FEDHA

Mwaka wa fedha utakuwa July

 

6.0 MENGINEYO

 1.  
 2.    UTARATIBU WA KAZI NDANI YA SHIRIKA

Shirika litahakikisha kuwa mwanachama yeyote hadhurumiwi pia ndio watakaosimamia na kutoa ushauri wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kila siku

Kazi zote za wanachama zitapitia kwenye shirika.

 

7.1 UHAI WA MUUNGANO

 1. Uhai wa muungano wa shirika hutategemea sana uhai wa wanachama. Hivyo kila mwanachama anatakiwa kudumisha uhai wake na uwepo wake ili kuufanya muungano uweze kudumu na kuendelea.

 2. Endapo shirika litakufa basi wanachama hai wanawajibika kwa yafuatayo

 • Kulipa madeni yanayodaiwa

 • Kudai na kukusanywa madeni yote shirika linalodai.

 • Kufanya mgao wa fedha kwa wanachama hai chini ya usimamizi wa ofisi ya maendeleo ya jamii iliyopo wilayani.

 • Shirika litakuwa na nguvu kwa kuwa na mshikamano uelewano na udugu na kauli moja kwa hiyo mwanachama anaweza kupoteza uanachama wake kutokana na majungu, ubinafsi, dhuruma na ubadhilifu. Ukweli na uwazi utawezasha shirika linakua na kuendelea.

7.2 MABADILIKO YA KATIBA

 1. Mabadiliko ya katiba yatafanywa kwa idhini ya mkutano mkuu tu.

 2. Mabadiliko yanaweza kufanyika kwa mujibu wa katiba kwa ajumbe wenye haki ya mkutano mkuu.