Log in
JOINT INITIATIVES FOR VULNERABLES SUPPORT (MZEITUNI).

JOINT INITIATIVES FOR VULNERABLES SUPPORT (MZEITUNI).

Nyegezi Mwanza, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

INSHA YANGU: ATHARI ZA VIRUSI VYA CORONA MWIBA WA NYIKA KWA WASIOONA NA WATU WENYE ULEMAVU WA VIUNGO NCHINI TANZANIA.

Jina kamili: Meshack Kisendi Masanja.

S.L.P 6085, Mwanza Tanzania.

Simu: +2550768177003.

Email: masanjameshack70@yahoo.com

Tarehe ya kuzaliwa: 16/8/1970.

Aina ya ulemavu: Asiyeona.

Jinsia: Mwanaume.

 

 

Kwa kipindi cha miezi mitatu yaani kuanzia March-June/2020 ikiwa ni baada ya serikali ya Tanzania kutangaza rasmi juu ya namna ya kila mwananchi kutambua, kuchukua hatua za kujikinga, kuzuia na kutoa taarifa ama kujitokeza kupima endapo atagundua kuwa na dalili za kuwa na virusi vya Corona katika vituo vya afya, Baadhi ya makundi ya watu wenye ulemavu yaani; Wasioona, Wenye uoni hafifu na Watu wenye ulemavu wa viungo ambao walikuwa wakipata mahitaji yao kwa njia ya kuombaomba mitaani waliweza kukabiliwa na changamoto za njaa, unyanyapaa, ubaguzi na kushindwa kabisa kupata mahitaji ya kila siku kulingana na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la afya la ulimwengu (WHO) kutangaza njia zinazopaswa kuchukuliwa na kila mtu katika kuyakabili maambukizi ya virusi vya Corona.

Baadhi ya kanuni zilizowekwa na kusababisha shida na dhiki kwa makundi hay ani; 1. Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka kwa sabuni ama kwa kutumia kitakasa mikono.

2. kutokugusa uso, pua,, macho na mdomo.

3. kutokushikana ama kusalimiana kwa kumshika mkono mtu ye yote.

4. kukaa umbali wa mita moja hadi tat una mtu unayemhitaji kuzungumza naye ana kwa ana.

Kanuni hizi zilileta dhahama kubwa kwani kwa Wasioona Maisha yao ya kila siku hutegemea sana milango ya fahamu ya kugusa, kushika, kusikia na kunusa jambo ambalo lilikuwa linashikiliwa kwa asilimia 99 na kanuni nilizozitaja hapo juu, Kulingana na adha hii, Makundi haya yay a Watu wenye ulemavu yaliweza kuwa ni waathirika wakuu kwani hata ile misaada waliyokuwa wakiikusanya toka kwa wasamaria, wapendwa wenye huruma na hisani hawakuonekana tena na hata watu wenye ulemavu wenyewe waliingiwa na hofu kubwa dhidi ya kifo inayosababishwa na kuenea na kuambukizwa kwa virusi vya Corona.

Hebu fikiria> Asiyeona anapogundulika kuwa ameambukizwa virusi vya Corona na anatakiwa kukaa karantini kwa siku 14 ni maswaibu gani yanayomkuta tofauti na yule anayeona? Wapo watu wenye ulemavu waliopoteza uhai wao kutokana na kukutwa na kushambuliwa na virusi vya Corona mwenyezi Mungu na azilaze roho zao peponi.

Janga hili limetufundisha mambo mengi hususan sisi watu wenye ulemavu, Kwani katika kipindi hicho wenye daladala waliweza kukataa Wasioona na Wenye ulemavu wa viungo kupanda magari yao kwakuwa tu wakiwashika wanaweza kuwaambukiza virusi vya Corona, Licha ya uwepo wa matukio kadha wa kadha yenye kuonesha unyanyapaa na ubaguzi unaotokana na matokeo ya athari za COVID-19 Ni vema tukaikumbusha serikali, Wadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla kwamba, majanga mbalimbali yanapotokea ni vema ubunifu wo wote unaobuniwa ili kuyakabili majanga hay ani vema uwe ni ule usiotenga kundi lolote la watu, ni vema ukawa shiriki, shirikishi na jumuishi, wenye kuzingatia mazingira Rafiki kwa kila mtu, usiovunja utu wa mtu wala heshima yake, Uwe wenye kulenga na kutoa thamani kwa kila mtu kwani hakuna haki bila watu wenye ulemavu.

Katika kipindi hicho, Watu wenye ulemavu tulishuhudia misaada ikitolewa kwa taasisi za afya pasipo kukumbuka kuwa yapo makundi ya watu wenye ulemavu ambayo hana uwezo wa kupata Barakoa, vifaa vya kunawia mikono na sabuni, Hata wabunifu wa Barakoa na vifaa vingine walipoanza kufanya ugunduzi wao walitengeneza vifaa vyao pasipo kufikiria kuwa Asiyeoona akivaa Barakoa yenye lastiki ya kubana masikio ataweza kusikia maumivu sana hali angali akiyategemea masikio hay ohayo katika kusikiliza vema, kufunikwa kwa pua kunamfanya asiweze kunusa vema ili kutambua anachokihitaji ili kumudu shughuli zake za kila siku, Wengine walitengeneza vifaa vya kunawia mikono vyenye kutumia mguu kukanyaga ili maji na sabuni viweze kutoka huku wakijua kuwa wapo watu wenye ulemavu wa viungo ambao hawawezi kutumia mguu kupata huduma hiyo, Hivyo basi, Hali hii, iliweza kubainisha wazi ukiukwaji na uvunjwaji wa sharia ya watu wenye ulemavu na hakuna chombo cho chote kilichoweza kusimamia ama kutoa maamuzi yenye kuwasaidia na kulind haki ya mahitaji ya wenye ulemavu japokuwa viongozi wenye mamlaka, watoa maamuzi na watunga sera walikuwepo wakitoa maelekezo na maagizo ya namna ya kulinusuru taifa letu dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Watu wenye ulemavu nchini Tanzania inatupasa tushikamane kwa pamoja katika kuitetea, kuisukuma na kuifuatilia sharia namba 9 ya mwaka 2010 (sharia ya watu wenye ulemavu ya Haki, Ulinzi na usalama) ikiwa ni nyenzo munimu ya kutokomboa dhidi ya vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi katika mapambano ya ubora na thamani ya Maisha yetu.


The Call to Action on Domestic Financing of Education post-Covid has now
been signed on to by an incredible list of 190 organisations from 55
countries and is publicly launched today, which is UN International
Literacy Day.

There is a short blog that I have drafted about this call to action,
which you can access here:

https://actionaid.org/opinions/2020/international-literacy-day-covid-19s-impact-equality-education

And the link to the final call to action with the full list of 190
organisations is here:

https://actionaid.org/sites/default/files/publications/Call%20to%20action%20on%20domestic%20financing%20of%20education%20WITH%20SIGN%20ONs.pdf