Eleza Uzoefu na Mawazo yoyote mapya mliyoyapata kutokana na kutekeleza shughuli za mradi huu
Maelezo |
---|
Most of community leaders are not aware of; and have not seen the National Environmental Policy of 1992. The policy has not been disseminated. |
There is intefearance in the enforcement of laws and regualation by higher authority. |
It is important to involve beneficiaries and stakeholders from outside the organisation in the evaluation of the project in order to get wider views and critical analysis of the report. |
Maelezo |
---|
The use of an improved firewood Cooking stove, to reduce the consumption of fire wood for energy purposes is ideal and very important in the conservation , management and protection of the Environment |
The increased and Continued empowerment of community based Soils and Water resources’ management around the water Sources may bring an eventual change of behavior in the management of the natural resources |
The use of women and women groups organizations in the Water services Management is a very Pivotal agenda of action that can Support the mass tree cutting |
The empowerment of the local Media groups and enhancing of the rural media power and capacities in development and protection of the natural resources is very important in exposing the environmental tyranny and the destruction of the Environment and its Biodiversity |
Maelezo |
---|
Kutokuwepo kwa mahusiano na ushirikiano usioridhisha/ sio mzuri kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa na wawakilishi wa AZAKi na wananchi kiujumla kuhusu michakato ya sera na maendeleo. |
Wananchi hawashirkishwi kikamilifu na ipasavyo katika michakato ya uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika ngazi ya vijiji.mitaa, vitongoji na kata. |
Mipango na miradi ya maendeleo katika Halmashauri za wilaya/Manispaa haitekelezwi kama ipasavyo na sawa na ilivyokusudiwa. |
Kukosekana kwa uwazi wa kutosha na uwajibikaji duni kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi. |
Wananchi kukosa uelewa juu ya haki na wajibu wao katika michakato ya sera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kupelekea kuwepo kwa ushiriki duni. |
AZAKi nyingi hazina uwezo, maarifa wala mbinu za kufanya ushiwishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki/kushirikishwa katika hatua tofauti za michakato ya kisera na maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. |
Maelezo |
---|
Kutakana na utedkelezaji wa mradi huu, viongozi na wanachama kwa jumla wamefahamu wajibu wao. |
Tum ekuwa na uhusiano mzuri baina ya Asasi ya Bagamoyo care organization na viongozi wa serikari kuu na Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo. |
Asasi imeadhimia mara tutapomaliza mradi huu tutawasilisha andiko la miradi mwingine ambao tutawafikia walengwa wetu waliomo ndani ya katiba |
Maelezo |
---|
Training in capacity building is important because it improves the ability of organization to run the projects. |
Maelezo |
---|
wananchi wengi bado waoga wa kutoa taarifa kwa TAKUKURU kwa sababu wanahisi nao pia wanashirikiana na watoa Rushwa. |
Wakati wa ufuatiliaji wananchi wengi wanasema vita dhidi ya Rushwa ni ngumu kwa sababu wakubwa wanawalinda wala Rushwa wakubwa. Pia kwamba huwezi kupata uongozi wa siasa bila kutoa Rushwa. |
- |
- |
- |
- |
Maelezo |
---|
Ili asasi iweze kufanya vizuri katika shughuli zake mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama ni jambo la lazima |
Asasi ni chombo hai, uhai wake hutoweka ikiwa hakuna mfumo ndani ya asasi ambao unachochea kukua kwake, hii inamaanisha kwamba kusipokuwepo na mifumo iliyowazi kiutendaji\ uwajibikaji |
Asasi inatakiwa kubuni na kuanzisha miradi ambayo itaingiza fedha kuliko kutegemea wafadhili pekee, kwani kutegemea wafadhili kwakila jambo ni hatari kwa ustawi na uhai wa asasi |
Asasi ili ikubalike kwa jamii inapswa kuwa wazi kwa wadau mbalimbali kwani uwazi huo utasababisha kufahamika kwa mafanikio na matatizo yanayoikabili asasi na kwamba katika hali hiyo hatua za kutatua matatizo na au kufaidi matunda ya shughuli za asasi kuhusisha jamii nzima. |
Maelezo |
---|
ELIMU KUHUSU SERA SHIRIKISHI HAIJAWAHI KUTOLEWA KWA JAMII |
KAESO IMEUNGANISHA KAMATI ZA MAZINGIRA ZA VIJIJI NA MAAFISA MISITU WA HALMASHAURI YA WILAYA |
KAMATI ZITOA MAPENDEKEZO YA ADHABU KWA WAHARIBIFU WA MISITU NA KUPELEKWA KWENYE VIKAO VYA KATA . |
Maelezo |
---|
Licha ya mila potofu kutoa mchango mkubwa kwa wanaume wengi kuwanyima wanawake haki zao, wanaume wengi walikuwa kikwazo kikubwa katika kuwapa wanawake haki yao ya kumiliki ardhi na hivyo tulipofika kijiji cha Amani wanawake waliomba kuwa katika timu itakayoendelea kutoa elimu wanaomba wanaume wahusike pia |
Wanasemina waliomba semina hiyo isiishie kutoa elimu juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi pekee bali iende hadi kumilikisha mali nyingine na haki za wajane pale waume zao wanapokuwa wamefariki |
Tumejifunza kuwa baadhi ya viongozi wa serikali ya vijiji hawaungi mkono jitihada za Asaasi za kiraia, kwani kila tulipowashiorikisha hawakuwa karibu sana nasi kama Asasi. |
Wanajamii na viongozi wa vijiji hawana uelewa juu ya sheria ya ardhi na. 5 ya mwaka 1999 sera ya maendeleo ya mwanamke ya mwaka 2002 |
Maelezo |
---|
Watu wenye ulemavu wamesahaulika katika kujengewa uwezo na uelewa kuhusu Sera na Sheria mbalimbali zinazolenga kulinda na kutetea haki zao. |
Watu wenye ulemavu hawajapatiwa nafasi na fursa ya kutosha ya kushiriki kikamilifu katika machakato mbalimbali ya kimaendeleo. |
Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo hawajakidhi haja na mahitaji ya watu wenye ulemavu kujiwezesha kujiletea maendeleo wao wenyewe. |
Watu wengi wenye ulemavu hawana kabisa na/au wana kiwango duni cha elimu hali inayosababisha na kupelekea kushindwa kukabiliana na mazingira yanayowazuguka na changamoto mbalimbali za kimaendeleo. |
Jamii bado ina mtizamo hasi na potofu kuhusu haki, wajibu na nafasi ya watu wenye ulemavu kiushiriki kikamilifu katika michakato tauti ya maendelo. |
Kukosekana kwa muda mrefu na kucheleweshwa utungaji na utekelezaji wa Sheria Na. 10 ya 2010 ya Watu Wenye Ulemavu imepelekea utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Watu wenye ulemavu kufanyika kutokana na matakwa na utashi wa mtu mmoja mmoja badala ya kuwa kwa mujibu ya sheria halali za nchi. |
Maelezo |
---|
Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mradi huu, tumepata mawazo makuu mapya yafuatayo kama sehemu ya uzoefu: 1. Sera nyingi zinazoandaliwa na serikali hazifiki/kuwafikia wadau wa maendeleo haswa ngazi ya Kata na Vijiji. 2. Katika kutekeleza mradi huu, tumejifunza kuwa ndoa nyingi ziko katika mazingira magumu kutokana na hali ya mfume dume kuendelea kushamiri katika maeneo yote ya tulikotekeleza mradi huu. 3.Viongozi wengi wa mabaraza ya Kata hawajui wajibu wao. |
Mabaraza ya Kata yaliyo mengi yanaendesha shughuli za utoaji haki kwa uzoefu na hayana mwongozo wa sheria mbalimbali. |
Ipo haja ya asasi za kirai kusaidia kuwajengea uwezo jamii haswa wale walioko katika famili kufundishwa juu ya kuwa na maadili mema, haswa katika kipindi cha malezi ya mtoto ili kuwa na taifa lenye viongozi na jamii bora siku zijazo. |
Tumejifunza kuwa vyombo vya habari ni mhimu sana katika kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hivyo itasaidia jamii kubwa zaidi kushiriki katika mijadala kwa njia ya radio, hatimaye jamii itakuwa na mabadiliko makubwa kijamii, kielimu, kiutamaduni na kiuchumi. |
Utegemezi wa vyombo vya usafiri kwa asasi za kiraia unaweza kuchangia kuchelewa kufikia malengo waliyojipangia. |
Mfumo wa mahusiano ya viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Kata hadi Vijiji unachangia kuzorotesha masuala ya utekelezaji wa sera haswa ya maendeleoa ya wanawake na jinsia. hivyo tumejifunza kwamba ipo haja ya asasi za kiraia kutoa elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa toka ngazi ya Wilaya hadi Kijiji ili watambue umhimu wa siasa katika kutekeleza sera mbalimbali za Serikali. |
Maelezo |
---|
1. Jamii ya watu wa Kibindu kwa ujumla wake hawajui namna ya kuwatumia wataalam na fursa zilizo wazunguka katika maeneo yao. Mf: Misitu, na ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo lakini makazi yao ni duni mno. Halmashauri ilileta Trecta kijijini hapo ili wananchi waweze kuongeza kilimo kwa kupanua mashamba yao, lakini Trecta walikataa kulitumia walisema kuwa eti inatifua kama NGIRI |
Kata ya Kibindu vitendo vya kishirikina vimeshika hatamu sana. Hii inatokana na kile tulichoelezwa kuwa watu wa Kibindu wanashindwa kujenga nyumba bora na kuanzisha biashara kwa hofu ya kupigwa ZONGO (Kulogwa). |
3. Katika Kata ya Kibindu wananchi wana mwitikio mkubwa sana kwenye mambo ya semina na warsha, lakini hawana mwitikio katika shughuli za maendeleo ya vijiji vyao. Mf: Kuna jengo moja kijiji cha Kibindu lilianzishwa mwaka 2007 kwa msaada wa SIDO ili wanakijiji waletewe mashine ya kusindika unga wa muhogo. Lakini hadi hivi leo limebakia pale pale ulipoishia msaada wa SIDO. Wananchi hawana moyo wa kujitolea na kujituma kwa ajili ya maendeleo yao. Jambo wanalipokea vizuri lakini mwisho wa siku wanaliachia pale pale bila kuanza kulitekeleza. Mhe Diwani ndugu Komu wa kata ya Kibindu alitoa falsafa ya U – 3 kwa maana ya Utambuzi, Uchambuzi na Utekelezaji. Alimalizia kwa kusema kwamba wananchi wake mambo mawili ya mwanzo wanayajua isipokuwa hilo la tatu la utekelezaji ndio mgogoro ulipo. |
Viongozi wengi wako katika nafasi za uongozi lakini hawana mafunzo maalum ya uongozi na utawala bora. |
Vikundi vingi vinajiendesha bila ya kuwa na dira, dhamira na malengo ya pamoja. Vikundi vingi havina katiba. |
Ilibainika kuwa katika kata ya Kibindu hakuna utawala wa sheria unaowabana wenyeviti wa vitongoji na kuwazuia wasiuze ardhi vijijini. |
Maelezo |
---|
Kuwa ukishirikisha jamii katika mipango na utekelezaji jamii inatoa ushirkiano mzuri. |
Tumejifunza kuawa miradi mingine inakwama kufanikiwa ni kutokana na viongozi kuweka maslahi yao mbele kwanza kuliko walengwa |
Tumejifunza kuwa kufanya mradi kipindi cha uchaguzi utekelezaji wake unakuwa mgumu kutokana na wanasiasa kutotoa ushirikiano kuogopa kutochaguliwa na wananchi. |
Tumejifunza kuwa kumbe watoto wengi wanapenda kwenda shuleni lakini wanashindwa kutokana na kutokuwa na mahitaji muhimu ya shuleni pamoja na sare. |
Maelezo |
---|
Wazo jipya tulilolipata katika kutekeleza mradi huu ni kwamba wanaume wakipata elimu ya kweli na ya kutosha juu ya haki za wanawake wanabadilika na wanapata mwitikio mkubwa pindi wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwani hata wanaume wenzao huwasikiliza kuliko mwanamke kusikilizwa kutokana na hali ya dharau iliyojengeka katika jamii kwamba mwanamke hapaswi kusikilizwa, kwa hiyo wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwa mwanamke ni faida kubwa. |
Wazo jingine ni kwamba pamoja na harakati nyingi za ukombozi kwa mwanamke zinazoendeshwa na asasi mbalimbali Tanzania, bado hali ya mateso kwa mwanamke wa kijijini ni kubwa, wanawake bado wanabakwa, wanapigwa, wananyimwa nafasi za ushiriki katika mipango ya maendeleo, kiujumla hawasikilizwi, hivyo bado tunakazi kubwa ya kufikia Wilaya yote ya Rungwe hasa tukilenga kuelimisha wanaume na viongozi wa vijiji. |
Bado viongozi wengi wa vijiji ni madikteta, wananchi wananyanyaswa na kupewa adhabu na faini zisizo na msingi, mfano washiriki wawili waliochelewa mafunzo tuliyokuwa tukiendesha kwa sababu za kufiwa , Mtendaji aliposikia hawajafika kwenye mafunzo kesho yake walipokuja aliweza kuwapigisha magoti kwa muda mrefu na kuwaamuru warudishe posho walizopewa kwenye mafunzo na faini ya elfu kumi kila mmoja kwa ajili ya mgambo aliyewafuata, kwakweli kama shangwe tulikataa wale akinamama kuturudishia posho, lakini ile faini ya mgambo aliwaamuru watoe, kwa kweli wenzetu vijijini wanateseka na hawa viongozi wa kata na vijiji. Yaani viongozi hao wanaabudiwa ni mungu watu. |
Katika kutekeleza miradi mingine inayokuja , kama tutaendelea kuwa pamoja, tumegundua ni vema kutenga fungu la msaada wa kisheria kwa wanawake, kwani tumekutana na kesi nyingi za uonevu na manyanyaso juu ya wanawake zinazohitaji fedha kwa ajili ya msaada wa kisheria lakini tumekwama, japo kesi zingine zilizokuwa ni mbaya sana ilibidi tuchangie kutoka mifukoni mwetu ili kuweza kunusuru hali zilizokuwa zikiendelea. |
Jambo jingine muhimu tulilojifunza ni kuhamasisha wanasheria sasa kufungua matawi yao vijijini hasa wanasheria wanawake kwani mateso ya wanawake vijijini ni makubwa sana kuliko mjini ambako wanawake wengi mjini wanatambua haki zao, katika miradi ijayo tumeona vema kutenga fungu kwa ajili ya kuhamasisha wanasheria na watetezi wa haki waliopo mjini wakitafuta ajira wafungue matawi vijijini kazi zipo nyingi. |
Wanawake wa vijijini ni waelewa sana na wanakiu ya kujifunza na kutafiti mambo muhimu yanayoendelea katika Nchi yetu. |
Maelezo |
---|
Baadhi ya viongozi wa vijiji na hata kata huwa hawaitishi mikutano kwa kuogopa kuulizwa maswali ambayo hawana majibu yake maana wanafahamu ukiukaji walioufanya |
Dola inawajengea uadui wanaharakati wanaotaka kuanzisha shughuli za maendeleo maana wakifanikiwa itawajenga hivyo inawazuia wananchi kunufaika |
Mradi umethibitisha kuwa wanyonge na wasiojiweza bado wanaendelea kukosa haki zao mbele ya watensaji wa Serikali mfano:- (a) Katika mji wa Makambako (Jimbo la Njomba Kaskazini) mwanamke mjane aliulizia kujenga nyumba ya kuishi na familia yake- alizuiliwa na Mkurugenzi kwa kumwambia haparuhusiwi kujengwa chochote lakini baada ya siku chache tajiri mmoja ameruhusiwa kujenga (b) Mjini Makambako, kuna eneo walizuiliwa wafanyabiashara kujenga na kufunga mashine za kukoboa mpunga kwa sababu ya kulinda afya za wananchi KUZUIA VUMBI) lakini baada ya siku chache tajiri mmoja aliruhusiwa kujenga ghala la kuhifadhi simenti! FEDHA/RUSHWA INAPOFUSHA NA AFYA ZA WANANCHI ZIMEINGIA HATARINI ZAIDI |
Baadhi ya wachabuliwa (Wabunge na Madiwani) huwanyanyapaa kwa kuwanyima huduma watu walio katika maeneo ambayo walipata kura chache jambo ambalo ni kinyume na utawala bora |
Katika maeneo ya utawala ambayo viongozi wanatoka familia moja, mwananchi akipeleka matatizo anaundiwa visa kwa kulinda maslahi ya familia yao. Wananchi hawana mahali pa kukimbilia kutatuliwa matatizo yao. (Kata ya Mdandu, Wilaya ya Wanin'gombe Diwani mwanamke na mume wake ni Katibu Kata, Shule ya Sekondari Mazombe katika Wilaya ya Kilolo, Mwanaume ni Mwenyekiti wa bodi ya shulke wakati mkewe ndiye mkuu wa shule |
Wananchi wamewatuhumu baadhi ya viongozi wao kutopendelea wananchi kuhudhuria katika mikutano na kushiriki kwa kuuliza maswali. Hutuma watu wa kuangalia nani alihudhuria na kuzungumza mambo gani, akiambiwa kuwa alilalamikiwa na mtu fulani basi mtu huyo huandamwa na manyanyaso |
Maelezo |
---|
Ushiriki wa wanawake katika mikutano ulikuwa mkubwa kuliko wa wanaume pia wanawake ni wajasiri zaidi wenye ari na moyo wa kuwawazi na kusaidia jamii |
Mfumo wa kutoa elimu kwa jamii ni dhaifu na pia hakuna vifaa za kusaidia utoaji elimu kwa umma kwa urahisi |
Mfumo rasmi wa kutoa ushauri na huduma za tiba kwa umma haupo na vituo vya upimaji |
Upimaji vvu ni vichache katika manispaa ya arusha |
Hakuna mfumo rasmi wa utoaji habari na mawasiliano sahih kati ya serikali za mitaa na asasi za kijamii na jamii |
Tiba ya ukimwi bado ni tatizo na kuna ongezeko kubwa la huduma ya tiba mbadla ya jadi na asili inayoendana na ongezeko ya dhana inayoendana na ongezeko ya dhana potofu ya kuamini tiba mbadala |
Maelezo |
---|
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI bado wanahitaji kujengewa uwezo zaidi kwa maarifa na stadi ili waweze kuboresha utoaji wa huduma na kuleta ufanisi. |
Watoa huduma kwa wagomjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo wanaoishi na VVU/UKIMWI wanahitaji motisha ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi. |
Baadhi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI (ARVs) hulazimika kusafiri umbali mrefu kufikia kilomita zaidi ya 30 ili kufika katika vituo vya kutolea / kupokelea ARVs (Clinical Treatment Centres - CTC). |
Baadhi ya watu waishio na VVU/UKIMWI hawana na/au wanahitaji elimu na stadi zaidi za ujasiriamali ili waweze kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na hivyo kujiletea kipato cha kuwawezesha kujikimu. |
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu waishio na VVU/UKIMWI mara nyingine hushindwa kuwafikia na kuwahudumia walengwa (wagonjwa) kwa wakati kutokana na kukosa nyenzo za usafiri kama vile; baiskeli n.k. |
Maelezo |
---|
THE LOCAL COMMUNITIES WHEN TRAINED CAN WORK FOR THE PERFORMANCE OF THE ORGANIZATION. |
Maelezo |
---|
During the conduction of this training, the participants learnt on: • Every person or organization had the right to advocate for any threatening issue • We need to gather the right information to the audience • People have different views, insights and opinions and therefore different strategies should be applied during advocacy work |
Maelezo |
---|
No organisation can survive and work in isolation. Therefore, there is a need for CODECOZ to extend its operation through coalition and network with other like minded CSOs both within and outside Tanzania. |
Not all CODECOZ members have same knowledge and information about the organisation. During project implementation especially Organisation Self Assessment some members have showed that they were not very conversant with the activities of the organisation. Therefore, there is a need for streamlining the flow of information from top to bottom. CODECOZ members have to be more proactive towards organisation. |
The importance of involving stakholders in planning process. Community leaders and other stakeholders made tremendous contributions during CODECOZ SP development process. |
« Rudi nyuma kwenye ripoti