Envaya

Foundation for Civil Society

FCS Narrative Report

Respondent: Patronage in Environmental Management and Health Care Warriors
Time Submitted: 20 Gicurasi, 2011 at 17:16 EAT

Introduction

Patronage in Environmental Management and Health Care Warriors
PEMWA
Kupunguza kasi ya Unyanyapaa kwa Watu Waishio na VVU/UKIMWI Wilaya ya Lindi
FCS/MG/3/08/094
Dates: Januari 01, 2011 - Machi 31, 2011Quarter(s): Robo ya Nne
Melania Felix
S.L.P. 552,
LINDI
Simu: Mezani; +255 23 220 2645, Kiganjani; +255 787 766660; +255 754 766660

Project Description

Policy Engagement
Mradi umelenga kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na UKIMWI ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuchangia shughuli za maendeleo. Mradi umeboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Pia jamii imeelimishwa na kuhamasishwa vya kutosha kuhusu athari za unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Vilevile mradi umesaidia kuwezesha Serikali za vijiji, watendaji wa serikali za mitaa na jamii kiujumla kutambua na kuzingatia mahitaji ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI katika uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika maeneo yao.

Mradi umetekeleza shughuli mbalimbali katika kufanikisha malengo yake ikiwa ni pamoja na:-

1. Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wapatao 64 toka kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini wamepatiwa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu namna ya kuhudumia wagonjwa na waishio na VVU/UKIMWI..

2. Watu waishio na VVU/UKIMWI wapatao 40 toka kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini wamejengewa uwezo kuhusu uelimishaji na uhamasishaji jamii kupiga vita unyanyapaa kwa watu waishio na VVU/UKIMWI.

3. Kufanyika kwa mikutano 8 katika kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini ya uelimishaji na uhamasishaji jamii juu ya umuhimu wa utoaji huduma kwa wagonjwa na kupiga vita unyanyapaa kwa watu waishio na VUU/UKIMWI.

4. Mdahalo wa wadau 60 wa maendeleo na wanaojishughulisha na vita dhidi ya VVU/UKIMWI na unyanyapaa umefanyika na kushirikisha wadau toka kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini.

5. Wadau 20 wameshirikishwa katika ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi

6. Wadau 34 wa kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini wameshiriki tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiManispaa LindiWailes, Matopeni, Msinjahili na Nachingwea.160
Lindi VijijiniRutamba, Mtama, Nyengedi na Mingoyo.238
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female278382
Male120198
Total398580

Project Outputs and Activities

1. Watoa huduma 64 wa ngazi ya jamii wa kata za wilaya ya Lindi wanatoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani na watu waishio na VVU/UKIMWI.

2. Uelewa wa jamii kuhusu unyanyapaa na uwezo wa utunzaji wa watu waishio na VVU/UKIMWI umeongezeka.

3. Jamii ya kata 8 za; Rutamba, Nyengedi, Wailes, Msinjahili, Matopeni, Nachingwea, Mtama na Mingoyo zimewezeshwa kuandaa mkakati wa utoaji huduma kwa watu waishio na VVU/UKIMWI.

4. Uelewa wa wadau na jamii kuhusu athari za unyanyapaa kwa watu waishio na VVU/UKIMWI katika Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini umeongezeka.

5. Mafanikio, mapungufu na changamoto za utekelezaji wa mradi vimebainika kuwekewa mikakati na kuboreka.
1. Kuendesha mdahalo wa wadau 60 wanaojishughulisha na vita dhidi ya VVU/UKIMWI na kujadili juu ya unyanyapaa kwa waishio na VVU/UKIMWI toka Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini.

2. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji mradi katika kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini.

3. Kufanya tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi.
1. Wadau 60 wanaojishughulisha na vita dhidi ya VVU/UKIMWI toka Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini wameshiriki mdahalo.

2. Kata 8 za mradi zilizopo Manispaa Lindi na Lindi vijijini zimefuatiliwa na kubainika kwa mafanikio, mapungufu na changamoto za utekelezaji wa mradi.

3. Wadau 34 wa maendeleo na mradi wameshiriki tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi na kuandaliwa kwa mpango wa siku za baadae wa kuendeleza mafanikio ya mradi.

Hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza katika utekelezaji wa shughuli za mradi.
1. Kuendesha mdahalo wa wadau kuhusu unyanyapaa (TZS. 3,075,500/=)

2. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi (TZS. 629,500/=)

3. Kufanya tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi (TZS. 1,262,500/=)

4. Gharama za utawala na uendeshaji wa mradi (TZS 990,000/=)

Project Outcomes and Impact

1. Watoa huduma 64 wa ngazi ya jamii wa kata za wilaya ya Lindi wanatoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani na watu waishio na VVU/UKIMWI.

2. Uelewa wa jamii kuhusu unyanyapaa na uwezo wa utunzaji wa watu waishio na VVU/UKIMWI umeongezeka.

3. Jamii ya kata 8 za; Rutamba, Nyengedi, Wailes, Msinjahili, Matopeni, Nachingwea, Mtama na Mingoyo zimewezeshwa kuandaa mkakati wa utoaji kwa watu waishio na VVU/UKIMWI.

4. Uelewa wa wadau na jamii kuhusu athari za unyanyapaa kwa watu waishio na VVU/UKIMWI katika Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini umeongezeka.

5. Mafanikio, mapungufu na changamoto za utekelezaji wa mradi vimebainika kuwekewa mikakati na kuboreka.
1. Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wanaojitokeza katika vituo vya kutolea huduma za matibabu toka 130 (2009) hadi 360 (2011).

2. Kuongezeka na kutumika kwa watu waishio na VVU/UKIMWI katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kujitokeza kupima VVU/UKIMWI, kutoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani na kupiga vita unyanyapaa kwa waishio na VVU/UKIMWI..

3. Kupungua kwa kujinyanyapaa wenyewe miongoni mwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na jamii kiujumla.

4. Watu waishio na VVU/UKIMWI wapatao 10 wamewezeshwa kuwa watoa ushauri nasaha katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini.
1. Kuimarika kwa ushirikiano baina ya viongozi wa serikali za mitaa ngazi ya vijiji na kata na watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo wanaoishi na VVU/UKIMWI.

2. Kuimarika kwa ushirikiano baina ya Serikali na Asasi za Kiraia katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii.
Hakuna tofauti ya mabadiliko ya mradi.

Lessons Learned

Explanation
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI bado wanahitaji kujengewa uwezo zaidi kwa maarifa na stadi ili waweze kuboresha utoaji wa huduma na kuleta ufanisi.
Watoa huduma kwa wagomjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo wanaoishi na VVU/UKIMWI wanahitaji motisha ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Baadhi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI (ARVs) hulazimika kusafiri umbali mrefu kufikia kilomita zaidi ya 30 ili kufika katika vituo vya kutolea / kupokelea ARVs (Clinical Treatment Centres - CTC).
Baadhi ya watu waishio na VVU/UKIMWI hawana na/au wanahitaji elimu na stadi zaidi za ujasiriamali ili waweze kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na hivyo kujiletea kipato cha kuwawezesha kujikimu.
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu waishio na VVU/UKIMWI mara nyingine hushindwa kuwafikia na kuwahudumia walengwa (wagonjwa) kwa wakati kutokana na kukosa nyenzo za usafiri kama vile; baiskeli n.k.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI kufanya kazi kwa kujitolea kwa muda mrefu hali inayowakatisha tamaa.Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wanahamasishwa kuendelea kujituma na kujitolea kwa manufaa ya jamii.
Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI kukosa nyenzo za usafiri ili kuwawezesha kuwatembelea na kutoa huduma kwa wakati na mara kwa mara.Watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo wanaoishi na VVU/UKIMWI wanahamasishwa kuendelea kujituma na kujitolea kwa manufaa ya jamii. Pia ushawishi unaendelea kufanyika kwa Serikali za Mitaa ili kusaidia upatikanaji wa nyenzo za usafiri kwa watoa huduma kama vile; Baiskeli.
Jamii kuwa na mtazamo hasi kwa watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo wanaoishi na VVU/UKIMWI kwamba wanafaidika huku wakijitolea kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma na kupunguza unyanyapaa kwa watu waishio na VVU/UKIMWI.Jamii inaelimishwa na kuhamasishwa kutoa ushirikiano kwa watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuongeza ubora na ufanisi wa utoaji huduma zao.
Baadhi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI kuendelea kujinyanyapaa wenyewe kama vile; kutopenda kujulikana kwamba wanatumia ARVs, kujitenga katika masuala tofauti ya kijamii n.k.Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wanaelimishwa na kuhamasishwa kutojinyanyapaa ili waweze kupata na kutumia huduma muhimu za kuimarisha lishe na afya zao.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Idara ya Afya - Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.Kutoa wataalamu wa afya na baadhi ya taarifa na takwimu muhimu zilizohitajika.
Idara ya Afya - Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.Kutoa wataalamu wa afya na baadhi ya taarifa na takwimu muhimu zilizohitajika.
Viongozi wa Serikali za mitaa (kata, mitaa na vijiji)Kuwatambua watoa huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani wakiwamo watu waishio na VVU/UKIMWI na walengwa wa mradi.
Asasi za Kiraia (AZAKi) na Waandishi wa HabariKushiriki mdahalo na tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi na kuhabarisha umma kuhusu taarifa za mradi.
Viongozi wa diniKushiriki mdahalo na tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi na kuelimisha waumini wao kuhusu athari za VVU/UKIMWI katika maendeleo na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Hakuna shughulin zilizopangwa kutekelezwa baadae kwa kuwa mradi umefikia mwisho (robo nne zote zimeshatekelezwa)

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale4652
Male2025
Total6677
People living with HIV/AIDSFemale3647
Male1423
Total5070
ElderlyFemale4849
Male1728
Total6577
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale1933
Male515
Total2448
YouthFemale3479
Male2037
Total54116
OtherFemale95122
Male4470
Total139192
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya usimamizi wa ruzukuAprili 2009Mbinu na stadi za kusimamia utekelezaji wa mradi kwa ufanisi.Kusimamia utekelezaji wa mradi kwa ufanisi.
Mafunzo ya usimamizi wa fedha2010Mbinu na stadi za kusimamia fedha za mradi kiufanisi. Fedha za ruzuku ya mradi zimesimamiwa kiufanisi.
Tamasha la Asasi za KiraiaMei, 2010Kubadilishana uzoefu, habari na taarifa mbalimbali kuhusu sekta ya AZAKiWadau mbalimbali wa AZAKi wa maeneo tofauti ya Lindi wamefikiwa na taarifa mbalimbali kuhusu AZAKi.

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report