Baada ya kuwa kwa muda mrefu shughuli za asasi zilisimama,
sasa asasi imeanza tena shughuli zake. Wanachama wamekutana
na kuazimia mambo kadhaa ya kuingia kwenye mpango wa mwaka
2016.
Asasi ya EPA-Ukimwi inakusudia kuanzisha vipindi vya utoaji elimu juu ya kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi waweze kujizalishia mali kwa kutumia raslimali zinazopatikana ndani ya maeneo yao. Mafunzo haya yatakayohusisha washiriki 30 wa kata za Namajani na Mbonde-mtapika yataendeshwa na wawezeshaji ambao watatoka kwenye idara ya maendeleo ya jamii. Matarajio ni kuwa watakaopata mafunzo hayo wataondokana na hali ya utegemezi na kuweza kujikimu wao wenyewe na familia zao. Muda kamili bado haujaoangwa ila itakuwa kabla ya kipindi cha kilimo ili kuwawezesha washiriki kutoingilia ratiba zao za shughuli za kilimo.
Jumla ya wanavikundi 20 wanaotoa huduma za wagonjwa majumbani
HBC attendants, wamepatiwa mafunzo ya rejea ya huduma zao
ili kuboresha stadi zao. Hii inafuatia mafunzo ya msingi waliyopatiwa
mnamo mwaka 2006. Ni matarajio ya asasi kuwa utendaji wao utaboreka
na kuleta manufaa kwa jamii wanazozihudumia.
Aasi yetu ya Epa ukimwi kwa kipindi cha June hadi July itakuwa inaendesha mafunzo ya awereness kwa makungwi na mangariba na manyakanga wa kata za Sululu, Mbonde na Namajani. Hiii ni kutokana na hitaji hilo katika kipindi hiki ambapo shughuli za unyago na jando ndiyo msimu wake. Jumla ya washiriki 33 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo na nyenzo za kuwasaidia.