Envaya

Nuru Halisi Development Group sasa wameanza kupewa mafunza ya kutengeneza Uyoga na tayari wameanza kwa vitendo kwa kushiriki wenyewe kuandaa vitendea kazi. Wanachama watakuwa wakifanya kazi kwa pamoja ili wapate elimu hii ili iweze kuwasaidia mmoja mmoja kujibunia miradi yake nje ya kikundi. Malengo ya kikundi hiki ni kuwawezesha wanachama kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa kutumia rasilimali walizonazo bila kutegemea kusaidiwa. Wanachama wamejiwekea akiba wenyewe na sasa wameweza kuanzisha mradi huu. Hii ni sehemu tu ya mikakati ya NURU HALISI

18 Mei, 2010
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.