Envaya

Nuru Halisi

Historia

Nuru Halisi ilianza kama kikundi ambacho kilikua kikitoa elimu kwa jamii mwaka 2008 katika Manispaa ya Dodoma. Baada ya kuona jamii inapokea elimu wanayopewa na kukubali kazi yetu, tuliona ni vyema kupata usajili ili tutambulike zaidi na kuweza kuifikia jamii nchi nzima na tulianza kufuata taratibu za usajili na hatimaye January 2009 tukapata usajili rasmi. Tulianza kazi kwa kujitangaza na kutanuka kwa kadri tulivyoweza na hadi sasa tumeishaifikia mikoa minne Tanzania Bara, Dar es salaam, Dodoma,Morogoro na Manyara. Tumeweza kupata mradi wa utunzaji wa mazingira na ukusanyaji wa taka ngumu katika mtaa wa Markazi kata ya Ukonga na vilevile tumeweza kuanzisha kikundi cha maendeleo cha Nuru Halisi(NURU DEVELOPMENT GROUP). Wana kikundi walihamasishwa na kufundishwa namna ya kujikwamua katika dimbwi la umaskini kwa kutumia rasilimali walizo nazo na kinatarajia kuanza miradi yake mwezi July mwaka huu.

Tumeweza kuongeza idadi ya wanachama na sasa tuna wanachama wengi. Nuru Halisi imefanikiwa kupata tuzo ya kwanza ya Mazingira ya mwaka 2009-2010. Tuzo iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh William Lukuvi.