NGOME imefungua tawi jingine la klabu ya wanafunzi kama zilivyo klabu zingine za NGOME katika shule za sekondari ya Mikindani na Mitengo. Klabu hiyo ya NGOME imefunguliwa katika shule ya sekondari NDUMBWE Mtwara vijijini. Klabu hizi ni kwaajili ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Stadi za Maisha kwa wanafunzi wa sekondari, ambao hufundishwa na wataalam wa Afya kutoka NGOME na kufundishana wao kwa wao{UELIMISHAJI RIKA} baada ya kupata mafunzo kutoka kwa wataalam.
Elimu ya Ukimwi na Jinsia katika shule za Sekondari, hapa mtaalam wa Afya akitoa Elimu hiyo kwa wanafunzi wa sekondari ya Mitengo Mtwara Mjini
Maelezo ya kina ya shirika la Huduma ya Afya ya jamii Mtwara(NGOME) yamewekwa katika tovuti hii pamoja na Ripoti ya mwaka 2010.MAELEZO_YA_ASASI_-_ORGANIZATION_PROFILE.doc
NGOME inafanya Utafiti wa Matatizo yanayofanya kuwe na Ndoa zinazovunjika mara kwa mara katika kata za Ufukoni na Mpapura ili kupanga mbinu mbadala ya kutatua tatizo hili linalopelekea maambukizi ya UKIMWI kuzidi kuenea kwa kasi kubwa pamoja na watoto wa Mitaani.
TUMEPATA ELIMU YA KUJIUNGA NA TOVUTI YA ENVAYA LEO TAREHE 18/05/2011 MAFUNZO MAZURI TUMEFURAHI KUYAPATA TUNAWASHUKURU WALIOTUWEZESHA KWANI WAMETUPATIA KITU KIPYA AMBACHO HATUJAKITEGEMEA TUNAWASHUKURU SANA.