Log in
Environment Media Network(EMNet)

Environment Media Network(EMNet)

Kinondoni, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

large.jpg

Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Arusha,wakiwa katika moja ya mafunzo kwa waandishi wa habari za mazingira.mafunzo hayo yaliandaliwa na EMNet kwa ufadhiri wa WWF-TCO.

large.jpg

Pichani ni Waandishi wa Habari za Mazingira mkoani Arusha,wakiwa katika moja ya mafunzo yaliyotolewa na mtandao wa wanahabari wa mazingira (EMNet)kwa waandishi wa Habari za Mazingira mkoani Arusha hivi karibuni.

EMNet Yatoa mafunzo kwa Waandishi wa habari za Mazingira.

Mtandao wa wanahabari wa mazingira EMNet,hivi karibuni umetoa mafunzo kwa baadhi ya waandishi wa habari za mazingira hapa nchini.

Mafunzo hayo yaliratibiwa na Mtandao huo wa wanahabari (Environment Media Network)chini ya ufadhiri wa WWF kupitia programu yake ya CSOP.Program hii ya CSOP hivi sasa imeshamaliza muda wake.Mafunzo hayo yaliwapa fulsa waandishi wa habari za mazingira katika mikoa ya Dar es salaam na Arusha.

Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo hayo mkoani Dar es salam ni kutoka katika vyombo vya Tanzania Daima,Nipashe,Guardian,Habari Leo,Mwananchi,TBC Taifa,TBC 1,Star TV,Radio Free Africa,Mlimani Radio,Mlimani TV,Majira,Uhuru FM,Passion FM na Radio One.

Mkoani Arusha waandishi wa habari walitoka katika vyombo vya Tanzania Daima, Nipashe, Guardian,Habari Leo,Mwananchi,TBC Taifa,TBC 1,Star TV,Radio Free Africa,Radio 5,Jambo leo,Majira,Business Times,Radio One na Boma Radio FM.

Katika mafunzo hayo waandishi hao walipata fulsa ya kufahamu na kuzielewa vizuri sera katika sekta tatu,sekta hizo ni UVUVI,MISITU na WANYAMAPOLI.

 

 Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wakielekezwa kitu na Meneja Misitu ya PUGU na KAZIMZUMBWI bwana Methew Mwanuo,katika moja ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na EMNet Mkoani Dar es salaam.

 

 

 

Mtandao wa wanahabari wa Mazingira unaojulikana kwa jina la Environment Media Network-EMNet,unashiriki katika utekelezaji wa mradi wa Hifadhi Mapafu ya Dar es salaam(HIMADA).

Mradi huu unaratibiwa na  chama cha Uhifadhi Maliasili Tanzania kwa lugha ya kigeni chama hiko kinajulikana kwa jina la Wildlife Conservation society of Tanzania (WCST) Chini ya ufadhiri wa ubalozi wa Norway hapa nchini.

Pamoja na mradi huu wa HIMADA kuratibiwa na WCST pia katika utekelezaji wa mradi huu wapo wadau wengine wanaoshiriki katika utekelezaji wa uhifadhi wa misitu hiii ya Pugu na Kazimzumbwi.

wadau hao wengine ni pamoja na idara ya misitu na nyuki (FBD),Environment Media Network(EMNet),LEAT,SUA na UDBS.

Katika utekelezaji wa mradi huo kila mdau anayoshughuri inayomfanya ashiriki katika utekelezaji wa uhifadhi wa misitu hii ya Pugu na Kazimzumbwi.

Mtandao wa wanahabari wa Mazingira,unajulikana kwa jina la Environment Media Network-EMNet,katika mradi huu wa HIMADA unatekeleza tokeo la nne ambalo linahusiana na mambo ya Advocacy, Education,Awareness and Knowledge management.

Mradi huu a HIMADA ni wa miaka minne ambao umeanza mwaka 2011 na unatarajiwa kumalizikaa mwaka 2014. 

 

Pichani ni moja ya mkutano uliyofanywa na mtandao wa wanahabari wa mazingira(EMNet)katika kata ya Pugu wilayani ilala mkoani Dar es salaam,katika utekelezaji wa tokeo lao la nne katika Mradi wa Hifadhi Mapafu ya Dar es salaam-HIMADA.

large.jpg

MS Secelela Balisidya Board Chairperson of EMNet explains something during the meeting with Environment Jouranalists

large.jpg

MEO's listen tentatively during the meeting with stakeholders during the meeting on illigal fishing

large.jpg

Samwel Ntapanta EMNet Coordinator explains something during the meeting

large.jpg

Meeting with fishery stakeholders at Somangira,kigamboni