Log in
Environment Media Network(EMNet)

Environment Media Network(EMNet)

Kinondoni, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

EMNet Yatoa mafunzo kwa Waandishi wa habari za Mazingira.

Mtandao wa wanahabari wa mazingira EMNet,hivi karibuni umetoa mafunzo kwa baadhi ya waandishi wa habari za mazingira hapa nchini.

Mafunzo hayo yaliratibiwa na Mtandao huo wa wanahabari (Environment Media Network)chini ya ufadhiri wa WWF kupitia programu yake ya CSOP.Program hii ya CSOP hivi sasa imeshamaliza muda wake.Mafunzo hayo yaliwapa fulsa waandishi wa habari za mazingira katika mikoa ya Dar es salaam na Arusha.

Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo hayo mkoani Dar es salam ni kutoka katika vyombo vya Tanzania Daima,Nipashe,Guardian,Habari Leo,Mwananchi,TBC Taifa,TBC 1,Star TV,Radio Free Africa,Mlimani Radio,Mlimani TV,Majira,Uhuru FM,Passion FM na Radio One.

Mkoani Arusha waandishi wa habari walitoka katika vyombo vya Tanzania Daima, Nipashe, Guardian,Habari Leo,Mwananchi,TBC Taifa,TBC 1,Star TV,Radio Free Africa,Radio 5,Jambo leo,Majira,Business Times,Radio One na Boma Radio FM.

Katika mafunzo hayo waandishi hao walipata fulsa ya kufahamu na kuzielewa vizuri sera katika sekta tatu,sekta hizo ni UVUVI,MISITU na WANYAMAPOLI.

 

 Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wakielekezwa kitu na Meneja Misitu ya PUGU na KAZIMZUMBWI bwana Methew Mwanuo,katika moja ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na EMNet Mkoani Dar es salaam.

 

 

 

June 6, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.