Fungua
DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION

DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION

WAMI DAKAWA, Tanzania

DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION.Inakaribisha wabia wa maendeleo kwa jamii katika kufanya nao kazi ili kufikia lengo la kuanzishwa kwa asasi.Miongoni mwa shughuli ambazo asasi inafanya ni;

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA HIFADHI YA MAZINGIRA KATIKA MILIMA YA ULUGURU.

DAKEDEO Kwa ushirikiano na shirika Rafiki la MUUNGANO MAZINGIRA ORGANIZATION.Linachukua fursa ya kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika matarajio yasiyo na mashaka,maisha yasiyo na woga wa kushambuliwa na matatizo na majanga yasababishwayo na uharibifu wa mazingira.

Kwa ushirika huo wa mtazamo wa kimaendeleo DAKEDEO Imehakikisha kuwa wataalamu wake wa sekta ya mazingira wanafanya kila jitihada za kuhakikisha kuwa jamii ya watu wanaoishi katika vyanzo vikuu vya maji na uoto asilia ambao haujavamiwa unawekwa katika ulinzina mpango mkakati wa kuuendeleza.

MUUNGANO MAZINGIRA ORGANIZATION Iliendesha mradi wa mafunzo wa "KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA NA JAMII MBINU BORA ZA KILIMO MITI" Katika milima ya Uluguru.Mradi huo umefadhiliwa na KAMPUNI YA SIGARA TANZA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 MAFUNZO YA AWALI KIDATO CHA KWANZA YASHIKA KASI.

Kituo cha elimu ya kujitegemea na mafunzo ya ujuzi kwa jamii (DAKAWA CENTRE FOR SELF RELIANCE AND SKILL DEVELOPMENT-DCSSD)KINAENDELEA NA MAFUNZO YA AWALI KWA KIDATO CHA KWANZA. ambayo yalianza mwezi november 2013.

Katika kuhakikisha kuwa kituo kinawajenga vema wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014 kituo kimeandaa Safari ya Mafunzo katika Hifadhi za Taifa za UDZUNGWA zilizopo katika wilaya ya Kilombero ziara itakayofanyika katika kipindi cha mwezi wa Disemba.

Ziara hiyo ya mafunzo inakusudia pia kuonesha jinsi asasi ya Uchumi na maendeleo Dakawa.(DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION(DAKEDEO)ambayo ndio inayosimamia kituo cha (DSSDC) katika ushiriki wake wa kukuza utalii wa ndani kwa jamii ambao kwa kiasi kikumbwa haujaeleweka vema kwa jamii.

Asasi inakaribisha wadau ambao ni wakereketwa wa maendeleo ya elimu katika jamii kushiriki katika kufanikisha ziara hiyo ya mafunzo.

 MRADI WA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

DAKEDEO itaanzisha  mradi wa hifadhi ya mazingira katika maeneo ya vijiji vilivyopo wilaya ya Mvomero katika kipindi cha mvua za masika 2014.

Mradi huo wenye mfumo shirikishi jamii katika hifadhi za mazingira unahusisha kuanzishwa kwa vitalu maalum vya miche ya miti ambapo aina ya miche kumi na mbili itahusishwa katika uzalishaji wake katika vitalu.

Miche hiyo itazalishwa  na DAKEDEO Ikishirikiana na asasi rafiki (CBO)'

Baada ya kuzalishwa kwa miche hiyo kutakuwepo na utaratibu wa kuipanda katika mashamba yanayomilikiwa na watu binafsi pamoja na asasi za kijamii ambapo wamiliki watahusika na utunzaji wake.

Mradi hhuo utahusisha njia bora za kitaalamu zenye gharama nafuu za kiuendeshaji katika miiradi ya uzalishaji mali lakini yenye tija kubwa katika kipato.

DAKEDEO Itasimamia mpango huo katika shughuli zifuatazo.

(i)Kutoa elimu /kuwajengea uwezo wanajamii mbinu za uhifadhi wa mazingira kwa mfumo wa kilimo miti.

(ii)Kuotesha miche pamoja na kusambaza kwa wadau washiiiriki katika mradi.

(iii)Kutoa huduma za kitaalamu katika kuhudumia mashamba hayo.

(iv)Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya mradi.

(v)Kutafuta wdau na wafadhili wa miradi ya uhifadhi wa mazingira ili washirikiane na wadau wanajamii katika uhifadhi.

DAKEDEO inakaribisha wadau mbali mbalimbali katika kushiriki katika mpango wa uhifadhi wa mazingira.