Injira
Africa Upendo Group

Africa Upendo Group

Shighatini,Mwanga,Kilimanjaro, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MATUNDA YA KUHUDHURIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KIVITENDO NA KUTHUBUTU KUYAFANYIA KAZI MAFUNZO NA KUKUBALI KUELEKEZWA NA KUSIMAMIWA IPASAVYO

Katika eneo la Tegeta kuelekea Twiga cement karibu na kanisa la KKKT kuna mfugaji mzuri wa samaki Ndugu KIbona ambaye hivi majuzi amevuna mazao yake ya kwanza katika Bwawa lake ambalo ukiliona utapenda kufuga samaki.Katika kufanya zoezi la Monitoring and evalution tuliamua kwenda kumtembelea Ndugu huyu kama kawaida ya shirika letu la Africa Upendo Group na kwa pamoja tulikutanika pamoja na wataalamu wetu mbalimbali kama Consaltant wetu kutoka Open Mind Tanzania ndugu Dominic Nduguru,Mwalimu KIssai na Mwalimu Lishela kutoka Mbegani fisheries Development Centre,Ndugu Neatness Msemo Mwenyekiti Mtendaji wa AUG,Dr.Ramadhani Shaban Katibu Mkuu wa AUG,Goodchance Sangiwa Mkurugenzi wa Fedha na mipango wa AUG na Dada Ruth Rinden Mhasibu Mkuu wa AUG.Hawa kwa pamoja,wakiambatana na  wajumbe wengine walikuwa faraja sana kwa Ndugu KIbona na Kwa utaalamu mkubwa aliweza kuvuna samaki katika Bwawa lake ambalo kwa kweli inaonekana ameiva kwelikweli baada ya kupata semina iliyoendeshwa mwaka mmoja uliopita na shirika lisilo la kiserikali la Africa Upendo Group(AUG).Ndugu KIbona ni mmoja wa wanafunzi ambayo walipata semina na mafunzo kivitendo na wapo wanasemina wengi mfano dada Rachel Mapande na wengine ambao ni miongoni mwa wanasemina ambao waliyatendea kazi mafunzo.Dada Rachel yeye alishavuna miezi kadhaa iliyopita na hivi sasa ana mikakati ya kujenga Bwawa kubwa lingine ili anapovuna hawa apate mbegu ya kuwafuga katika bwawa jipya badala ya kwenda tena KInguruwira au kunduchi au Mbegani .Ameona ni vema aanze kuzalisha mbegu kwa wingi hata kuwauzia watu wengine watakaohitaji.Kaka Kibona na yeye ana mpango wa kujenga mabwawa mengi zaidi pale tegeta pamoja na eneo lake kubwa huko Madale kwani ameona faida kubwa.Samaki ni rahisi sana kufugwa kwani hawahitaji chakula kingi na hawana magonjwa wanachohitaji zaidi ni chakula kidogo tu na hewa zaidi.Karibu katika

UFUGAJI WA SAMAKI KWA LISHE BORA NA KIPATO ZAIDI.

15 Mata, 2011
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.