Log in
Africa Upendo Group

Africa Upendo Group

Dar es salaam, Tanzania

Africa Upendo Group (AUG) is a private, voluntary non governmental, non partisan, non religious and non-profit making organization established and registered in the Ministry for Gender, Women and Children with registration number OONGO/1932.
Before its registration as an independent autonomous entity in January, 2007 Africa Upendo Group was working in association with other NGOs of the related objective from 2005 in uplifting the social and economic lives of the drug addicts, street children Andrew 8 HIV/AIDS orphans through its Facility and Home Based care Approaches.
This time AUG has a lot of objectives to implement as we are trying to cope up with the Globalization challenges of the contemporary societies. It’s our dream that if this
organization shall obtain greater partnership with various local and international donors, we hope to make the greater positive social change.


It’s not only due to our professionalism, but it’s due to our capacity accompanied with deep knowledge of working with the socially excluded members of the society.Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Africa Upendo Group akifungua semina ya wajasiriamali wafungaji/wanaotarajia kufuga Samaki Ndugu Neatness Msemo. Kulia kwake yupo pamoja na Mkurugenzi wa Ufugaji Samaki kutoka Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya MIfugo Tanzania Dr.Mahika pamoja na Mkurugenzi Mstaafu wa ukaguzi wa fedha kutoka TASAF  Dr.Masenga

Hapa mmoja wa waalimu kutoka Africa Upendo Group ndugu Erick Mshana ambaye sasa ni marehemu akitoa mada ya jinsi ya kujenga Bwawa la kisasa kwa wana semina.

Dr.Mahika akiwafundisha wana semina juu ya kufanikiwa Katika kufuga samaki.Kama Mkurugenzi anao udhoefu mkubwa sana katika eneo hili na ukimsikiliza utapenda tu aendelee wakati wote kwani anajua mbinu na kwa utaalamu alionao,Hakika kufanikiwa ni lazima.Hapa anatoa mikakati ya jinsi ya kutengeneza chakula cha samaki pia jinsi ya kufuga kibiashara na lishe bora ya mazao ya samaki isiyo na chemikali ambayo sisi kama Wanajamii tunapaswa kuzizingatia mbinu hizi kabla ya kuamua kufuga samaki. Hapa kama kioo kwa jamii anatuongoza katika kufanikisha sera ya  KIlimo kwanza na ufugaji wa kisasa wa samaki kama chakula na lishe pia kikiwa ni kipato cha uhakika cha kusaidia sana kuondoa umaskini.

Wanasemia wakimsikiliza mkufunzi kwa makini Bwana Kissai ambaye ni mtaalamu wa ufugaji wa samaki kutoka katika chuo cha uvuvi cha Mbegani aliyebobea na hivi karibuni alikuwa kule nchini Korea na ukikutana naye utapenda kujua zaidi kwani anaeleza jinsi wenzetu wa kule Korea walivyoendelea na walivyofanikiwa sana kwa kutumia kilimo hiki cha kufuga Samaki kama mboga na kipato.Usikose kuhudhuria semina mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika hili .

 Asasi yetu imeelekeza nguvu zake mikoani.Katika wilaya ya Kigoma na wilaya ya Mwanga.Katika wilaya ya Mwanga asasi kuanzia mwaka 2014 imeelekeza nguvu zake katika kutunza mazingira na kutoa elimu ya ujasiriamali na kuanzisha vikundi mbalimbali vya maendeleo.Asasi inafanya majaribio yake kwa kujikita katika Kata ya Shighatini.Kata ya Shighatini Ina vijiji sita yaani Shighatini,Ibaya,Mfinga,Lambo,Mkuu na Ndambwe.katika kuanzisha miradi mbalimbali wamekuwa zaidi wakishirikisha wanafunzi wa shule ya msingi ili kuwajengea uwezo wa kutunza mazingira katika umri mdogo pia vijana wamepewa elimu ya kutengeneza mizinga ya nyuki na upandaji miti ya asili ili kutunza na kulinda mazingira,asasi kwa kushirikiana na wananchi wameanza kurudisha misitu ya asili(MBUNGI)ili kutunza vyanzo vya maji na utalii.