Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Ulimwenguni huadhimishwa tarehe 26 Juni ya kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuungana na mataifa mengine duniani yaliyo kwenye harakati za kupambana na matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo mwaka huu 2014 inabebwa na kauli mbiu isemayo “Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua”.
Mkurugenzi wa shirika la VIYOSO Bwn Freddy Ng'atigwa katikati akiwa na baadhi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya mkoani Morogoro ambao waneamua kuachana na uteja.
Vijana wanaotumia matawa ya kulevya wanaopatiwa huduma ya kuacha kutoka shirika la VIYOSO wakiwa katika mahojianao na waandishi wa habari Ndg Tindwa na msilo
Mtumiaji wa Dawa za kulevya Bw. John akiwa kwenye pozi alipokuwa akifanya mahojihano na waandishi wa habari wa VIYOSO siku ya dawa za kulevya JUNE 26 2014
Bw. Martini akitoa maelezo jinsi shirika la VIYOSO linavyomsaidia kuachana na dawa za kulevya kwenye siku ya kupunguza dawa za kulevya duniani JUNE 26 2014.
Mkurugenzi wa shirika la vijana la VIYOSO mkoani Morogoro Bw Freddy Ng'atigwa wa kwanza kushoto akiwapa ushauli vijana wanaotumia dawa za kulevya hili kuachana nazo
CHUO CHA VICTORY CHATOA VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA ICT
Victory & Faith Training Centre kimewakabidhi vyeti zaidi ya vijana 16 waliohitimu mafunzo ya compyuta ICT ngazi ya cheti.
Mkurugenzi wa Victory ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la vijana morogoro-VIYOS0 aliwaasa vijana kutumia ujuzi walioupata wa ujasiliamali na compyuta kujiajili na kutosubili kuajiliwa.
Vijana nao walikishukulu chuo cha VICTORY kwa malezi bora kwa vijana na ufundishaji wenye tija unaokwenda na technologia ya kisasa na kuwataka vijana ndani na nje ya Morogoro kujiunga na Kituo kihi cha vijana hili kujiendeleza kitaaluma.
Mkurugenzi wa Shirika la Vijana - VIYOSO Bw. Freddy Ng'atigwa akiwa na baadhi ya wanachuo wa VICTORY waliohitimu mafunzo ya ICT mara baada ya kupewa vyeti vyao Mai 3,2014
VICTORY YASHIRIKI MEI MOSI
Chuo Cha Victory & Faith Training Centre kimeshiriki katika maazimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi katika viwanja vya Jamuhuli Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa chuo cha Victory akiwa na baadhi ya wanachuo wakifuatilia kwa makini maazimisho ya siku ya Mei mosi katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro
Baadhi ya wanachuo wakifuatilia maonyesho yaliyofanyika katika siku ya wafanyakazi Mei mosi ndani ya uwanja wa Jamuhuli morogoro
CHUO CHA VICTORY & fAITH TRAINING CENTRE CHAAMASICHA UTALII WA NDANI KWA VIJANA
Chou cha Victory Kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kipo chini ya shirika la VIYOSO kimeamasisha utalii wa ndani kwa vijana kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii yaliyopo ndani ya mji wa morogoro.
Akizungumza na wanachuo Mkurugenzi Bw. Freddy Ng'atigwa Alisema wakati umefika sasa kwa vijana kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani ilikujua historia ya nchi yao hasa katika siku za mapumziko ya masomo yao.
Baadhi ya wanachuo cha VICTORY wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wao na mkurugenzi wa chuo hiko Bw. Freddy Ng'atigwa
Katika kufanikisha ziara yao ya utalii wa ndani wanachuo cha Victory hawakusita kuoga maji ya mto Morogoro
Wanachuo wa victory wakiwa na mkurugenzi wao Bw. Freddy Ng'atigwa walipofanya utalii katika milima Uluguru.
CHUO CHA VICTORY TRAINING CENTRE CHAFANYA MAONYESHO WIKI YA ELIMU
Victory & Faith Training Centre ni chuo kinachotoa mafunzo ya Vocation na Ujasiliamali kwa jamii ya vijana mkoani Morogoro yakiwemo masomo ya Secretarial, Ushonaji, Hotel Managment, Computer na Lugha.
Victory ni cvhuo kilichopo chini ya shirika la vijana la VIYOSO na kinatoa mafuzo hayo ya Vocation kwa jamii ya vijana wanaotoka katika familia duni Mkoani morogoro.
Hivi karibuni Chuo kilishiriki wiki ya elimu iliyoanzimishwa chuoni hapo ambapo pia ndio makao ya shirika la VIYOSO
Volontia kutoka chuo kikuu huria Bw.Hamisi akiongea na wanachuo wa Victory wakati wa ufunguzi wa wiki ya elimu