Log in
Victory Youth Support Organization

Victory Youth Support Organization

Morogoro Mjini, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Mwezeshaji wa semina kutoka ofisi za TRA  kitengo cha mlipa kodi Bw. Ibrahim wa kwanza kushoto waliosimama akitoa mada juu ya umuhimu wa wajasiliamali kulipa kodi bila kushulutishwa hili kuchangia pato la Taifa.

Mtoa Mada juu ya Kijana kujitambua Dr. Bagati Richson akiwasilisha mada juu ya kijana kujitambua

vijana wa manispaa wakiwa katika kikundi kazi wakijadili mambo mbalimbali juu ya ujasiliamali

Baadhi ya vijana wakiwa katika kikundi kazi wakijadili mambo mbalimbali kuhusu mafunzo ya ujasiliamali yaliyotolewa na asasi ya viyoso

Kijana Frola John akiwasilisha maoni ya kikundi kazi kuhusu fulsa za kijana katika ujasiliamali

Kijana Irene Cyprian kutoka manispaa ya morogoro akiwasilicha mchango wa maoni kutoka kwa Vijana kuhusu changamoto za ujasiliamali baada ya kazi za vikundi

Victory Youth Support Organization (VIYOSO) ni shirika la vijana lisilo la kiserikali (NGO) lisilotengeneza faida  lililopo ndani ya kata ya Uwanja wa Taifa Mainspaa ya morogoro.

Shirika linafanya miradi mbalimbali kwa vijana yenye lego la kumsaidia kijana wa kitanzania kujitambua na hatimaye kupambana na umasikini kwa njia kujiajili katika shughuli  mbalimbali za ujasiliamali.

Pia shirika la  VIYOSO  linatoa mafunzo mbalimbali kwa vijana kupitia kituo chake cha VICTORY & FAITH TRAINING CENTRE kilichopo manispaa ya Morogoro.

yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyo jitokeza kwenye utekelezaji wa program mbalimbali za shirika la VIYOSO.

vijana wanafunzi wa kozi mbalimbali kutoka katika mradi wa Victory & faith unaoendeshwa na Shirika la viyoso- Morogoro

 

mkurugenzi wa Shirika la VIYOSO Bwn Freddy Ngatigwa akiwa na mavolontia Jannis na jan kutoka chuo kikuu cha Dusseldorf Nchini ujerumani walipo tembelea mradi wa ICT wa victory & faith morogoro

baadhi ya vijana wakipatiwa mafunzo ya ushonaji kwa lengo la kujiajili kwenye ujasiliamali kutoka katika mradi wa Victory & Faith unaoendeshwa na shirika la VIYOSO