Log in
Victory Youth Support Organization

Victory Youth Support Organization

Morogoro Mjini, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations
RIPOTI ya umoja wa mataifa ni kuwa Tanzania inaongoza kwa upitishaji wa madawa ya kulevya ikifuatiwa  na Kenya  katika ukanda wa Afrika ya mashariki
Jumla ya tani sitini na nne za dawa za kulevya aina ya Heroine zilisafirishwa bila ya kukamatwa kwenda  au kupitia afrika ya mashariki ikiwamo Tanzania kati ya mwaka elfu mbili na kumi na elfu mbili na kumi na tatu

Mkoani Morogoro katika siku ya kuadhimisha upingaji wa matumizi ya madawa hayo ya kulevya imeadhimishwa pia katika shirika la vijana la VIYOSO ambapo baadhi Taasisi na watumiaji wa madawa ya kulevya wametoa sababu za kupinga matumizi hayo kuwa ni pamoja na kusababisha kufifia kwa nguvu kazi ya taifa kwani watumiaji wakubwa wa madawa hayo ni vijana.

Mkurugenzi wa kituo cha  vijana  cha VIYOSO kilichopo Morogoro Bwana Freddy Ng’atigwa ameelezea juhudi zinazofanywa na taasisi ya VIYOSO katika kuwaondoa vijana kwenye matumizi ya madawa ya kulevya katika manispaa ya Morogoro. Na kuitaka jamii Serikali na Wadau mbalimbali Tanzania kuunga mkono Juhudi hizi za shirika la VIYOSO.


Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Ulimwenguni huadhimishwa tarehe 26 Juni ya kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuungana na mataifa mengine duniani yaliyo kwenye harakati za kupambana na matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo mwaka huu 2014 inabebwa na kauli mbiu isemayo “Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua.

Mkurugenzi wa shirika la VIYOSO Bwn Freddy Ng'atigwa katikati akiwa na baadhi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya mkoani Morogoro ambao waneamua kuachana na uteja.

June 27, 2014
« Previous

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.