Unaweza kutumia Envaya kwenye simu yako kupitia njia mbili: kwa kupeleka ujumbe mfupi (SMS), au kwa kutumia kivinjari kwenye simu. Sehemu hapo chini zitaeleza jinsi ya kutumia njia hizi mbili.
Kutumia Envaya kupitia Ujumbe Mfupi (SMS)
Uwezo wa SMS wa Envaya unakuruhusu kutumia Envaya kutoka kwenye simu yoyote ya mkononi, karibu na popote duniani, hata mahali bila intaneti. Kwa sasa, uwezo huu unakuruhusu kuchapisha taarifa ya habari fupi kwenye tovuti ya shirika lako kupitia. Uwezo zaidi umepangwa kwa SMS hivi karibuni.
Ili kutumia Envaya kupitia SMS, peleka amri zifuatazo kwa namba ya SMS ya Envaya:
(Tanzania) 0763 077677
(Nchi nyingine) +1 484 544 4443
- Ili kuchapisha habari kwenye tovuti yako, peleka:
P [your message here]
kwa mfano: "P Hii ni habari zangu mpya."
- Ili kubadili lugha ya mfumo wa SMS, peleka:
L [lugha]
kwa Kiswahili: "L sw"
kwa Kiingereza: "L en"
kwa Kinyarwanda: "L rw"
- Ili kufungua akaunti yako ya Envaya, peleka:
IN [your username] [your password]
kwa mfano: "IN exampleorg secretpassword"
- Ili kuondoka akaunti yako ya Envaya, peleka:
OUT
Bei za kawaida hutumika kwa kupeleka ujumbe mfupi kwa Envaya. Namba ya SMS hapo juu ipo Merekani na inafanya kazi kutoka nchi nyingi duniani.
Kutumia Envaya kwenye Kivinjari cha Simu
Envaya inaweza kutumika kwenye simu yoyote yenye uwezo wa intaneti. Envaya inafanya kazi hata kwenye simu nyingi za zamani, na simu zenye intaneti polepole sana.
Ili kutumia Envaya kwenye simu yako, fungua kivinjari ya simu yako na na ingiza anwani envaya.org .

Kupitia simu yako, unaweza kusoma habari zilizochapishwa na mashirika juu ya Envaya, kuandika maoni, kuongeza ujumbe kwenye majadiliano, na hata kufungua na kuchapisha habari na picha kwenye tovuti yako.
Kubadilisha kati ya Simu na Kawaida
Kwa kawaida, Envaya inaonyesha toleo la Simu kama unatumia simu ya mkononi. Hata hivyo, wakati mwingine unaweza kubadili kati ya matoleo ya kawaida na simu ya Envaya.
Ili kubadili matoleo, tembeza ("scroll") kwa chini ya ukurasa na kubonyeza Standard au Simu, kama hapo chini:


Kwa mfano, kama unatumia kivinjari kwenye kompyuta yenye intaneti polepole sana, unaweza kubadili kwa toleo la Simu ili kutumia Envaya kwa kasi zaidi.
Au, kama unatumia "smartphone" yenye kivinjari kipya, unaweza kubadili kwa toleo la Kawaida ili kutumia uwezo ambao haupatikani katika toleo la Simu.