Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Respondent: Promotion of Education Link Organisation (PELO)
Time Submitted: 30 Januari, 2012 20:44 EAT
Msimbazi bondeni
Inahitajika nguvu ya pamoja kushinikiza serikali kumwondoa yule mfanyabiashara aliyezungusha ukuta eneo la Kigogo sambusa ili mvua za wakati mwingine,maji yake yasizuiliwe na ukuta yakarudia kuingia kwenye nyumba za watu na kusababisha mafuriko.
Duka langu lilikuwa limejaa vitu vya thamani kama ya shilingi millioni mbili.Vyote vimesombwa na maji.Achilia vyombo vyangu vya ndani.
Nilazimika kurudisha familia kijijini Moshi ili nianze kuhangaika upya.Kwa sasa natafuta chumba cha kupanga Mbagala.
Siwezi nikajua
Kabla ya mafuriko: Saa 1Sasa: Saa 1
Hii ni sehemu ya ukuta wa uzio unaolalamikiwa na wakazi wa maeneo ya Kigogo na msimbazi kuwa ulichangia kwa kiasi kikubwa kuathiriwa kwa maeneo haya na mafuriko.Angalia umbali wake kutoka kwenye mto.Ukuta huu ukiangalia utaona kama haujamalizika kujengwa isipokuwa ni mafuriko yaliyouangusha,na hiki ni kiashiria kwamba kweli ukuta huu upo kwenye njia ya maji.Uzio huu unaomilikiwa na kampuni ya Highland estates umejengwa eneo la Kigogo sambusa lililokuwa wazi kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa maelezo ya diwani wa kata ya Kigogo Mh.Chegula wakati wa kipindi cha malumbano ya hoja cha ITV mwishoni mwa mwaka jana,ni kwamba aliyekuwa Makamu wa Rais Marehemu Dr.Omary Ally Juma alikataa pasijengwe,lakini baada ya yeye kufariki pamejengwa na kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mmoja wa serikali ya mtaa wa msimbazi bondeni anasema wao kama viongoni wa mtaa hawakushirikishwa katika ujio wa kampuni hii katika eneo hili lililokuwa wazi.Swali lililopo ni kwamba je,kuwepo kwa uzio huu hapa hakujakiuka sheria za mazingira?Kama ndivyo kwa nini uendelee kuwepo?
« Jibu lililotanguliaJibu lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti