Log in
TUNAWEZA WOMEN GROUP

TUNAWEZA WOMEN GROUP

stakishari ukonga,ILALA, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

 

TUNAWEZA WOMEN GROUP (TWG) ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililosajiriwa kama ‘NGO’ kisheria. Shirika hili lilianzishwa mwaka 2008 na kikundi cha akina mama 15 wote ni wakazi wa Kata ya Kipawa. Ilipofika   mwezi Juni 2008 akina mama hawa waliamua kurasimisha shughuli za umoja huu na kuamua kujisajili kama NGO. Tarehe 22 Februari, 2009 umoja huu ulipata usajili chini ya sheria ya NGO ya mwaka 2002; hivyo TWG ilipata usajili kwa cheti nambari NGO ,002857.

MISINGI YA KUANZISHA SHIRIKA:

Lengo kuu la kuanzishwa kwa umoja huu lilitokana na hali halisi kuwa akina mama ni nguzo kuu katika familia na malezi ya watoto. Ongezeko la hali duni ya maisha ya akina mama, watoto ,na hasa wasichana liliwagusa sana akina mama na kuona umuhimu wa kuchukua majukumu ili kuisaidia jamii hasa katika changamoto zinazoyakumba makundi matatu: mama, mtoto na wasichana.

Changamoto nyingi zinayakumba makundi haya katika jamii ikiwemo kupuuzwa, kunyanyaswa, kukosa na kunyimwa haki za msingi, maradhi, ukosefu wa chakula bora na ongezeko la watoto wa mitaani.

Sisi wana Tunaweza Women Group tuliona kuwa mama ni chachu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii ya mtanzania. Kwa nini tusibebe majukumu yetu? Tuliona upo umuhimu wa kujijengea uwezo ili tuweze kupiga hatua.

MADHUMUNI YETU:

    • Kuwaunganisha wanawake kushiriki katika ujenzi wa taifa letu kwa kutumia vyema vipaji,
    • nguvu,elimu, na rasilimali zilizopo ili ziwezeshe kujiajiri na kuleta maendeleo kwa jamii nzima ya Tanzania.
    • Kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kutoa huduma kwa waathirika na waathiriwa,yatima vijana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
    • Kuimarisha haki ya usawa kwa jinsia zote na kujenga utetezi juu ya haki za akina mama.
    • Kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia, ukandamizaji, unyonyaji na ubaguzi kwa wanawake
    • Kujenga na kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na usawa katika kutoa huduma za msingi ndani ya jamii.
    • Kuondoa umaskini kwa kutoa  elimu na stadi za kazi mbali mbali na shughuli za ujasiria mali na kusimamia njia bora za kuweka na kukopa ili kujipatia mtaji.
    • Kutunza mazingira kw ajili ya afya bora.
    • MAFANIKIO:

      Kwa kipindi cha mwaka 2009 na 2011, shughuli za shirika letu zimeleta mabadiliko na mafanikio makubwa ndani ya kata ya Kipawa :

      • Kutoa misaada kwa watoto yatima wapatao 70 wengi wao wakiwa wanaishi katika mazingira magumu
      • Kutoa misaada ya chakula na mahitaji mengine kwa waathirika wa ukimwi wapatao 19
      • Kuweka walezi wa watoto yatima ili waweze kuendelea na elimu ya msingi huku wakiendelea kupata mahitaji kama vile nauli, kalamu, daftari, nguo za shule na ushauri nasaha.
      • Kutoa mafunzo ya stadi za awali za ujasiriamali kwa akina mama 86 kata ya Ukonga na kuwaunganisha akina mama 150  kuanzisha vikundi vya kiuchumi-VICOBA.
      • Tumedumisha umoja na ushirikiano ndani ya shirika ndani ya kipindi kigumu cha miaka 4 tangu 2008 bila ruzuku.
      • Tunashirikiana na wataalamu waelekezi katika kutushauri na kupata mafunzo jinsi ya kuendesha shirika letu.
      • Kuhamasisha jamii kupima virusi vya ukimwi na kutoa elimu jinsi ya kujikinga na maambukizo.
    • CHANGAMOTO:

      • Shirika halina fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo
      • Hatuna wafadhili na hatujawahi kupata mafunzo juu ya kupata ufadhili
      • Hatuna wafanyakazi wa kudumu kutokana na ukosefu wa fedha
      • Hatuna ofisi ya kudumu

      WITO WETU WADAU WA MAENDELEO.

      • Tunawaomba wadau wa maendeleo na wafadhili kulichangia fedha shirika letu ili huduma zetu ziwafikie wengi
      • Tunahitaji taarifa za wafadhili
      • Tunahitaji vifaa vya kufanyia kazi Komputa 2, simu ya ofisi, meza 3 na viti vyake, viti vya wageni 4, modemu ya internet.
      Tunahitaji kupata ufadhili wa mafunzo ili kuongezea ujuzi na umakini wa kazi zetu
    • MALENGO YA MIAKA 5 IJAYO(2012-2016):

      • Kuwa na mpango mkakati wa miaka mitano
      • Kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa akina mama kwa riba nafuu
      • Kutoa mafunzo ya ujasirimali kwa wanachama na vikundi vya akina mama
      Kuimarisha zaidi mafunzo ya ushonaji angalau kufikia wahitimu 20 kila mwaka
    • Kuimarisha mafunzo ya uelimishaji rika pamoja na michezo kwa vijana.
      • Kukuza ustawi wa jamii hasa kata ya Kipawa kwa kuwajengea uwezo akina mama na wasichana kuweza kujikimu na kujiajiri wenyewe.
      • Kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.