Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MIRADI YA SHIRIKA:

Shirika letu linayo miradi midogo midogo mitatu:

  1. Afya ya Jamii:
  • Mradi huu ni wa kuhudumia wagonjwa walioathirika na ukonjwa wa ukimwi
  • Pia tunatoa elimu rika
  • Tuna elimisha jamii juu ya mpango wa uzazi na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi
  • Kutoa misaada ya hali na mali kwa watoto walio katika mazingira magumu ili waweze kupata mahitaji ya elimu ya msingi kama vile kalamu, daftari na mavazi.

 

  1. Mradi wa ushonaji:
  • Mradi huu unatoa mafunzo ya ushonaji kwa wasichana waliokatika mazingira magumu ili baadaye waweze kujiajiri wenyewe.
  • Mradi huu umefikisha muda wa mwaka mmoja sasa.

 

  1. Mradi wa kujenga uchumi:
  • Mradi huu unalenga kuwajengea akina mama wanachama wa TWG mbinu za kujikimu kimaisha.
  • Mradi huu unaendeshwa kwa michango ya wanachama ya kila mwezi