Envaya
Parts of this page have been translated from Swahili to English. View original · Edit translations

25/06/2010

                         MATATIZO YA KIKUNDI

Wanachama tulitukutana kujadili tatizo la UKOSEFU WA OFISI YA KIKUNDI.

Kwani mpaka sasa shughuli zote za kikundi zinafanyika SEBULENI kwa Mwenyekiti hivyo kupunguza ufanisi wa shughuli za kikundi.Pia ukosefu wa vitendea kazi unarudisha nyuma shughuli za kikundi.Kikundi kinaomba kuwezeshwa kupatiwa Ofisi na Vitendea kazi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za kikundi.

10/06/2010

Wanakikundi wa TUPENDANE walimtembelea bwana KIKA MJATA mzalishaji wa mafuta ya Ubuyu.Tuliweza kuona hatua kwa hatua za uzalishaji wa mafuta hayo,ambayo yamethibitika kuongeza idadi ta CD4 kwa haraka sana na kupunguza idadi ya VVU mwilini.

05/06/2010

Wanachama walikutana kuangalia uwezekanowa kuanzisha mradi wa pamoja ili waweze kujikimu na ugumu wa maisha.

Kwani mpaka sasa tuna miradi ya mtu mmoja mmoja inayotuwezesha kujikimu na ugumu wa maisha.Kuna wanakikundi wanaofanya shughuli mbalimbali kama

1:Ushonaji

2:Mama lishe

3:Uuuzaji wa mitumba,viatu na mapambo ya nyumbani

4:Usukaji wa nywele

5:Uuzaji wa samaki wa kukaanga na mbogamboga

tarehe 25/04/2010
kulitokea msakowa wafanya biashara ndogo ndogo katika manispaa ya dodoma .Hii ilikuwa imelengwa kwa watu wote ambao wanafanya biashara katika kituo cha mabasi ya usafirishaji mjini (Daladala)
Miongoni mwa waathirika katika zoezi hili walikuwepo wanachama wa kikundi chetu ambao wanafanya biashara ya samaki,nguo,viatu na mapambo ya nyumbani.
Waachama wetu wamepoteza baadhi ya mali zao ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika kujikimu kimaisha na kuwapatia mahitaji yao yote ikiwemo lishe.

27/04/2010
Wanaachama walipita mitaani kuomba msaada ili kumnusuru mwanachama mwenzetu ambaye alipata ajali ya kuanguka na pikipiki na kuvunjika mguu pamoja na majeraha makubwa usoni.
Michango hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kumfanya apate matibabu sahihi,, tunatoa shukurani zetu kwa watu wote waliotuwezesha kwa michango mbalimbali

28/05/2010
Wanakikundi walihudhuria semina iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma katika ukumbi wa Mambo Poa
Semina hiyo ilikuwa ni kuhusu lishe bora na matumizi sahihi ya ARV. Kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya chakula na dawa kwa waathirika wa VVU/UKIMWI na KIFUA KIKUU(TB).
Katika semina hiyo tulijifunza na kufahamu mambo mapya kuhusu VVU na Lishe bora. Pia ilikuwa nafasi nzuri ya kufahamiana na wenzetu wanaoishi na VVU, Katika semina hii tulianzisha mtandao unaoitwa WAVIU ili kufarijiana,kupeana moyo na mshikamano miongoni mwetu.

29/05/2010
Mwenyekiti wa kikundi chetu alihudhuria mkutano wa kila mwezi wa kamati ya maboresho ya huduma za CTC, Katika Hospitali kuu ya Mkoa kwakua yeye ni mjumbe wa kamati hiyo.

05/06/2010
Mwekiti wa TUPENDANE alihudhuria semina iliyoandaliwa na ENVAYA ili kuyawezesha mashirika kuwa na tovuti zao.
Wakufunzi wa ENVAYA walitufundisha namna ya kuweka habari zetu katika tovuti ili kufanya shirika letu kufahamika zaidi .
Wakufunzi wa ENVAYA akiwemo Bi.Radhina Kipozi walituelekeza vizuri namna ya kufungua tovuti na namna ya kuweka habari. Na kwamba huduma hii ni bure
Tunawashukuru ENVAYA kwa msaada mkubwa waliotupa kwa kuwa tusingeweza kuwa na tovuti yetu kutokana na ukubwa wa gharama za kuendesha tovuti.
The head of TUPENDANE GROUP has eye pain from being infected. She has been advised to go to Mvumi Admission Hospital to receive treatment. We, her companions of TUPENDANE GROUP, ask for her to get better quickly so that the work of Tupendane may continue.