Base (Swahili) | English |
---|---|
HABARI ZA UTAWALA BORA. Katika mapambano ya kupunguza umasikini,ujinga na maradhi utawala bora na nyenzo mhimu katika mapambano haya. Lakini unaweza kushanga kusikia kuwa tangu uchaguzi umemalizika kuna kijiji kimoja hakina serikali kwa mda wa miezi kadhaa na hivyo kusababisha maendeleo ya eneo husika kuzorota kutokana na maswala ya kisiasa tu. Kijiji kimoja katika wilaya Mvomero tarafa ya Turiani na Kata ya Dingoya kinachojulikana kwa jina la Lusanga hakina serikali kutoka na kujiuzuru kwa serikali iliyokuwepo ya chama cha mapinduzi na kumuacha mwenyekiti wa chama cha cuf akibakia pekee bila serikali na hivyo kuwa na wakati mgumu wa kutoa maamuzi yanayohusu maendeleo ya kijiji hicho. Kijiji hiki ni moja ya vijiji vyenye miradi mingi toka wahisani mbalimbali pamoja na serikali lakini miradi hiyo haitekelezwi kwa ufanisi na viwango vinavyohitajika hii ni kutokana na utawala duni wa kijiji hicho. Mfano ni mradi wa soko na maji ambayo kwa pamoja viligharimu kiasi cha sh 160 milioni hivi, lakini utekelezaji wake ni wa kiwango cha chini mno kiasi cha soko kuanza kubomoka kabla hata halijatumiwa au kufunguliwa, wakati maji yenyewe bado ni kitendawili katika kijiji hicho, wanawake hukaa visimani hadi saa 6 usiku wakisubiri kuchota maji na hivyo kushindwa kufanya kazi za maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. MAZINGIRA. Je wajua kuwa ile dhahabu ya miti iitwayo mitiki inapatikana katika kijiji hicho cha Lusanga na vijiji vingine vya Kunke,Dihinda na Madizini lakini wananchi wake ndio wanaongoza kwa umasikini illihali mrahaba wa msitu huo ukiishia mifukoni mwa wachache wenye ujanja,hivi karibuni pamekuwa na ugawaji wa cbm kadhaa kwa wananchi ili kushiriki uvunaji shirikishi, kupitia ukurasa huu tutawajulisheni wanaharakati yaliyojili katika mgao huu kama walengwa watapatiwa kipaumbele. Hapa tunamaanisha msitu wa mitiki mtibwa. UTETEZI Ukizungumza juu ya ukeketaji watu wengi wanamulika mikoa ya Mara,Arusha,Dodoma, Kilimanjaro na Manyara. Lakini aminiusiamini mkoa wa Tanga unaoongoza kwa ukeketaji pia, pana ukeketaji wa kisiri sana kwa kabila la wazigua kwani kitendo cha kumuweka mwali ndani huambatana na ukeketaji ambao huwa siri kubwa sana kwa wahusika kiasi cha kutishwa ikiwa atatoa siri ya ngoma hiyo ya mwali. Huu ni utafiti uliofanywa na asasi yetu kwa mda mrefu na kubaini matokeo, hivyo tunajulisha wapendwa wanaharakati kuelekeza jitihada za kwatetea wanawake katika maeneo husika katika mkoa wa Tanga na Morogoro kwani sisi pekee hatuwezi kutoshereza huduma hii japo tunaifanya sasa. |
NEWS OF GOOD GOVERNANCE. In the struggle to reduce poverty, ignorance and disease governance and essential tools in this struggle. But you can hear the beads that since the election has concluded there is no village government for a period of several months and thus lead to the development of the area to deteriorate due to political issues only. Village in the district Mvomero division Turiani and Ward Dingoya known by the name of Lusanga no government from the kujiuzuru government that was the party of revolution and let the chairman of the party cuf he remained alone without government and hence have a hard time making decisions about development of the village. This village is one of the villages contain many projects from various donors and government but the project is not being honored for efficiency standards required by this rule is due to poor village. An example is a project to market and water, which together cost about Sh 160 million in this, but its implementation is less so the market started crumble before it lijatumiwa or released, while the water itself is still a mystery in the village, the women sit wells up to 6 hours at night waiting to fetch water and so fail to work in community development and nation as a whole. ENVIRONMENT. Did you know that the gold of trees called Tiki available in the village of Lusanga and other villages with Kunke, Dihinda and Madizini but its citizens are the ones who ran for poverty illihali royalty of the forest if you end up pockets of the few who are cunning, recently there has been redistribution of cbm several people to share collaborative harvesting, through this page will be made known activists yaliyojili in this allocation will be given priority as beneficiaries. Here we mean a forest of Tiki Mtibwa. ADVOCACY Speaking on FGM many people shine Mara, Arusha, Dodoma, Kilimanjaro and Manyara. But aminiusiamini Tanga region leading to mutilation as well, no mutilation of the highly secretive tribe wazigua as the act of putting him in a flame accompanied by mutilation, which is very big secret to the characters so much shocked as to render it a secret dance of flame. This is a study conducted by the institutions of our long-term and identify the results, so we inform loved ones activists focusing efforts kwatetea women in areas in the region of Tanga and Morogoro as we only can we can be satisfied with this service even though we made it now. |
Translation History
|