Base (Swahili) | English |
---|---|
DIRA THEATRE GROUP (DTG) ni asasi ya kiraia ambayo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa mwaka 2006 kwa No.BST/2560 chini ya sheria No. 23 ya mwaka 1984. Kutokana na aina hii ya usajili Dira imeruhusiwa kufanya kazi zake mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kushiriki katika mialiko mbalimbali ya nje ya nchi. Kuanzishwa kwa Dira kulitokana na mwamko/uelewa mdogo wa jamii katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani katika nyanja za elimu, afya, uchumi na utamaduni hali inayoifanya iendelee kuwa na maisha duni. Katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii, Dira imejikita zaidi katika kupambana na vyanzo vya matatizo kama Elimu, Magonjwa, Umaskini wa kipato na migogoro mbalimbali katika jamii. Katika kutekeleza dhima hiyo Dira imetekeleza miradi na shughuli mbalimbali katika maeneo tofauti. Miongoni mwa miradi hiyo ni Utawara bora kwa viongozi wa vijiji, Elimu ya jinsi na jinsia, Elimu kuhusu magonjwa mbalimbali, Athali za dawa za kulevya, Athari za rushwa katika jamii, Sera na sheria za ardhi, Maadili ya utumishi wa umma, Haki na wajibu wa jamii katika chaguzi,Utunzaji wa mazingira, Kukuza vipaji vya watoto mashuleni, Sanaa kwa maendeleo n.k. DIRA Kuwa na jamii yenye uwezo na ari ya kupambana na changamoto mbalimbali zinazoikabili na kuwa na maisha bora. LENGO Kuhimiza, kusukuma na kusaidia maendeleo ya jamii. Kielimu, Kiuchumi na kiutamaduni ili iweze kupambana na changamoto mbalimbali zinazoikabili. MADHUMUNI Kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia njia mbalimbali kama vile Semina, Warsha, Makongamano na Sanaa shirikishi kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa, umaskini, haki, mazingira n.k. Kuongeza uwezo wa jamii hususani wasanii ili waweze kutumia sanaa zao (sanaa za maonyesho, na sanaa za ufundi) kuboresha maisha yao na kukuza utamaduni wetu. Kuihamasisha jamii kutoa malezi bora kwa watoto ili kuwajengea mazingira mazuri ya maisha yao ya baadae. Kufanya mahusiano mema miongoni mwa asasi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Kusaidia jamii kwa njia mbalimbali katika kumbana na tatizo la umaskini wa kipato.
|
DIRA THEATRE GROUP (DTG) is Community Based Organization (CBOs) that established on year 2005 na registered on year 2006 with reg. No.BST/2560 under Law Act No. 23 of year 1984. According to that kind of registration, Dira Theatre is allowed to do its activities anywhere within Tanzania Mainland also to attend any invitations from outside the Tanzania. Establishment of Dira Theatre was due to poor community awareness in dealing with various challenges most especially in various sectors like Education, Health, Economics and Culture which made them still having poor life. In order to ensure Community Development is achieved, Dira Theatre engaged in combating the social problems like deseases, poverty, other social conflicts in the community. By implementing that, Dira Theatre has been implemeting some projects in differents areas within Tanzania. Among of those Projects are; Good Governance to Local authorities, Sex and Gender Education, Education About Various Diseases, Effects of Drugs Abuse, Effects of Corruption in Comminuty, Land Laws and Policies, Code and Ethics of public Services, Rights and Duties of Community in General Election, Environmental Conservation and Protection, Rise School Children Talents, Arts for Development...etc VISION To have a Community with ability and eager to deal and tackle various Challenges that facing them so as to have better life. GOAL To speed up, pushing and help the Community in improving Economically, Socially and Education in order to deal with various Challenges. OBJECTIVES To provide Education to Community by through conducting some seminars, workshops and Artwork by participation in order to defy diseases, poverty etc. To rise ability of Community especially artists so to be able to apply their Artwork to improve they are lives and grow our Culture To create better relation among other Community Based Organizations (CBOs) and various stakeholders in and outside the Tanzania. To help the Community in various ways in combating the problem of Poverty.
|
Translation History
|