Envaya

Dira Group

Amateka

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

DIRA THEATRE GROUP (DTG) ni asasi ya kiraia ambayo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa mwaka 2006 kwa No.BST/2560 chini ya sheria No. 23 ya mwaka 1984. Kutokana na aina hii ya usajili Dira imeruhusiwa kufanya kazi zake mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kushiriki katika mialiko mbalimbali ya nje ya nchi.

Kuanzishwa kwa Dira kulitokana na mwamko/uelewa mdogo wa jamii katika  kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani katika nyanja za elimu, afya, uchumi na utamaduni hali inayoifanya iendelee kuwa na maisha duni.

Katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii, Dira imejikita zaidi katika kupambana na vyanzo vya matatizo kama Elimu, Magonjwa, Umaskini wa kipato na migogoro mbalimbali katika jamii.

Katika kutekeleza dhima hiyo Dira imetekeleza miradi na shughuli mbalimbali katika maeneo tofauti. Miongoni mwa miradi hiyo ni Utawara bora kwa viongozi wa vijiji, Elimu ya jinsi na jinsia, Elimu kuhusu magonjwa mbalimbali, Athali za dawa za kulevya, Athari za rushwa katika jamii, Sera na sheria  za ardhi, Maadili ya utumishi wa umma, Haki na wajibu wa jamii katika chaguzi,Utunzaji wa mazingira, Kukuza vipaji vya watoto mashuleni, Sanaa kwa maendeleo n.k.

DIRA

Kuwa na jamii yenye uwezo na ari ya kupambana na changamoto mbalimbali zinazoikabili na kuwa na maisha bora.

LENGO

Kuhimiza, kusukuma na kusaidia maendeleo ya jamii. Kielimu, Kiuchumi na kiutamaduni ili iweze kupambana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.

MADHUMUNI

Kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia njia mbalimbali kama vile Semina, Warsha, Makongamano na Sanaa shirikishi kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa, umaskini, haki, mazingira n.k.

Kuongeza uwezo wa jamii hususani wasanii ili waweze kutumia sanaa zao (sanaa za maonyesho, na sanaa za ufundi) kuboresha maisha yao na kukuza utamaduni wetu.

Kuihamasisha jamii kutoa malezi bora kwa watoto ili kuwajengea mazingira mazuri ya maisha yao ya baadae.

Kufanya mahusiano mema miongoni mwa asasi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Kusaidia jamii kwa njia mbalimbali katika kumbana na tatizo la umaskini wa kipato.