Envaya

/WAENDELEE/history: English: WIh7GFkV4uIIY03fe3WquiPc:content

Base (Swahili) English

Chimbuko la WAENDELEE ni fikra, tafakuri na mawazo ya muda mrefu yaliyotokana na majadiliano na mazungumzo kuhusu hali halisi ya maendeleo duni na maisha ya Wirwana na Wairwana. Changamoto zilizopo katika jamii yetu huko Singida, Kielimu, Kiafya, Uduni wa miundombinu ya barabara, Uharibifu wa mazingira, kilimo duni na ufugaji wa mazoea usio na tija.  Mambo haya yalipelekea kupatikana wazo la kuanzisha Group  la WhatsApp lijulikanao kama Team Wirwana ambapo wairwana walianza kujadili masuala mbalimbali ya Wairwana mwanzilishi wa kundi hili akiwa ndugu MLALI ABEID IRUNDE ambaye alikuwa mwenyekiti. Baada ya majadiliano ndiyo ikakubalika tuanzishe jumuiya ya uwezeshaji na maendeleo (WAENDELEE) ili tuweze kutimiza ndoto zetu kwa kushirikiana na wanajamii walioko Singida na mamlaka mbalimbali. Jumuiya hii ni ya Wanasingida Vijijini walioko sehemu mbalimbali za nchi na dunia kwa ujumla na ni wanataaluma wa fani mbalimbali. Kwa kutumia taaluma hizi tumeamua tuanze kuboresha hali za kimaisha za sehemu tulikotoka.

Malengo Makuu

  1.  Kuendeleza na kukuza uchumi na maendeleo ya watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo kiuchumi, afya, kijamii na kiutamaduni.
  2. Kusaidia na kuwatambua watu wanaoishi nje ya Singida Vijijini ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.
  3. Kutengeneza umoja na mshikamano baina ya wale waliotoka Singida Vijijini na kuwaunganisha ili waweze kuwekeza katika maendeleo

 Malengo Mengineyo

  • Kuibua na kutambua fursa zilizopo Singida ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili ziwaletee wananchi maendeleo

  • Kushiriki katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji huko Singida sehemu zenye vyanzo vya maji kama vile Ntambuko.

  • Kuhamasisha upatikanaji wa Elimu bora kwa wananchi wetu

  • Kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti,kutunza vyanzo vya maji ili kukomesha ukame na hali ya jangwa wirwana.

  • Kuhamasisha kilimo cha kisasa na ufugaji bora.

  • Kutengeneza mtandao (networking) kwa wale wote ambao wako maeneo tofauti tofauti duniani katika kujenga Singida.

 

Sisi kama wanajumuiya wa  Singida tunaamini jamii yoyote popote pale wanaunganishwa kwa karibu na mazingira halisi waliomo. Shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kiwango kikubwa zinafanyika kutokana na mchanganyiko wa mali asili mbalimbali zilizopo kwenye eneo husika, jiografia ya eneo, hali ya hewa, mabadiliko ya hali za kiasili na tabia mbalimbali za kimazingira.Kwa hiyo mazingira bora yanaboresha uchumi na ustawi wetu wana Singida, tuyalinde yasichafuliwe na kuharibiwa.

Kwa maana hiyo jumuiya

  • Ilianzisha mradi wa kuotesha na kupanda miti Wilaya nzima ya Halmashauri ya Singida kuanzia msimu wa 2015/2016 na kuwezesha kupandwa kwa miti zaidi ya 150,000. Kwa msimu wa 2016/2016 jumuiya imeaanda bustani za kuotesha miti zaidi ya 40 ili kuotesha miti zaidi 1,400,000.
  • Imekuwa bega kwa bega na Halmashauri ya Singida katika kuboresha hali za kimaisha za wananchi wa Singida kama kupambana na maradhi mbalimbali kama kipindupindu na kushiriki kwenye programu za usafi wa mazingira.
  • Inashiriki katika kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari kwa kuangalia uwezekano wa kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
  • Inaendelea kuangalia uwezekano wa kushiriki katika kuboresha hifadhi za mazingira na mabwawa mbalimbali yaliyoko Singida.
  • Inandaa utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi ili kuwapa ufahamu wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Jumuiya ina uongozi wake ambapo ina Bodi ya Wakurugenzi, Mtendaji Mkuu, Waratibu wa Idara na Waratibu wa programu mbalimbali kwenye Tarafa tatu za Wilaya ya Singida.


(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register