Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Chimbuko la WAENDELEE ni fikra, tafakuri na mawazo ya muda mrefu yaliyotokana na majadiliano na mazungumzo kuhusu hali halisi ya maendeleo duni na maisha ya Wirwana na Wairwana. Changamoto zilizopo katika jamii yetu huko Singida, Kielimu, Kiafya, Uduni wa miundombinu ya barabara, Uharibifu wa mazingira, kilimo duni na ufugaji wa mazoea usio na tija. Mambo haya yalipelekea kupatikana wazo la kuanzisha Group la WhatsApp lijulikanao kama Team Wirwana ambapo wairwana walianza kujadili masuala mbalimbali ya Wairwana mwanzilishi wa kundi hili akiwa ndugu MLALI ABEID IRUNDE ambaye alikuwa mwenyekiti. Baada ya majadiliano ndiyo ikakubalika tuanzishe jumuiya ya uwezeshaji na maendeleo (WAENDELEE) ili tuweze kutimiza ndoto zetu kwa kushirikiana na wanajamii walioko Singida na mamlaka mbalimbali. Jumuiya hii ni ya Wanasingida Vijijini walioko sehemu mbalimbali za nchi na dunia kwa ujumla na ni wanataaluma wa fani mbalimbali. Kwa kutumia taaluma hizi tumeamua tuanze kuboresha hali za kimaisha za sehemu tulikotoka. Malengo Makuu
Malengo Mengineyo
Sisi kama wanajumuiya wa Singida tunaamini jamii yoyote popote pale wanaunganishwa kwa karibu na mazingira halisi waliomo. Shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kiwango kikubwa zinafanyika kutokana na mchanganyiko wa mali asili mbalimbali zilizopo kwenye eneo husika, jiografia ya eneo, hali ya hewa, mabadiliko ya hali za kiasili na tabia mbalimbali za kimazingira.Kwa hiyo mazingira bora yanaboresha uchumi na ustawi wetu wana Singida, tuyalinde yasichafuliwe na kuharibiwa. Kwa maana hiyo jumuiya
Jumuiya ina uongozi wake ambapo ina Bodi ya Wakurugenzi, Mtendaji Mkuu, Waratibu wa Idara na Waratibu wa programu mbalimbali kwenye Tarafa tatu za Wilaya ya Singida. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe