TEYODEN yakamilisha shughuli ya ufuatiliaji wa shughuli za vijana katika vituo 7 vya vijana kati ya vituo 12 vya mradi manispaa ya Temeke.
- UTANGULIZI
TEYODEN ipo katika kipindi cha utekelzaji wa mradi wa kuinua ari ya uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kimaendeleo na za kijamii.Mradi huu unafanyika katika kata 12 za Manispaa ya Temeke.Katika robo hii ya kwanza ya mradi shughuli 2 zimefanyika ambazo ni utambulisho wa mradi kwa wadau wa maendeleo 26 Manispaa ya Temeke na Mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwa vijana 40,24 kutoka vituo vya vijana, 12 vya kata na 12 kutoka asasi za vijana na 8 taasisi nyingine zilizopo Manispaa ya Temeke.Taarifa hii inatoa picha halisi ya mwendelezo wa mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana kwa vijana wengine katika kata kama matokeo ya mafunzo yaliyoendeshwa na makubaliano ya waandaaji wawezeshaji na vijana 40 walioshiriki mafunzo hayo.Hii ni taarifa ya shughuli ya ufuatiliaji katika kata 7 ambazo ni:- Sandali, Azimio, Vijibweni, Somangila, Kimbiji, Charambe na Yombo vituka.
- LENGO LA ZIARA YA UFUATILIAJI
-Lengo la shughuli hiini kupata takwimu na taarifa za vijana juu ya usambazaji wa sera ya vijna na stadi za maisha kwa vijana wengine katika kata.
Lakini pia kuweka mazingira mazuri ili vijana waweze kupokea jukwaa la vijana katika kata husika.
- KATA ZA MRADI ZILIZOTEMBELEWA
Tarehe |
kata |
Tarehe |
Kata |
29/1/2011 |
Somangila |
4/2/2011 |
Vituka |
29/1/2011 |
Vijibweni |
5/2/2011 |
Charambe |
30/2/2011 |
Kimbiji |
13/2/2011 |
Azimio |
31/1/2011 |
Sandali |
|
|
- KATA AMBAZO BADO HAZIJATEMEBELEWA
Tarehe |
kata |
Tarehe |
Kata |
|
Makangarawe |
|
Mjimwema |
|
Tandika |
|
Chang’ombe |
|
kibada |
|
|
- SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
- Vikao vya vijana vya kituo
- Vikao vya mrejesho vya vijana
- IDADI YA VIJANA WALIOFIKIWA
Kata |
Idadi ya vijana waliofikiwa |
Idadi ya wawezeshaji wanaoendelea |
|||
|
Me |
Ke |
Jumla |
|
|
Somangila |
9 |
14 |
23 |
3 |
- |
Azimio |
30 |
12 |
42 |
3 |
- |
Charambe |
20 |
12 |
32 |
3 |
- |
Sandali |
16 |
11 |
27 |
1 |
2 |
Kimbiji |
20 |
25 |
45 |
3 |
- |
Vijibweni |
7 |
3 |
10 |
2 |
1 |
Vituka |
16 |
14 |
30 |
3 |
- |
Jumla |
118 |
91 |
209 |
18 |
3 |
- MADA AMBAZO VIJANA WAMEZUNGUMZIA KATIKA MIJADALA NA VIKAO VYAO
- Sera ya vijana,stadi za maisha na umuhimu wa jukwaa la vijana.
- ZANA ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA VIJANA
- Chaki,bao na vitini
- MBINU ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA VIJANA ZA KATA
- Majadiliano shirikishi
- Maswali na majibu na visa mkasa
- JINSI MBINU ZILIZOTUMIKA ZILIVYOFAA
- Mbinu shirikishi husaidia vijana kila mmoja kushiriki katika kupanga jambo.
- Mbinu zilizotumika zinaibua hisia za vijana hasa kuzungumzia matatizo yao.
- MAMBO YALIYOIBULIWA KATIKA MIJADALA YA VIJANA
- Vijana hawajui namna ya kujiunganisha ili kujenga timu jambo ambalo ni muhimu sana katika kufanya jambo Fulani libadilike.
- Vijana hawana mbinu za namna ya kujenga hoja zenye ushirikiano wa pamoja ili waweze kusikilizwa.Imeonekana kuwa lazima vijana wawezeshwe kuona umuhimu wa dahana ya kuwa na hoja zenye ushahidi na tija mbazo wakizisimamia watoa maamuzi wataziweka katika mipango ya utekelezaji.
- Umuhimu wa vijana kushiriki katika michezo na burudani limeonekana kuwa ni jambo ambalo litafanya vijana kuwa pamoja na kushirikiana.
- Vijana kuwa na miradi ya pamoja ya uchumi na kuwezeshwa kupata mikopo itakuwa ni njia ya kuwafanya waweze kuitegemea ki uchumi.
- Upatikanaji wa sera ya maendeleo ya vijana ni jambo ambalo vijana wamelisisitiza kwa kuelewa sera itawafanya wawe kwenye nafasi nzuri ya kutetea haki zao.
- MAONO YA VIJANA KUHUSU MRADI WA KUINUA ARI UWJIBIKAJI NA USHIRIKI
- Vijana wanaunga mkono mpango kwa kuwa utawezesha vijana kujitambua,kuwa wathubutu na wenye kuleta tija.
- Vijana wanaona mpango huu utawezesha vijana kushriki kwenye ngazi mablimbali za maamuzi kutoka mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi ngazi ya taifa.
3. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA
- Viwango tofauti vya uelewa wa vijana katika masuala ya kijamii na kikaendeleo vinapunguza kasi ya mpango wa uwajibikaji na ushiriki kufanya kazi ipasavyo.
- Vijana wa mitaa michache wameshirikishwa katika hatua za awali za mpango
- Dhana ya kutojiamini miongoni mwa vijana.imejionyesha katika baadhi ya kata pamoja na kuwezeshwa kwa muda wa siku 6 bado baadhi ya vijana wameshindwa kufanya uwasilishaji wa mada ipasavyo kwa vijana wenzao
- Ukosefu wa vindea kazi umefanya uwaslishaji wa elimu kwa vijana kuwa mgumu kiasi.
- Kasi ya vijana kujiunga kama timu na kuanza kujenga hoja imekuwa ndogo ukilinganisha na mawazo ya awali wakati wa mafunzo.
- Ushiriki mdogo wa vijana katika baadhi ya kata mfano kata ya Vijibweni vijana 10 tu walishriki badala ya wastani wa vijna 30 kwa kila kata.
- Ushiriki mdogo wa jinsia ya kike na mwamko wao katika kuchangia masuala ya kimaendeleon aya kijamii umekuwa mdogo.
- MAPENDEKEZO YA NAMNA YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
- Kutoa taarifa kwa uongozi wa kata kabla ya kuanza shughuli za vijana katika kata.Hii itasaidia kupata ushiriki wa vijana kutoka mitaa yote ya kata husika.
- Kushirikisha vijana katika mitaa yote ya kata husika katika shughuli zao ili kuleta maamuzi ya pamoja.
- Wahusishe hata kempu za vijana na maendeo mengine ili kupata idadi kubwa ya vijana katika kata.
- Ofisi ya mtandao iwe na programu maalumu ya kutembelea kataza mradi ili kuwaongezea kujiamini vijana.
- Ofisi ya mtandao kua na mawasiliano ya moja kwamoja na mtendaji wakata ili kujua kama yapo mahusinao ya karibu n kubadilishana mawazo na vijana.
- Katika kipindi kijacho cha mradi wasichana watiliwe mkazo zaidi ili kuleta usawa wa kijinsia.
- JINSI MAFUNZO YALIVYOSAIDIA VIJANA
Pamoja na madhaifu madogo madogo yaliyojitokeza kwa baadhi ya kata za mradi
Yapo mafanikio makubwa yaliyotokana na mafunzo na shughuli za mradi.
- Mafunzo yamefanya vijana waliyoyapata kuamsha ari kwao katika kujitambua na kufahamu haki zao pamoja na kujenga hoja.
- Mawasiliano mazuri kati ya viongozi kata na vijana mfano katika kata ya azimio mtendaji wa kata hiyo anafanya vikao na vijana kama hatua ya kutambua na kufanikisha shughuli za vijanan hao.
- Zipo kata ambazo kumekuwa na mwamko wa vijana yaliyovuka kiwango cha makadilio ya vijana yaliyowekwa mafano kata ya kimbiji na azimio.
- HADITHI MAFUNZO
Mpaka katika hatua hii ya mwanzo ya ufuatiliaji bado kulikuwa hakuna kisa mafunzo ha kusisimua kilichoweza kulekodiwa kutoka katika kata za lengwa za mradi lakini tunategemea kupata mengo kutoka katika kata hizo.
- HITIMISHO
Zoezi la ufuatiliaji katika kata 7 za awali ni hatua moja kuelekea katika kumalizia kata nyingine 5 za mradi tunatemea zoezi hili litakamilika mpaka kufikia katikati ya mwezi februari hatua itayotoa picha halisi ya matokeo ya awali katika kipindi hiki cha robo ya kwanza ya mradi.Picha hii imetupa mafunzo makubwa katika kubadili mbinu na taratibu za mradi katika kipindi kijacho cha mradi na ni matumaini yetu makubwa kuwa mrdi utafanya vizuri katika kuzifanya ndoto za vijana kuwa kweli.Ni matumaini yetu kuwa kila ngazi itawajibika vya kutosha katika kuhakikisha ndoto ya mradi huu inakuwa kweli.