TEYODEN yajiandaa kuendesha mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA Temeke
Katika kupambana na umaskini TEYODEN itaendesha mafunzo kupitia midahalo ya kila wiki kwa vijana wake juu ya uanzishaji wa benki za kijamii,maarufu kama VICOBA.
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa njia ya midahalo na mwezeshaji Gabriel Gesine aliyehudhuria mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA yaliyoendeshwa na WWF ofisi ya Tanzania pale Maili Moja,Kibaha.
Mafunzo hayo yalihusisha juu ya uanzishaji wa vikundi,uongozi katika vikundi hivyo,uchaguzi huru,kanuni na taratibu za ununuzi wa hisa na jinsi ya kukopa,mfuko wa jamii,uundaji wa katiba ya kikundi,utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu,ununuzi wa hisa kwa mara ya kwanza,utoaji wa mikopo,ulipaji wa mikopo na jinsi ya utunzaji wa kumbukumbu za kila siku.
Ibitekerezo (1)