Log in
Tanzania Women of Action(Tawa)

Tanzania Women of Action(Tawa)

Dar es salaam, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

             KWA NINI TUNAHITAJI USHIRIKI WA MWNAMKE KATIKA KATIBA MPYA?

Kwa kuwa tunahitaji katiba itakayokidhi matakwa ya mwanamke na mwanaume ,hivyo ushiriki wa makundi yote haya kwa uwiano sawa ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya kweli na kupata katiba itakayosimamia  usawa, haki ,utu na heshima  ya wananchi wake bila kujali jinsia.

   Kutokana na changamoto hii na kwakuzingatia  idadi ya watanzania inayoonyesha kuwa wanawake wana idadi kubwa ikilinganishwa na idadi ya wanaume katika sensa iliyopita inayoonyesha wanawake ni asilimia hamsini na moja ( 51%  )ya watanzania wote ,Hivyo wanawake tunalojukumu la kuwahamasisha wanawake wenzetu walioko pembezoni  ili wajue umuhimu wa katiba ya nchi na waweze kujitokeza kushiriki katika mchakato wa kuandaa katiba mpya kwa kuchangia / kutoa maoni yao.

October 29, 2012
« Previous Next »

Comments (5)

Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
Wanawake wanatakiwa wapate elimu ya uraia ,vile vile wahamasishwe vya kutosha ili waweze kujitokeza katika kutoa miochango yao ya mawazo katika katiba mpya ili kubadilisha mfumo kandamizi dhidi ya mtoto wa kike na (wanawake kwa ujumla.
October 29, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
Tunahitaji katiba itakayotoa fursa na haki sawa kwa mwananchi bila kujali jinsia.(umiliki wa rasilimali za nchi, elimu , ajira, na huduma nyingine za kijamii
October 29, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
Tunasisitiza wanawake wote tujenge nguvu za pamoja bila kujali cheo,elimu uwezo wa kimiliki pesa n,k Vile vile tusibaguane kutokana na jinsi tuhakikishe makundi yote ya wanawake yanashirikishwa( walemavu, wanawake wenye jinsia mbili (intersex0MAJIKE DUME)transgender na wenza wao
October 29, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
Tuondoe ubaguzi miongoni mwetu (wanawake)ili tuweze kuwa na sauti ya pamoja itakayotulea mabadiliko na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi
November 10, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) said:
elimu ya uraia kwa wanawke ni muhimu ili watambue umuhimu wao wa kuchangia na kutoa maoni katika mchakato mpya wa katiba,ili katiba mpya itoe haki na fursa sawa kwa watanzania wote (wanawake ,wanaume)
November 10, 2012

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.