Mradi wa UNASIHI NA UPIMAJI WA HIARI WA VIRUSI VYA UKIMWI ni endelevu, na sasa hivi Asasi imepokea fedha Sh.21,692,190/=(Milioni ishirini na moja mia sita tisini na mbili elfu mia moja tisini) kwaajili ya kufanya mafunzo ya unasihi katika kata Nne za Malatu,Mchemo,Mtopwa na C/Nandwahi. Mradi huu ulionesha mafanikio mazuri kwa kata za Kitangari na Maputi kwasababu baada ya mafunzo hayo kutolewa jamii imeonesha uelewa wa kutaka kujua Afya zao.
Idadi ya watu wanaokwenda kupima kwa hiari kituo cha afya imeongezeka toka watu wawili kwa wiki hadi watu 6 (Sita).
Pia akina mama wajawazito tabia ya kujifungulia majumbani imetoweka kabisa.