SAWATA MARA baada ya kutoa semina juu ya Sera ya Taifa ya Wazee, Ujasiriamari na Sheria Na.1 ya mwaka 2001, ya mfuko wa bima ya Afya ya jamii iliyotolewa katika kijiji cha Mwibagi Kata ya Kyanyari, kwa ufadhili wa "The Foundation For Civil Society" Dar-es-salaam, Tanzania. Semina hii ilitolewa mwezi Agosti, 2011. Na uundaji wa mabaraza ya wazee kwa ngazi ya kijiji na Kata. Vivyo hivyo, Mabaraza haya, yaliundwa katika vijiji mbalimbali kwa Kata nne za Bukima, Nyambono, Kyanyari na Bwiregi, katika kipindi cha Agosti, 2011 hadi Oktoba, 2011.
Wazee baada ya kupata semina juu ya Sera ya Taifa ya Wazee, Ujasiriamari na Sheria Na.1 ya mwaka 2001, ya mfuko wa bima ya Afya ya jamii iliyotolewa katika kijiji cha Nyambono Kata ya Nyambono, kwa ufadhili wa "The Foundation For Civil Society" Dar-es-salaam, Tanzania. Semina hii ilitolewa mwezi Agosti, 2011. Vile vile ilitolewa katika Kata za Bukima, Kyanyari na Bwiregi, kwa ushirikiano na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini.
Kwenye mradi uliotekelezwa na SAWATA MARA chini ya ufadhili wa "HelpAge International" jamii ilishirikishwa kuwajengea nyumba wazee wasiokuwa na uwezo. Hapa mzee mmoja anajengewa nyumba katika Kata ya Suguti, kijiji cha Kusenyi.
Wezee hawa baada yakupatiwa elimu ya Sera ya Taifa ya wazee, kwenye mradi uliofadhiliwa na "HelpAge International" Dar-es-salaam. Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini, iliwaingiza kwenye miradi ya TASAF ya uvuvi.
Hii ni picha ya wazee baada ya kuvuna pamba kwenye shamba lao la mradi wa pamba waliobuni baada ya uundaji wa mabaraza ya wazee Kata ya Suguti, kijiji cha Wenyere.