Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

KWANINI VIONGOZI WETU WANASHINDWA KUWEZESHA MABADILIKO CHANYA KATIKA NCHI YETU?.

Sakale Development Foundation (Muheza,Kata ya Mbomole)
November 24, 2012 at 5:58 PM EAT

Nchi/Watu lazima iwe na viongozi, huo ni mpango wa mungu.Hakuna ubishi katika hilo, lakini je yeyote aweza kuwa kiongozi? bila shaka jibu ni hapana, hapa ina maana kwamba kuongoza ni kipaji kama ilivyo kwa vipaji vingine ambavyo mwanadamu hujaliwa na mwenyezi mungu.Katika Tanzania siku hizi inaonekana kipaji cha kuongoza kinatokana na utajiri wa mtu na au kama baba/mama akiwa na madaraka wakati huo.Hali hii imetandaa hadi katika kupata ajira. Bahati mbaya jamii imeendelea kunung,unikia hali hii bila kuchukua hatua ili kuleta mabadiliko katika hali hii. Ndugu jamii, Mnataka hamtaki hali itazidi kuwa mbaya siku zetu zote za maisha hapa Tanzania. nasema hivyo kwasababu nyepesi kwa kila mmoja wetu na kwamba haihitaji kuwa na shahada kubaini hilo kwamba viongozi wetu sio wanaostahili.Tunasema uongozi katika jamii ni mpango wa mungu, hivyo njia haramu katika kusaka uongozi hauwezi kuwa mpango wa mungu, kwa hivyo kiongozi anayepata nafasi ya kuongoza kwa njia haramu hawezi kuwa na maono katika kuongoza jamii ili ikabiliane na changamoto zinazo na zitakazo jiri katika jamii husika. Maana yake jamii husika itakumbana na dhiki, na hasa kwa kuwa jamii husika inakuwa imeshiriki  kwa namna moja kuwapa uongozi watu ambao si mpango wa mungu bali kwa kuwa walipokea viperushi vyenye "GUNDI" au kijana kakabidhiwa ofisi kwa kuwa baba/mama yupo katika madaraka.Watanzania na hasa viongozi wetu kama kweli tunataka taifa letu lisonge mbele, basi tuwezeshe taratibu halali na kubalifu kwa jamii ili kupata viongozi na watenda kazi na hizo taratibu zifuatwe. Kwa kufanya hivyo baraka kutoka kwa mungu zitaingia katika taifa letu. na ikiwa hivyo maana yake tutapata watu wenye karama za kuongoza ambao kwa hakika watabuni mbinu zitakazosaidia taifa kuondokana na dhiki.Mtindo uliochukua nafasi katika kujipatia kazi na uongozi ni chukizo mbele za mwenyezi mungu na kwa vyovyote vile utalitumbukiza Taifa katika Vurugu jambo ambalo madhara yake ni kwa taifa zima, kwamba hata hao matajiriri na watoto na wajukuu ambao mnawapa uongozi na kazi hawatakuwa na muda wa kufaidi nafasi hizo.Tanzania itakuwa Kisima/Kisiwa cha Amani na chenye maendeleo ya kiuchumi, siasa na kijamii kama taratibu za kupata viongozi na wafanyakazi zitaheshimiwa na kufuatwa. kwa kuwa ni ukweli tupu kwamba wenye vipaji na ujuzi watapata nafasi na kwakweli lazima wataonyesha tofauti na wengine. Sasa hivi watu wenye vipaji hivyo hawana nafasi ya kuvionesha. Waliopo kwenye nafasi sasa wengi wamefika hapo kwa namna haramu, hawawezi kuonyesha chochote cha maana isipokuwa kufuja kodi za watanzania,kwani hawana maono yoyote."Tuache watu wapambane kwa hoja na ujuzi mwenye kushinda lazima atatuonyesha tofauti za kwanini aliwashinda wenzake".


Add New Message

Invite people to participate