Injira
ST RAYMOND UNIVERSAL  INSTITUTE

ST RAYMOND UNIVERSAL INSTITUTE

MULEBA, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Taasisi ya St.Raymond Universal Institute Chimbuko lake ni huduma ya Glori care yenye makao yake mkoani Shinyanga Tanzania ambayo ilijihusisha na huduma za kijamii ikiwemo mafunzo ya jinsi ya kuendesha  vituo vya malezi ya watoto wadogo{day care center}.

Kufuatana na kupanuka kwa huduma za taasisi ya Glori care Muhasisi mnamo mwaka mwaka 2007 alifungua tawi dogo chini ya Glori Care Mjini Muleba Mkoani Kagera.

Mnamo  mwaka  2010. Huduma iliyotolewa na kituo hiki ni kama ifuatavyo:

-Mafunzo kwa ajili ya vituo vya  malezi ya watoto wadogo.

-Mafunzo ya ujasiliamali ikilenga kuboresha ajira kwa vijana.

-Mafunzo ya Computer {ICT}.

-Elimu ya watu wazima kiwango cha shule za msingi na Sekondari.

-Stadi za maisha ili kupambana na UKIMWI na madawa ya kulevya ikiwemo kuboresha maadili kati ya vijana.

Kituo hiki kufikia mwaka 2012 kilikuwa kimeandikisha vijana 250 katika mafunzo mbalimbali.

Kituo kinashirikiana kwa karibu na Halimashauri ya Wilaya ya Muleba,wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo taasisi zisizokuwa za kiserikali.